Piariz Hizza adaiwa kunyongwa na mumewe mpaka kufariki dunia

Piariz Hizza adaiwa kunyongwa na mumewe mpaka kufariki dunia

Daah! Aisee watoto bado wadogo sana wameachwa ,
pole kwa familia yake
 
Mnapenda wanawake weupe sana,wabongo wanaangalia rangi,hapo lazima ulale na viatu,kesi nyingi ni wanawake weupe,jamaa aliyempiga risasi mkewe mwanza alikua mweupe,Mke wa Masanja ni mweupe,Ba mdogo wangu alijinyonga mke wake alikua mweupe,Tuoe wa kawaida Sio hawa Azam Burudani kwa wote
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] Azam
 
Yawezekana kabisa mkuu, alafu wengine wamekuwa wezi kuliko hata hawa wanawake tunaokutana nao mitaani. Yaani mpaka unawaza kama kweli mlioana kwa nia ya kujenga familia au la. Yaani asione pesa mbele yake, unaweka mitego na unamnasa anakwambia nimechukua kidogo tu nilikuwa na shida nayo, na hapo umetoka kumpa hela na biashara umemfungulia.

Nimewahi kushangaa diku moja askari wananifuata kitaa, naambiwa natakiwa kituoni, kufika nawekwa selo hadi kesho yake mchana. Nawauliza kosa ni nini na kwa nini niko hapa, naambiwa utajua kesho. Inafika keho yake mchana wife kafika, napelekwa dawati la jinsia, na shauri linasikilizwa. Naambiwa siuudumii familia, napigwa na butwaa, na mshangao kabisa, anadai anataka ATM kadi yangu,nakumbuka niliwahi kumwachia kadi hiyo nikiwa masomoni nje kwa takribani miaka miwili na nikakuta hakuna hata balance. Usafiri nimemnunulia, mafuta naweka mimi, watoto shule wanasoma nzuri kabisa. yeye mwenyewe nimempeleka shule na ajira nimemtafutia, ameacha ajira anataka bishara. Biashara imemshinda kutwa ni kubadilisha nguo na style za nywele. Natoka selo mchana wa saa nane, napokea simu toka kwa HR, ananambia brother nini tena kimetokea! Mkeo kaja hapa anataka mgawane mshahara 50/50, Naona huyu sasa ana mental kesi au karogwa.

Nikaamua kuondoka nianze maisha mapya, mzee wangu mmoja akanishauri nisiondoke. Akasema kata mirija yote ya pesa na adabu itarudi, kukimbia familia ni laana kwa mila zetu. Nikakata mirija, biashara imecolapse, gari mafuta na hata aservice hakuna. Familia natoa mahitaji yote ya muhimu, ngumu kumeza nikapunguza kabisa. Kwa sasa adabu inarudi na sitorudi nyuma.

Kuna baadhi ya wanawake ni pasua kichwa kwelikweli. unamwambia ondoka ukapumzike kwenu anagoma. Mama mkwe anatetea binti yake balaa. Nayakumbuka maneno ya mama, miaka takribani 17 nyuma, akinikanya kuwa huyu unayemuoa atakusumbua. Nabaki kukumbuka na kusikitika sana.
Shida hamsikilizi wazazi wenu Wana maono sana
 
Sasa imebaki majuto ni mjukuu, kuna siku ningeishia sero, ilinaki kidogo nimtoboe toboe na mkasi uliokuwa mezani. Mzee wangu mmoja anagonga mlango hodi, kungia namuona kaongozana na balozi. Kesi inaibuka, anamdai mke wangu zaidi ya 2M. Alipokuwa anafanya biashara alikuwa anaenda kuchukua malighafi kwenye duka la jumla la huyu mzee. Mzee mwenyewe alikuwa ananiamini sana na ndiye aliyenipokea ofisini na kunisaidia pia kwenye biashara, mashamba na ushauri mwingine kibao.

Huyu mzee alikuwa ananiamini sana, so wife anachukua malighafi kwa mali kauli, huku nyuma ananipanga namtumia hela ya kumuongezea mtaji, kumbe madeni lukuki. Namuomba mzee wangu arudishe moyo nyuma, nampa nusu ya pesa na kumuahidi nyingine mwisho wa mwezi. Siku si nyingi nawaona VICOBA wamefika, wanadai 4.9M, nauliza alikopa za nini na mimi akunishirikisha, anasema huoni vitu nivyofanya! nauliza umefanyia nini? Nawaambia VICOBA siutambui huo mkopo na sikushirikishwa.

Hayo yote yamebaki historia, adabu imerudi, hagusi hata shilingi yangu moja, amekuwa mama house 100% na mahitaji yote anapata. Nabaki kuwaza, siku nikizima, watoto watapoteza mwelekeo jumla, kwani huyu ni mwanamke asiyejitambua. Nabaki kuomba japo niwepo hata kwa miaka kadhaa ijayo niwasogeze watoto kielimu.
[emoji849]kumbe Hawa wanawake wapogi, nilikuaga najua visa TU vya kusadikika eti
 
[emoji849]kumbe Hawa wanawake wapogi, nilikuaga najua visa TU vya kusadikika eti
Mkuu, hawa wapo kabisa, na niliyosimulia ni machache sana. Niliwahi kuchangia comments nyingi kwenye uzi huu hapa Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Kiufupi mengi sijayaongea lakini haya nililiyosema yamenipata mimi binafsi, na yalipelekea nikabobea kwenye ulevi uliopitiliza. Sasa niko poa kabisa na maisha yanaenda.
 
Shida hamsikilizi wazazi wenu Wana maono sana
Wengi tukiwa vijana na ukaenda shule kidogo tunawaona wazazi kama wamepitwa na wakati. Maza alitaka kunipa laana. Alinitembelea na akakutana na huyu mwanamke. Kiufupi alitoka nje na kusema hakubaliani na uamuzi wangu. Akiwa ameegemea kwenye kabila la huyu mwanamke, mama akasema hapana na akatoa hadi machozi. Kiufupi alikuwa sawa, na alikuwa sawa kabisa.
 
Wengi tukiwa vijana na ukaenda shule kidogo tunawaona wazazi kama wamepitwa na wakati. Maza alitaka kunipa laana. Alinitembelea na akakutana na huyu mwanamke. Kiufupi alitoka nje na kusema hakubaliani na uamuzi wangu. Akiwa ameegemea kwenye kabila la huyu mwanamke, mama akasema hapana na akatoa hadi machozi. Kiufupi alikuwa sawa, na alikuwa sawa kabisa.
Kumbe huyu mwanamke ndo sababu!?

Vipi unaendeleaje sasa na unywaji?
 
Kumbe huyu mwanamke ndo sababu!?

Vipi unaendeleaje sasa na unywaji?
Mkuu niko vizuri kabisa, kwa sasa situmii tena kilevi. Nitajitahidi kumaintain hili kwani nimerudi kwenye line zangu kitambo kidogo.
 
Ikifika hatua serekali ikaanza kuchukua hatua kali kwa hawa wanaoua watu kwa kesi za mapenzi ndipo haya mambo yatakapopotea.
Kwa hali tulionayo sasa Mtu anaua na bado anafanywa ndio shujaa jamii hayataweza kuisha kamwe.
 
Back
Top Bottom