Picha: Bodaboda huwa wanawahi wapi?

Picha: Bodaboda huwa wanawahi wapi?

Kwahiyo mkuu serikali haitoi semina kila wakati kuhusu mambo ya usalama na tahadhali barabarani?
Labda ungesema ifungie mojakwamoja hii kazi ya boda boda kua kazi lasmi nasio ui Raumu serikali kwakila kitu..baadhi yamambo nisababu binafsi tuu.
WABADILIKE👈
Kwa nini serikali isilaumiwe wakati madereva wengi wa bodaboda na bajaji wanaendesha vyombo vyao bila leseni?!

Kwa nini serikali isilaumiwe wakati Hawa bodaboda na bajaji wanakiuka Sheria za usalama Barbarani kama ku-overtake kushoto, kusimama mahali popote kupakia au kushusha abiria, kupakia mishikaki, kupakia mizigo hatarishi n.k. bila kuchukuliwa hatua yoyote na polisi was usalama Barbarani?!
 
Hapo bodaboda ndio amefika alikokuwa anakimbilia.
 
Wanasema Bodaboda zinakuwaga na mizimu, ukiendesha hata kama ulikuwa na akili timamu Akili ghafla zinafyatuka unakuwa kama wao huelewi yaani
 
Wanahangaika na wakina boni yai lakini hao wendawazimu wanaokufa kila siku kwa hayo mamichina hawana habari nao, kimsingi bodaboda ni janga la kitaifa, Kagame pekeyake ndio kaweza maana ukithubutu kukutwa imekula kwako ndiomaana hata kwenye taa wanasimama na kuheshimu, lakini bongo yapo kama manyumbu tu.
 
Kama itawezekana, wangezifunga speed governor yenye limit ya 80km/hr

Vinginevyo watatuua abiria wao.

Kuna Siku nilikuwa nawahi ku-check-in ndege, maana zilibaki dakika 65 hivi ndege iruke na Mimi muda huo nilikuwa Sinza.

Ili kuwahi nikachukua boda ani-rush

Jamaa mwendo aliokuwa anaendesha, ukafanya nishukie njia ya panda ya Segerea, nikapiga simu kuomba nisafiri Kwa ndege ya Jioni.

Unaweza kuondoka Duniani kabla ya Siku zako Kwa uzembe wa hao bodaboda 🙌
Mbona ulikuwa umefika!?
 
Mbona ulikuwa umefika!?
Ni kweli, nilikuwa nakaribia lakini Kwa mwendo ule pamoja na kupitishwa katikati ya yale Malori nilihisi roho inataka kutoka 😅

Wale Jamaa ni risk taker sana

Bora upande Uber/bolts huwa wanafata protocol zote za barabarani
 
Back
Top Bottom