Hilo sasa ni jukumu lako kama mzazi kumtafutia mwanao ni wapi sehemu sahihi ya kwenda kuchukua Dini yake. Na kumsimamia na kumfuatilia. Watu tunazembea tu katika Dini na kuichukulia poa. Nitatoa mfano kwa Dini yangu ya Uislam, huku wapo wazazi hawajali mtoto anasoma Dini sehemu gani, usahihi wa elimu anayosoma na hali ya wafundishaji. Hii ni kwa sababu hawajajua umuhimu wa Elimu ya Dini, wanazembea, wameghafilika au wanapuuza tu.
Mbona hayo mambo machafu yamejaa mashuleni, lakini wazazi hawaogopi kuwapeleka watoto Shule?? Tena wanawapeleka wabaki huko huko (Mabwenini). Wanachofanya utakuta mzazi anakuwa makini juu ya mtoto, atatafuta shule bora kabisa yenye mazingira mazuri, atakuwa tayari kumpeleka shule ya mbali kwa sababu ya ubora wa elimu na mazingira na usalama. Na ataendelea kufuatilia.
Ila kwenye dini anachukulia poa.