LGE2024 Picha: CHADEMA tunakubali hali ya kiuchumi ni ngumu lakini this is too much. Hii ni stage au kichanja cha vyombo?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Wakuu,

Nimelia sana baada ya kuona picha hii ya Tundu Lissu akiwa anahutubia huko Singida.

Najua kuendesha chama cha siasa Tanzaniani ngumu hasa upande wa kifedha lakini ifike hatua mjipe thamani kama Chama Kikuu Cha Upinzani.

Hivi inakuwaje mtu mzito kama Tundu Lissu mnamsimamisha kwenye jukwaa chakavu na baya kiasi hiki?

Stage kama inataka kudondoka, serious?

Soma Pia: Tundu Lissu: Tanzania sio Jamhuri, tuko chini ya Utawala wa Kijeshi. Ukiondoa Polisi na Wakurugenzi CCM hakuna!

Mna uhakika huyu ndo Mwenyekiti wa CHADEMA ngazi ya kitaifa?

Kweli mlishindwa kutengeneza stage fulani hata kama ni ndogo lakini ya kisasa inayoendana na HADHI ya chama chenu?

View attachment 3162368

Ukichukua picha hii ukaipeleka hata hapo Malawi, kwa mtu asiyejua ukubwa wa CHADEMA anaweza akasema Lissu ni mjumbe wa nyumba 10 anahutubia wanakijiji.

Tunaelewa hali ni ngumu lakini zingatieni mambo madogo madogo kama haya.

Mjinga mjinga unaonyesha upande wa barabarani wakati watu wamekaa upande mwingine. Hamjui hata kutengeneza picha fake
 
Tundu Lissu akigawa fomu za Mawakala wa CHADEMA Tarafa ya Ikungi mkoani Singida walioapishwa leo Novemba 26, 2024 tayari kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024..

View: https://m.youtube.com/watch?v=BA1GgidGg8k

Ila kusema kweli CCM wangeruhusu uchaguzi wa haki wangetoka madarakani. Hawa watu wameitika kwenda kusimamia uchaguzi pamoja na wajumbe wao kukatwa!
 
Wakuu,

Nimelia sana baada ya kuona picha hii ya Tundu Lissu akiwa anahutubia huko Singida.

Najua kuendesha chama cha siasa Tanzaniani ngumu hasa upande wa kifedha lakini ifike hatua mjipe thamani kama Chama Kikuu Cha Upinzani.

Hivi inakuwaje mtu mzito kama Tundu Lissu mnamsimamisha kwenye jukwaa chakavu na baya kiasi hiki?

Stage kama inataka kudondoka, serious?

Soma Pia: Tundu Lissu: Tanzania sio Jamhuri, tuko chini ya Utawala wa Kijeshi. Ukiondoa Polisi na Wakurugenzi CCM hakuna!

Mna uhakika huyu ndo Mwenyekiti wa CHADEMA ngazi ya kitaifa?

Kweli mlishindwa kutengeneza stage fulani hata kama ni ndogo lakini ya kisasa inayoendana na HADHI ya chama chenu?

View attachment 3162368

Ukichukua picha hii ukaipeleka hata hapo Malawi, kwa mtu asiyejua ukubwa wa CHADEMA anaweza akasema Lissu ni mjumbe wa nyumba 10 anahutubia wanakijiji.

Tunaelewa hali ni ngumu lakini zingatieni mambo madogo madogo kama haya.
Unaanza kwa kusema wewe "UMELIA SANA"!
Siyo kwa sababu ya kulionea huruma taifa lako linalo bakwa sasa hivi, ila kwa sababu za chama ambacho hakitakiwi kuwepo wameshindwa kuwa na 'platform' ya kifahari uliyo nayo akilini mwako!

Lakini pia, pamoja na "KULIA KWAKO" (kwa kinafiki kama kweli unaweza kufanya hivyo); hukuweza hata kwa sekunde moja kufikiria ujumbe alio uwasilisha huyo unaye mhofia kuwa atadhurika kwa kuwa kwenye jukwaa kama hilo!

Kwako "Jukwaa" limekuwa muhimu zaidi kuliko ujumbe ulio tolewa kwenye jukwaa hilo!
 
Ila kusema kweli CCM wangeruhusu uchaguzi wa haki wangetoka madarakani. Hawa watu wameitika kwenda kusimamia uchaguzi pamoja na wajumbe wao kukatwa!
Mwamko huo uwe ndio maandalizi na mwanzo wa yatakayo fanyika 2025.
Hili ndilo linalo takiwa kuzingatiwa, tokea sasa na kwenda mbele.

Lisiwe tena jambo la "CCM wange ruhusu"..., CCM ni lazima ilazimishwe kukubali, siyo "kuruhusu"
nafasi hii ikiachiwa kupita wakati huu, taifa hili litadidimia sana chini ya hiyo CCM.
 
Binafsi nahitaji Sera na kuonyesha ni vipi wabangaizaji na have nots (the downtrodden) wanaweza wakakombolewa na kesho yao kuwa nafuu..., na sio kuonyesha ni vipi nyie mpo well off kuliko waliowazunguka...,

Mentality hizi ndio watu wanajaza ma v8 kwa kodi ya mtu ambaye hapati hata milo mitatu, badala ya kumjengea hata barabara ya kupita na baiskeli au hospitali za kumtibu miguu inayosumbuliwa na miiba sababu ya barabara zenye vichaka...
 
Unaanza kwa kusema wewe "UMELIA SANA"!
Siyo kwa sababu ya kulionea huruma taifa lako linalo bakwa sasa hivi, ila kwa sababu za chama ambacho hakitakiwi kuwepo wameshindwa kuwa na 'platform' ya kifahari uliyo nayo akilini mwako!

Lakini pia, pamoja na "KULIA KWAKO" (kwa kinafiki kama kweli unaweza kufanya hivyo); hukuweza hata kwa sekunde moja kufikiria ujumbe alio uwasilisha huyo unaye mhofia kuwa atadhurika kwa kuwa kwenye jukwaa kama hilo!

Kwako "Jukwaa" limekuwa muhimu zaidi kuliko ujumbe ulio tolewa kwenye jukwaa hilo!

Umeonesha ulivyo mweupe kichwani.

Tazama nyuzi zangu tatu za nyuma kabla ya uzi huu alafu rudi tena.

Acha kujifanya unajua watu huku mitandaoni and who they are.
 
Kuna mahali nime andika kuwa ninakujuwa?

Mimi ninaweza "kuwa mweupe kichwani"; lakini kweli ulitegemea nika some hizo "nyuzi zako tatu za nyuma" ndipo nije kuweka maoni yangu kwenye nyuzi yako hapa? Ndivyo ulivyo tegemea iwe?

'Any way' nadhani hakuna sababu ya maana sana kukwaruzana hapa kati yako na mimi. Sioni kuwa unavyo vimelea vya ujinga ujinga mwingi unaoonyeshwa na baadhi ya watu humu JF.
 
Back
Top Bottom