Jamani kwa uchache tu fuatilieni matukio haya;
Nakumbuka waandishi wa habari walipopigwa na kujeruhiwa na askari magereza pale ukonga, waziri wa mambo ya ndani wakati huo Omari Mapuri aliropoka na kuwaponda waandishi hao badala ya kuwapa pole. Kulitokea ka-umoja ka wanahabari;wakaungana kususia habari yoyote ya wizara ya mambo ya ndani. Angalau mapuri aliondolewa japo amepelekwa china kuwa balozi.
Mwangosi ameuawa na askari polisi akina kibanda watafanya nini?
- Mwandishi wa Tanzania Daima Samson Mwigamba alifunguliwa mashitaka wakidai aliandika makala ya kuwachochea askari wasaliti utawala uliopo as if mwandishi ni IGP au mkuu wa majeshi.
- Mhariri mkuu wa gazeti hilohilo Absalom Kibanda akafunguliwa kesi kwa kuruhu makala ile ichapishwe
- Gazeti la mwanahalisi limefungiwa kwa kuandika ukweli juu ya yaliyompata Dr Ulimboka.
- Siku chache baada ya gazeti kufungiwa Kikwete aliwaita ikulu waandishi wa habari kupima upepo, wakanywa juice na kupewa bahasha. Wakaishia kuuliza maswali ya chekechea likiwemo alilouliza Absalom Kibanda
- Mwandishi wa chanel ten Daudi Mwangosi apigwa bomu na polisi karibu kumi na kufa papo hapo huko Iringa.
- ............. ongezea orodha.