Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PICHA ADIMU ZA TANU, JULIUS NYERERE NA WAZALENDO WALIOSAHAULIKA KATIKA HISTORIA YA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961



Written By Mohamed Said on Saturday, May 2, 2015 | 11:25 AM




Abdulrahman Ali Msham sasa ni mtu mzima na ana umri wa miaka 65. Wakati TANU inaasisiwa Dar es Salaam mwaka 1954 yeye alikuwa mtoto wa miaka minne. Majuma machache yaliyopita alikisikia kipindi kilichorushwa na Radio Kheri 104.10 FM kuhusu safari yaMwalimu Nyerere UNO mwaka 1955. Kwa kauli yake mwenyewe anasema kipindi kile kilimrudisha nyuma sana akamkumbuka marehemu baba yake Ali Msham ambae alikuwa moja wa wazalendo waliokuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukoloni. Abdulrahman Ali Msham akawa na hamu kubwa ya kukutana na aliyekuwa akieleza safari ile ya kihistoria. Alikuwa na hamu kwa kuwa na yeye alikuwa na machache angependa kueleza nini baba yakeMzee Ali Msham alifanya katika TANU katika ile miaka ya 1950.

Abdulrahman
alianza kwa kueleza kuwa baba yake alikuja Dar es Salaam kutoka Kilwa katika miaka ya 1950 akiwa fundi seremala na likuwa akifanya shughuli zake za kutengezeza samani Mtaa wa Kariakoo na Congo. TANU ilipoasisiwa mwaka wa 1954 baba yake alijiunga na kuwa mwanachama kwa kukata kadi ya TANU. Makazi yake yalikuwa Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa ambako alikuwa akiishi kwenye nyumba yake mwenyewe. Katika hamasa zile za kupambana na ukoloni baba yake alitoa chumba kimoja katika nyumba yake akafungua tawi la TANU na yeye mwenyewe akiwa mwenyekiti.

Katika harakati zile za kupambana na ukoloni alisikitiswa na hali ya ofisi ya Mwalimu Nyerere pale New Street kwa kuwa hakuwa na samani za maana katika ile ofisi yake. Baba yake alirejea kwenye kiwanda chake pale Mtaa wa Kariakoo na Congo akatengeneza meza ya ofisi ya hadhi ya rais wa TANU pamoja na viti kadhaa. Mzee Ali Msham alimwalika Mwalimu Nyerere kwenye tawi la TANU la Magomeni Mapipa ili makabidhi samani mpya kwa ajili ya ofisi yake. Mwalimu Nyerere alifika pale kwenye tawi la TANU na katika sherehe fupi Mwalimu Nyerere akakabidhiwa samani ile.


Kumaliza mazungumzo yetu Abdulrahman Msham alikabidhi picha za baba yake za wakati ule wa kupigania uhuru. Picha hizo nami naziweka hapa kwa ajili ya kuhifadhi na kuthamini mchango wa wazee wetu mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini kwa bahati mbaya michango yao haijathaminiwa.


Picha hiyo hapo chini inamwonyesha Mwalimu Nyerere akipokea samani hiyo iliyotengezewa na Mzee Ali Msham. Aliyesimama wa kwanza kulia ni Mzee Ali Msham mwenyekiti wa tawi la TANU Magomeni Mapipa wakati TANU inawaunganisha wananchi kupigani uhuru wa Tanganyika.

img258.jpg



img259.jpg


img257.jpg


[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
img256.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Ali Msham aliyekaa katikati katika moja ya mikutano ya ndani ya TANU aliyokuwa akifanya uani nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu, Magomeni Mapipa[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
img255.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Kushoto Wakwanza Ali Msham


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
img257.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Ali Msham (kushoto aliyesimama) akiwahutubia wanachama wa TANU uani nyumbani kwake katika mkutano wa ndani

Tawi hili la TANU Magomeni Mapipa lilikuwa na nguvu na viongozi mashuhuri wa TANU walifika mara nyingi kuzungumza na wanachama na viongozi wao. Picha ya chini wanaonekana Zuberi Mtemvu (aliyeshika tama) aliyekuwa Katibu Mwenezi wa TANU akiwa na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na kushoto yake Mzee John Rupia Makamu wa Rais wa TANU wakiwa katika moja ya hafla za TANU katika tawi hilo. Rais wa TANU Mwalimu Nyerere haonekani amezibwa na John Rupia lakini mlinzi wake katika vijana wa BANTU Group anaoenakana amesimamakaribu yake amevaa lubega.​


img250.jpg
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
img260.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Kushoto: John Rupia, Julius Nyerere, Zuberi Mtemvu
Waliosimama nyuma yao ni BANTU Group Vijana Walinzi wa Viongozi wa TANU[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
img251.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa kama ilivyokuwa ikionekana katika miaka ya 1950 ikiwa imezungikwa na wanachama wake.

img252.jpg
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

img254.jpg




























Search This Blog



 
The Boss,
Katika historia nzima hiyo ulichoona ni kofia tu?
Huna mchango mwingine wowote?

