Picha bora ya mwezi barani Afrika kutoka kwa Mke wa Rais Mteule wa Botswana na somo kwa wanawake wengi wa viongozi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio picha bora kabisa kwa Mwezi huu Barani Afrika kutoka Kwa Mke wa Rais mteule wa Botswana siku ya uapisho wa Mume wake.

Ni picha inayoonyesha namna mwanamke huyu alivyo Mnyenyekevu, mtiifu kwa Mume wake ,Mwanamke mwenye maadili ya kiafrika, aliyefundwa akafundika,aliye lelewa akaleleka, mwenye hofu ya Mungu na upendo wa dhati kifuani pake.

Ikumbukwe ya kuwa Mwanamke huyu ni Msomi sana na aliyepiga kitabu vizuri. Lakini bado ni mnyenyekevu na anayetambua nafasi yake na wajibu wake kwa mume wake. Anajuwa pamoja na Elimu yake kubwa lakini bado yeye ni Mke wa Mtu ,ni Ubavu wa mtu.

Huyu Mama hata ukifuatilia watoto wake utakuta ni wanyenyekevu,wakarimu,wenye hekima, busara na upendo kwa watu wote pasipo viburi, dharau, majivuno wala nyodo. Kwa sababu wamepita katika mikono ya Mwanamke Mwenye hofu ya Mungu, upendo, utii, unyenyekevu na heshima.

Mwanamke huyu ni somo kwa wanawake wengi ambao wakisoma na kuwa na nafasi fulani unakuta hadi ndoa zao zinaanza kuyumba, kukosa mshikamano na upendo. Unakuta ndoa zinapumulia mipira na zilizojaa migogoro, malumbano,ugomvi, mabishano, mpasuko na mashindano kwa kila kitu.

Unakuta kutawala kwa majivuno, viburi na dharau pamoja na kutafuta ushindi na ushindani kwa kila kitu.

Angekuwa Mwengine hapo ungeona akiingia hapo amepandisha mabega utafikiri anataka kuyachomoa juu, angeanza kiburi na kutamani wanawake wengine wote wanyoe vipara utafikiri wamepata Majeraha kichwani na kuanza kubadilisha hata namna ya kuweka mdomo wakati wa kuongea.

Huyu mwanamke unaona kabisa kuwa ni ubavu sahihi na aliyechangia mume wake kufika hapo alipo fika hapo kuwa Rais. Mwanamke wa hivi huifanya ndoa na hata Familia kutamalaki kwa amani, furaha, upendo, maelewano, masikilizano na mshikamano wakati wote.

Screenshot_20241110-081829_1.jpg
Screenshot_20241110-081838_1.jpg
Screenshot_20241110-081844_1.jpg
Screenshot_20241110-081853_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
sioni cha ajabu, this might be a showoff to the crowd. Is she doing the same at home?
Kwa hiyo unataka kujua kama anafanya nyumbani au hafanyi? Alichofanya hadharani ndicho afanyacho kwake na mahali penginepo popote pale.Mwenye heshima ni mwenye heshima tu,mwenye unyenyekevu ni mwenye unyenyekevu tu na utamtambua awapo mahali popote pale.
 
Subiri aanze kuitafuna nchi kwa visacoss uchwara na foundations

Anyway jamaa katusua so lazima apewe heshima hata bandia ili mradi pesa zipo
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio picha bora kabisa kwa Mwezi huu Barani Afrika kutoka Kwa Mke wa Rais mteule wa Botswana siku ya uapisho wa Mume wake.

Ni picha inayoonyesha namna mwanamke huyu alivyo Mnyenyekevu, mtiifu kwa Mume wake ,Mwanamke mwenye maadili ya kiafrika, aliyefundwa akafundika,aliye lelewa akaleleka, mwenye hofu ya Mungu na upendo wa dhati kifuani pake.

Ikumbukwe ya kuwa Mwanamke huyu ni Msomi sana na aliyepiga kitabu vizuri. Lakini bado ni mnyenyekevu na anayetambua nafasi yake na wajibu wake kwa mume wake. Anajuwa pamoja na Elimu yake kubwa lakini bado yeye ni Mke wa Mtu ,ni Ubavu wa mtu.

Huyu Mama hata ukifuatilia watoto wake utakuta ni wanyenyekevu,wakarimu,wenye hekima, busara na upendo kwa watu wote pasipo viburi, dharau, majivuno wala nyodo. Kwa sababu wamepita katika mikono ya Mwanamke Mwenye hofu ya Mungu, upendo, utii, unyenyekevu na heshima.

Mwanamke huyu ni somo kwa wanawake wengi ambao wakisoma na kuwa na nafasi fulani unakuta hadi ndoa zao zinaanza kuyumba, kukosa mshikamano na upendo. Unakuta ndoa zinapumulia mipira na zilizojaa migogoro, malumbano,ugomvi, mabishano, mpasuko na mashindano kwa kila kitu.

Unakuta kutawala kwa majivuno, viburi na dharau pamoja na kutafuta ushindi na ushindani kwa kila kitu.

Angekuwa Mwengine hapo ungeona akiingia hapo amepandisha mabega utafikiri anataka kuyachomoa juu, angeanza kiburi na kutamani wanawake wengine wote wanyoe vipara utafikiri wamepata Majeraha kichwani na kuanza kubadilisha hata namna ya kuweka mdomo wakati wa kuongea.

Huyu mwanamke unaona kabisa kuwa ni ubavu sahihi na aliyechangia mume wake kufika hapo alipo fika hapo kuwa Rais. Mwanamke wa hivi huifanya ndoa na hata Familia kutamalaki kwa amani, furaha, upendo, maelewano, masikilizano na mshikamano wakati wote.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

View: https://youtu.be/BfODo_mb1z0
 
Back
Top Bottom