DANNYBAVICHA
Senior Member
- Oct 22, 2013
- 109
- 33
Wana Jf, kumekuwa na malalamiko mengi humu jamnvini kuhusu kiburi cha watangazaji wa kituo cha radio cha Clouds FM kuwa juu ya sheria za nchi kwa kufanya mambo watakavyo.
Leo mmoja wao ameonja joto la jiwe baada ya kujifanya mbabe na kumtukana askari wa usalama barabarani Leo asubuhi, picha hapa ikionyesha EPHRAHIM Kibonde akiwekwa chini ya ulinzi baada ya kumtusi askari.

Tatizo ni foleni wandugu. Tuko wengi tuna hasira kutokana na kucheleweshwa makazini na foleni ya magari jijini. Maaskari wa barabarani ni wasumbufu sana,mara nyingi wanachelewesha magari ya upande fulani,na kuruhusu ya upande mwingine kwa muda mrefu. Nafikiri jamaa alikuwa anawahi airport. Lakini kwa nini adhalilishwe hadharani kiasi hicho,askari wetu wanatumia maguvu zaidi,kichwani zero. Sikubaliani na kibonde kwa mengi,lakini kwa hili amedhalilihwa.