Nafikiri hiyo ilikuwa bahati mbaya, kwasababu ninavyoone imetokea, hiyo bunduki kwanza si ya risasi, ni ya mabomu ya machozi kwa wale wanaofahamu bunduki watakubaliana na mimi...
Hilo bomu la machozi wakati mwingine huwa linalipuka vibaya, na nionavyo mwili wa marehemu hapo umesambaratishwa kama na utumbo unaonekana na kuna askari mmoja kwenye hizo picha amedondoka chini kama askari wenzie wanamsaidia vile...
Hebu angalia vizuri..inaonyesha ni kama hapo ilo bomu limefyatuka kwa bahati mbaya likajeruhi marehemu na askari....ni maoni tu lakini....na hawa polisi wetu ambao wametoka depo juzi tu hawa hawajui hata madhara ya hizi vitu.
Mkuu poleni sana kwa msiba wa mwandishi mwenzenu wa habari, aliopoteza maisha hakiwa kazini inasikitisha sana ni mauaji ya kinyama, mkuu jipangeni kama waandishi habari mlifungulie mashitaka ya mauaji Jeshi la Polisi Iringa, mkuu msitiri marehemu kuhusu baadhi ya picha unazosema inaonyesha sehemu ya uume wake.
...Mkuu mauaji haya ya kinyama hayawahusu waandishi wa habari pekee bali Watanzania wote ambao wanaitakia mema nchi yetu.
Mkuu n00b, kwani ilikuwaje hadi ikafikia hawa jamaa wakamzingira namna hii hayati mwandishi Mwangosi?
Hebu funguka kidogo basi!
This' too much!Sasa tuseme basi na tuanze kujadili way forward.
Napendekeza:
Kwanza, tuungane mkuu wa jeshi la Polisi ajiuzulu
Pili, Tusikubali uchunguzi wa tume zao. Uchunguzi sasa uwe huru askari wakiwa magereza.
Tatu, Waziri wa mambo ya ndani ambaye katika wiki moja tu ameshindwa kuzuia mauaji ya Raia wasio na hatia sasa AJIUZULU.
Hayo yakishindikana, tujiunge na kumtaka Rais Kikwete ajiuzulu.
Bila kufanya hayo, tutachinjwa zaidi kama kuku wa nyama, tutapondwa vichwa kama nguruwe, tutakuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Wakati umefika na tuanze sasa.
Narudia salaam zitaendelea lakini it is time we make statement to rulers. Let start now.
MWEMA, NCHIMBI MUST GO WITHIN 48hrs
huyu aliyevalia kiraia kama kashika bastola...........
Ukiweka video ni sawa kabisa,tunaomba ututumie ama uiweke na tuhakikishe zinaonekana dunia nzima kwa wapenda amani na wapinga udhalimu wa serikali zinazotumia vyombo vya dola kuuwa wananchi kwasababu za kisiasa.Ni wazi watataka kupotosha, video ya tukio zima itawekwa YouTube.
Kama waandishi hatutashirikiana katika hili, naachana rasmi na tasnia hii.
Tumekuwa kimya kira mara ikitokea, hatusemi, hatukatazi, tunaangalia tu na kila siku inakuwa poa, hakuna matata.
Lets hope this time round, it wont be poa na hakuna matata.
Sio poa kabisa na matata yapo sana.