Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika tuna Rais wa nguvu mbele yetu, tuna kiongozi shupavu Nchini,tuna Amiri Jeshi Mkuu Mwenye Utimamu wa akili na Mwili,Tuna Kiongozi ambaye Mungu alimuandaa kuongoza Taifa letu, tuna Shujaa mbele yetu, tuna Rais ambaye Muda wote yupo tayari kimajukumu na anajua wajibu wake kwa Taifa letu.
Ukimuangalia Rais Samia namna anavyotembea na Muonekano wake unagundua kuwa ni kiongozi ambaye Ana morali kubwa sana ya kuwatumikia watanzania, anaipenda kwelikweli kazi yake na anatambua wajibu wake kwa Maisha ya watanzania.
Mama yupo shapu ,imara na hodari utafikiri Kijana wa miaka 30 aliyetoka kufuzu mafunzo maalumu ya kijeshi katika kikosi maalumu cha Makomandoo Au Majasusi Ya TISS au MOSSAD au CIA.
Huwezi ukaona Mama na Rais wetu Mpendwa yupo kinyonge au kizembe zembe. Rais wetu yupo Smart sana kiukweli. Na hii ndio maana ya mtu kuwa Rais na Taswira ya Nchi. Ameiheshimisha sana nafasi na taasisi ya Urais. ameipa heshima ,hadhi na kuiweka kwenye viwango vya hali ya juu sana.
Ona hata tu mpangilio wa mavazi yake na hata Rangi ya mavazi anayovaa Rais wetu Mpendwa. Unaona ni mavazi ya heshima ,hadhi ,staha na yenye kuakisi Mamlaka .Siyo mwingine anavaa mavazi utafikiri anakwenda msibani au yupo msibani au amevaa nguo ambazo vipimo vyake vilikosewa au ameshonewa nguo ambazo vipimo alipimwa mtu mwingine. Mwingine anavaa utafikiri anakwenda kufyatua tofali mbugani kule Mbozi. Inakuwa ni aibu kwa Nchi na Taifa na kuonekana ni Taifa la watu wasiojielewa. Maana hata muonekano wa mavazi ya mtu unaweza leta taswira ya akili ya mtu.
Ndio maana unaweza ukakutana na mtu mitaani au barabarani na ukajua tu ni kichaa au mgonjwa wa akili hata bila kuambiwa na mtu kwa kuangalia tu mavazi na muonekano wake. Kiukweli Rais Samia anastahili kuwa Rais wetu , kiongozi wetu na Amiri Jeshi Mkuu wetu. Anastahili kuendelea kutuongoza. Na tunapaswa kwenda kumchagua kwa kura nyingi sana mwishoni Mwa Mwaka huu.
Embu jionee Mwenyewe hapa chini picha hii ya Rais wetu Mpendwa ya hii Leo . Picha Iliyoteka Mitandaoni na kuteka nyoyo za watu na kuleta tabasamu kwa mamilioni ya watu ndani na nje ya Nchi. Picha ambayo ndio imekuwa mada kuu ya siku,picha iliyowafurahisha sana watanzania na kupelekea kufunikwa kwa habari zote za hii leo na yenyewe kubakia kama mada kuu ya siku.
Watanzania Tembeeni vifua mbeleee na kwa kujiamini kabisa. Nchi na Taifa lipo katika mikono salama na kila kitu kipo salama mikononi Mwake Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Sasa Subirini kesho Muone Moto wake. Usipange Kukosa kufutilia na kuelekeza macho yako pale katika viunga vya Mji Mkuu wa Tanzania.
View attachment 3384758
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.