Piariz Hizza adaiwa kunyongwa na mumewe mpaka kufariki dunia

Piariz Hizza adaiwa kunyongwa na mumewe mpaka kufariki dunia

Nakumbuka ulianza majaribio 2020

Maana yake una miaka miwili au ulitetereka kidogo
Mkuu, nilikaa kama miezi mitano nikashindwa. Sasa nina miezi kumi na moja sijagusa tena, na ninaendelea poa kabisa.
 
Mkuu, nilikaa kama miezi mitano nikashindwa. Sasa nina miezi kumi na moja sijagusa tena, na ninaendelea poa kabisa.
Bila shaka hata siha yako njema sasa.

Mimi nilifanikiwa kuacha ulevi japo mara chache nikiimiss nalewa ila natulia kipindi kirefu tena bila kugusa
 
Bila shaka hata siha yako njema sasa.

Mimi nilifanikiwa kuacha ulevi japo mara chache nikiimiss nalewa ila natulia kipindi kirefu tena bila kugusa
Mkuu, naendelea vizuri kabisa. Natumaini kuendelea kumaintain hali hii kadri niwezavyo. Kwa mtu ambaye hajapitia janga la ulevi anaweza asielewe ni kwa kiasi gani hili dubwasha (monster) la ulevi lilivyo changamoto kubwa sana
 
Yawezekana kabisa mkuu, alafu wengine wamekuwa wezi kuliko hata hawa wanawake tunaokutana nao mitaani. Yaani mpaka unawaza kama kweli mlioana kwa nia ya kujenga familia au la. Yaani asione pesa mbele yake, unaweka mitego na unamnasa anakwambia nimechukua kidogo tu nilikuwa na shida nayo, na hapo umetoka kumpa hela na biashara umemfungulia.

Nimewahi kushangaa diku moja askari wananifuata kitaa, naambiwa natakiwa kituoni, kufika nawekwa selo hadi kesho yake mchana. Nawauliza kosa ni nini na kwa nini niko hapa, naambiwa utajua kesho. Inafika keho yake mchana wife kafika, napelekwa dawati la jinsia, na shauri linasikilizwa. Naambiwa siuudumii familia, napigwa na butwaa, na mshangao kabisa, anadai anataka ATM kadi yangu,nakumbuka niliwahi kumwachia kadi hiyo nikiwa masomoni nje kwa takribani miaka miwili na nikakuta hakuna hata balance. Usafiri nimemnunulia, mafuta naweka mimi, watoto shule wanasoma nzuri kabisa. yeye mwenyewe nimempeleka shule na ajira nimemtafutia, ameacha ajira anataka bishara. Biashara imemshinda kutwa ni kubadilisha nguo na style za nywele. Natoka selo mchana wa saa nane, napokea simu toka kwa HR, ananambia brother nini tena kimetokea! Mkeo kaja hapa anataka mgawane mshahara 50/50, Naona huyu sasa ana mental kesi au karogwa.

Nikaamua kuondoka nianze maisha mapya, mzee wangu mmoja akanishauri nisiondoke. Akasema kata mirija yote ya pesa na adabu itarudi, kukimbia familia ni laana kwa mila zetu. Nikakata mirija, biashara imecolapse, gari mafuta na hata aservice hakuna. Familia natoa mahitaji yote ya muhimu, ngumu kumeza nikapunguza kabisa. Kwa sasa adabu inarudi na sitorudi nyuma.

Kuna baadhi ya wanawake ni pasua kichwa kwelikweli. unamwambia ondoka ukapumzike kwenu anagoma. Mama mkwe anatetea binti yake balaa. Nayakumbuka maneno ya mama, miaka takribani 17 nyuma, akinikanya kuwa huyu unayemuoa atakusumbua. Nabaki kukumbuka na kusikitika sana.
Mkuu naomba uandike huu uzi tafadhali kuna somo hapa
 
Mkuu naomba uandike huu uzi tafadhali kuna somo hapa
Ha hahahahaha, Mkuu nimegusia machache sana, nikisema niandike mengi zaidi nitajulikana na hapa tunatumia ID fake. Kwa kipindi hiki ambako mambo ya kifamilia yameanza kuwa stable, ni busara kutokuandika kwa undani.
Kuna siku huko mbeleni tukijaliwa uhai nitajaribu kuandika, kwani ninaweza kutoa makala kabisa. Sijasema matukio makubwa yaliyonikuta ughaibuni na kuninyima fursa ya kazi FAO. Ukisoma huu uzi utaona baadhi ya mikasa niliyokutana nayo
 
Back
Top Bottom