Hiyo nimeona very interesting
sababu siku hizi vibarakashia kwenye mikutano vinaitwa 'udini'
wakati kumbe hata TANU vilikuwepo vingi na havikuwa na shida
now CUF wanaitwa chama cha kidini sababu ya kanzu na vibarakashia...
 
Kuna kitabu kilikuwepo zamani cha baba chaa nyerere picha zote mwanzo mwisho nna hamu niwe nacho maktabani kwangu.sijui napata wapi?
 
Hiyo nimeona very interesting
sababu siku hizi vibarakashia kwenye mikutano vinaitwa 'udini'
wakati kumbe hata TANU vilikuwepo vingi na havikuwa na shida
now CUF wanaitwa chama cha kidini sababu ya kanzu na vibarakashia...

Safi sana mkuu ndo ajabu hyo pia watu walikua hawajui kuwa ilikua ikifika ramadhani huyo nyerere alikua anafunga pia.
 
Hiyo nimeona very interesting
sababu siku hizi vibarakashia kwenye mikutano vinaitwa 'udini'
wakati kumbe hata TANU vilikuwepo vingi na havikuwa na shida
now CUF wanaitwa chama cha kidini sababu ya kanzu na vibarakashia...

The Boss,
Wakati ule utazuia vipi lebasi hizo ilhali hao ndiyo wenye chama chao?
Utaanzia wapi kuliambia Baraza la Wazee wa TANU wasivae kanzu na kofia?
 
Hii ni Nyundo hasa. Heko Mzee Mohamed Said.

Mwendabure,
Katika vitu vinavyonisikitisha sana ni kule mimi kujua kuwa nyaraka nyingi za
historia ya TANU zipo katika hifadhi ya watu binafsi na nyaraka hizo nyingi
zimepotea na hizo abazo bado zipo zitatoweka kabisa kwa kukosa uangalizi.

Hizi picha nimezipata kwa bahati tu baada ya mtoto wa marehemu Ali Mshama
kusikiliza kile kipindi cha Miaka 60 ya Hotuba ya Nyerere UNO mwaka 1955
ndipo akanitafuta anieleze historia ya baba yake.

Hapo ndipo alipokuja na hizi picha kunionyesha.
 
TANU zamani ilikuwa kama CUF ya sasa
vibarakashia kwa kwenda mbele

WAZEE+WA+TANU.jpg


Waliokuwa Katika Picha Hii na Ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU
(Wengine: Hawapo)



  1. [*=left]Abdallah Shomari (Tandamti No. 3)
    [*=left]Nassoro Kalumbanya (Simba)
    [*=left]Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo)
    [*=left]Mtoro Ally (Muhonda)
    [*=left]John Rupia (Misheni Kota)
    [*=left]Julius Nyerere (Pugu Sekondari)
    [*=left]Said Chaurembo (Congo/Mkunguni)
    [*=left]Jumbe Tambaza (Upanga)
    [*=left]Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
    [*=left]Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande)
    [*=left]Mshume Kiyate (Tandamti)
    [*=left]Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo)
    [*=left]Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
    [*=left]Rajab Simba (Kiungani)
    [*=left]Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala)
    [*=left]Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
    [*=left]Makisi Mbwana (Aggrey/Congo)
    [*=left]Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
    [*=left]Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo).
 
WAZEE+WA+TANU.jpg


Waliokuwa Katika Picha Hii na Ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU
(Wengine: Hawapo)



  1. [*=left]Abdallah Shomari (Tandamti No. 3)
    [*=left]Nassoro Kalumbanya (Simba)
    [*=left]Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo)
    [*=left]Mtoro Ally (Muhonda)
    [*=left]John Rupia (Misheni Kota)
    [*=left]Julius Nyerere (Pugu Sekondari)
    [*=left]Said Chaurembo (Congo/Mkunguni)
    [*=left]Jumbe Tambaza (Upanga)
    [*=left]Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
    [*=left]Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande)
    [*=left]Mshume Kiyate (Tandamti)
    [*=left]Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo)
    [*=left]Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
    [*=left]Rajab Simba (Kiungani)
    [*=left]Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala)
    [*=left]Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
    [*=left]Makisi Mbwana (Aggrey/Congo)
    [*=left]Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
    [*=left]Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo).


Hapo Kina Msekwa hata hawajulikani wapo wapi
ajabu afte Uhuru tu hao washachukua positions....
nimeambiwa hapo alikosekana Ally Sykes tu.....
 
Back
Top Bottom