PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Nafikiri hiyo ilikuwa bahati mbaya, kwasababu ninavyoone imetokea, hiyo bunduki kwanza si ya risasi, ni ya mabomu ya machozi kwa wale wanaofahamu bunduki watakubaliana na mimi...

Hilo bomu la machozi wakati mwingine huwa linalipuka vibaya, na nionavyo mwili wa marehemu hapo umesambaratishwa kama na utumbo unaonekana na kuna askari mmoja kwenye hizo picha amedondoka chini kama askari wenzie wanamsaidia vile...

Hebu angalia vizuri..inaonyesha ni kama hapo ilo bomu limefyatuka kwa bahati mbaya likajeruhi marehemu na askari....ni maoni tu lakini....na hawa polisi wetu ambao wametoka depo juzi tu hawa hawajui hata madhara ya hizi vitu.


hakuna issue ya bahati mbaya hapa, hao ni askari waliokuwa trained. tanzania kila kitu bahati mbaya, kuanzia olympic mpaka maisha yetu? usanii umetosha sasa.
 
...Siku nyingine huwa unaandika mambo ya maana sana ambayo yanaweka mbele maslahi ya nchi badala ya yale ya magamba. Wanaostahili kujipanga si waandishi wa habari pekee yao bali ni Watanzania wote ndani na nje ya nchi. Nasema hivyo kwa sababu mauaji yanayoendelea hivi sasa nchini yalikaribia kuwagusa madaktari (Ulimboka) na Watanzania wengine waliouwawa kule Arusha, Igunga, Tarime, Mbeya, Morogoro ambao wanajingizia riziki zao kupitia fani mbali mbali nchini. Kwa hiyo Watanzania wote tuungane ili kuukomesha udhalimu unaofanywa na Kikwete kwa kutumia vyombo vya dola.

Waandishi wa habari wanaweza kujizatiti na kususia kuandika habari zozote za kuhusu Serikali na magamba.

Mkuu poleni sana kwa msiba wa mwandishi mwenzenu wa habari, aliopoteza maisha hakiwa kazini inasikitisha sana ni mauaji ya kinyama, mkuu jipangeni kama waandishi habari mlifungulie mashitaka ya mauaji Jeshi la Polisi Iringa, mkuu msitiri marehemu kuhusu baadhi ya picha unazosema inaonyesha sehemu ya uume wake.
 
Wanajamvi,

Hakuna maelezo yenye mantiki yatakayoeleza, kuhalalisha au kusamehe unyama huu. Hakuna tume itakayochunguza ukweli usiohitaji fikra hata kidogo.

Ilianza taratibu kwa watu kupotea. Yakatokea ya Tarime tukakaa kimya, yakahamia Arusha tukalaani, yakaenda Igunga zikaundwa tume kutupumbaza, yakjirudia Arumeru tubaki kulalamika. Mlolongo ni mkubwa sana. Kila yanapotokea mauji kama haya tunalalamika na kulaani sana tu halafu tunakaa kimya yanapita.

Naomba sasa, katika post hii tumetoa R.I.P za kutosha. Tumesononeshwa kiasi kwamba hatuwezi kusononeka zaidi. Tumetoa pole na tutaendelea kutoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na Taaluma nzima ya wanahabari.

Sasa tuseme basi na tuanze kujadili way forward.

Napendekeza:
Kwanza, tuungane mkuu wa jeshi la Polisi ajiuzulu
Pili, Tusikubali uchunguzi wa tume zao. Uchunguzi sasa uwe huru askari wakiwa magereza.
Tatu, Waziri wa mambo ya ndani ambaye katika wiki moja tu ameshindwa kuzuia mauaji ya Raia wasio na hatia sasa AJIUZULU.

Hayo yakishindikana, tujiunge na kumtaka Rais Kikwete ajiuzulu.

Bila kufanya hayo, tutachinjwa zaidi kama kuku wa nyama, tutapondwa vichwa kama nguruwe, tutakuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Wakati umefika na tuanze sasa.

Narudia salaam zitaendelea lakini it is time we make statement to rulers. Let start now.

MWEMA, NCHIMBI MUST GO WITHIN 48hrs
 
Hivi hawa polisi wamesahau sababu ya kuwaweka peke yal kwenye kambi?!!! What do they think?????????
 
...Mkuu mauaji haya ya kinyama hayawahusu waandishi wa habari pekee bali Watanzania wote ambao wanaitakia mema nchi yetu.

Tumekuwa kimya kira mara ikitokea, hatusemi, hatukatazi, tunaangalia tu na kila siku inakuwa poa, hakuna matata.

Lets hope this time round, it wont be poa na hakuna matata.

Sio poa kabisa na matata yapo sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu n00b, kwani ilikuwaje hadi ikafikia hawa jamaa wakamzingira namna hii hayati mwandishi Mwangosi?
Hebu funguka kidogo basi!

marehemu ni mwenyekiti w waandishi habari mkoa wa iringa...kuna mwandishi wa nipashe alikamatwa na polis sasa marehemu akaenda kuuliza kisa cha kukamatwa mwandishi wa nipashe ndipo akafanyiwa hicho alochofanyiwa na nsio maana unaona ni pembeni na hakuna raia mwingine bali yeye peke yake na hao polisi
 
Rest In Peace My Beloved Journalist, the God Of Revenge Will Do Something for You in Heaven, and on Earth

Daudi Mwangosi
 
I see, SECONDED!
Sasa tuseme basi na tuanze kujadili way forward.

Napendekeza:
Kwanza, tuungane mkuu wa jeshi la Polisi ajiuzulu
Pili, Tusikubali uchunguzi wa tume zao. Uchunguzi sasa uwe huru askari wakiwa magereza.
Tatu, Waziri wa mambo ya ndani ambaye katika wiki moja tu ameshindwa kuzuia mauaji ya Raia wasio na hatia sasa AJIUZULU.

Hayo yakishindikana, tujiunge na kumtaka Rais Kikwete ajiuzulu.

Bila kufanya hayo, tutachinjwa zaidi kama kuku wa nyama, tutapondwa vichwa kama nguruwe, tutakuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Wakati umefika na tuanze sasa.

Narudia salaam zitaendelea lakini it is time we make statement to rulers. Let start now.

MWEMA, NCHIMBI MUST GO WITHIN 48hrs
This' too much!
 
huyu aliyevalia kiraia kama kashika bastola...........

Askari wote wako loaded, hakukuwa na sababu, risasi za moto kwenye mkutano wa siasa wapi na wapi, mbona ngao wanazo nyingi tu kwaandamanaji hawaendi na silaha mikutanoni, labda Rage, wengine tuliobaki tunaenda bila silaha.
 
unaweza kuwa mjanja sana lakini umesahau kitu kimoja dakika 20 kabla ya kuuawa marehemu alikuwa ana jeans ya blue,alibadilisha saa ngapi akavaa suruali ya khaki?
 
Ni wazi watataka kupotosha, video ya tukio zima itawekwa YouTube.

Kama waandishi hatutashirikiana katika hili, naachana rasmi na tasnia hii.
Ukiweka video ni sawa kabisa,tunaomba ututumie ama uiweke na tuhakikishe zinaonekana dunia nzima kwa wapenda amani na wapinga udhalimu wa serikali zinazotumia vyombo vya dola kuuwa wananchi kwasababu za kisiasa.
Nakushauri usiachane na tasnia hii kwasbabu unawatumikia wananchi na si waandishi,unajuwa kuna wenye kupokea bahasha,so unachotakiwa kutafuta ni sapoti ya wananchi.
Najuwa umekasirika sana,kila mpenda haki amekasirishwa na kusikitishwa na tukio hili.So pengine linaweza kuleta ile hali ya kukata tamaa.Ukifanya hivyo,basi damu ya mwandishi mwenzako mpigania haki itakuwa imepotea bure?
Pole sana ndugu yangu,lakini tukio hili,limeibadilisha mioyo ya wengi wetu
 
...Unachosema Mkuu Ngambo Ngali ni kweli kabisa. Watanzania tumekuwa wapumbavu mno wa kunyamazia unyama unaofanywa dhidi ya Watanzania wenzetu na hivi vyombo vya dola. Kwa sababu hao wanaouwawa si ndugu zetu wa karibu basi tunafumbia macho udhalimu mkubwa unaoendelea nchini lakini tujue udhalimu huu hauna macho jana kauwawa mwandishi wa habari kule Iringa kesho anaweza kuuwawa mtu wako wa karibu kabisa labda mume/mke/mtoto n.k.

Tuungane Watanzania kukomesha udhalimu huu au nchi yetu ndio itazidi kuangamia kwa mauaji ya kutisha katika sehemu mbali mbali nchini.
Tukumbuke umoja ni nguvu na utendano ni udhaifu.

Tumekuwa kimya kira mara ikitokea, hatusemi, hatukatazi, tunaangalia tu na kila siku inakuwa poa, hakuna matata.

Lets hope this time round, it wont be poa na hakuna matata.

Sio poa kabisa na matata yapo sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom