PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Asante noob kwa taarifa iliyowazi!....

...Polisi wamesema Mwangosi alikimbilia waliko polisi kuomba msaada na kumkumbatia polisi ndipo kitu ambacho hakijulikani kilikotoka kikamlipua! ......Hizi bangi!..
Yaani hata aibu jamaa hawana. Sasa hapo kwenye picha ndiyo wanampa msaada?
 
attachment.php

nimeskiza spin movie za RPC Iringa, asubuhi hii kupitia Wapo Radio FM. Eti bomu lilirushwa. hivi kama bomu lingerushwa kuna askari angepona hapo?

au kwanza ilikuwaje kuwaje, hata kama bomu lingekuwa la kurushwa, alengwe Daudi (huku wakiwa wamemzingira namna ile)?

polisisiemu lazima waheshimu haki za binadamu.
 
Sasa hivi nimesikiliza mahojiano kati ya RPC na mwandishi wa WAPO radio, anadai mwandishi DM alikuwa anafukuzwa na wananchi (wanachama wa Chadema) ambao walikuwa wanapambana na polisi kwa kutumia mawe. Na amepigwa na bomu ambalo polisi hawakuwa nalo, Polisi wanawashikilia watu saba kuhusiana na mauaji hayo.

Shuhuda mwingine aliyekuwepo kwenye tukio, anasema Polisi walimfyatulia bomu marehemu ambapo polisi aliyekuwa nyuma ya marehemu alijeruhiwa, maelezo ya shuhuda yanaendana na picha ya kwanza hapo juu. Na kwa mujibu wa shuhuda, kamanda wa Polisi wa mkoa alikuwa anashuhudia wakati unyama huo unatendeka.

Vifo vya watanzania wenzetu vinavyohusishwa na jeshi la polisi vinaanza kuwa matukio ya kawaida, hivi tunavyosikia ni kwavile kuna mkono wa siasa ndani yake, lakini polisi wetu wamekuwa wakiua wananchi kwa visingizio mbalimbali as if wao ni mahakama na wako juu ya sheria.

Sidhani kama wanaharakati au vyama vya siasa pekee wanaweza kupiga kelele ya kuleta mabadiliko, ni sisi wananchi wote bila kujali tofauti zetu za kiitikadi kupiga kelele na kuomba hatua stahiki zichukuliwa dhidi ya wote waliohusika na matukio ya vifo vya wananchi. Zaidi kushinikiza reform kwenye jeshi la Polisi. Lazima kuwa na jeshi litakalofanya kazi kwa uadifu na kutokuwa tayari kufanyia kazi maslahi binafsi ya wanasiasa

Kwa kweli hata mimi nimeshangazwa sana na maelezo ya huyo RPC!!! Hivi hawa poilisi huwa hawana akili kiasi hicho??!! RPC hana hata akili ya kudanganya?!!! Ina maana alikua hajui kama kuna waandishi wengine zaidi ya huyo waliyemuua na walikua wakichukua picha??!! Hivi huyu RPC bubu anawezaje kuelezea picha za tukio hilo tunazoziona humu JF??!! Kwamba hao Polisi waliomzunguka huyo mwandishi wakimsulubu ni wanachama wa CDM???!! Na wanafanya hivyo kwa kuwa wameshaona watanzania tumezidi utorozobi!!

Mkubwa Mzawa halisi naungana na wewe kabisa. Ni wakati sasa tukaacha uoga na kuwawajibisha hawa mazimwi!!

 
n00B

Mgonja anadai Mwangosi alikimbia kutoka kwa waandamanaji akiomba msaada wa Polisi ni kweli ndugu yangu? Na kama sivyo tutaisubiria video tujionee ukweli, nakushauri disseminate hizo evidence ulizonazo kabla hawajakuvamia na wewe!

Mungu Ibariki Tanzania.

Hv kumbe changonja nae ni
mwepesi namna hii! Ina maana hajui
kama watu wanapicha za kitu halisi
kilichotokea kwenye field?
They say a picture tells 1,000
words but when I see these all I see is 3 words: 'THEY KILLED HIM'.
Rip DM
 
siamini ninachokiona hapa.... dah!! Hivi tumefikia hapa? kweli Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!
 
Hii hali sana inatisha, inabidi Serikali na jeshi la polisi wawajibishwe kwa unyama huu!
 
Hii Nchi tunaelekea Wapi?! Mungu Mwenyezi, mlaze mahali pema kaka huyu. Ijalie familia yake nguvu pamoja na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu!!
 
nimepokea taarifa hizi ka masikitiko makubwa....mda si mrefu tutajua kwa undani
 
Policccm washasema alirushiwa kitu kizito wa wananchi
 
Picha ya mwisho juu, ambayo inaonyesha mwili wa marehemu, utaona buti la askari aliyeanguka! Inaonekana kweli kuna askari aliyeumizwa.
Ila hii ni Tanzania bwana, chini ya CCM dhaifu, hakuna action yoyote itakayochukuliwa hapo. Mtalia, mtatukana na mtazika. Zaidi zaidi for revenge or justice ndugu waende kwa mganga wa kienyeji ampe huyo polisi busha na upele wa maisha, ila wasitegemee justice yoyote kutoka serikalini!
 
Naanza mkakati wa kuwaroga polisi wote popote paLE WALIPO MBWA WAKUBWA HAWA
 
Najua mapolisi na ccm yao watasema chadema ndio waliomuua mwandishi Daudi Mwangosi. Sasa wakiua waandishi wa habari ili mambo yasijulikane, serikali hii na wasira wao wanatupeleka Bosnia au Afganistan au wapi???? Morogoro wamemuua muuza gazeti asiyehusiana kabisa na Chadema, sasa Iringa wameua mwandishi wa habari. Wako kinyume na habari. Ulimboka waitaka afe ili habari za madaktari zisitoke kupitia yeye kiongozi wao. Enough is enough, kama ningekuwa mimi ndo napata urais watu wote wenye harufu ya damu sasa wasingeruhusiwa kuvuta hewa Tanzania. Binadamu hawezi kukaa pamoja na wanyama wenye sura ya watu.
 
Huyo askari analiyeshika chupa ya Maji namfahamu sana huyu jamaa.
 
Taarifa ipi wakati huyu anaongea ujinga,angalia picha ya marehemu kwa chini ni jeans hiyo au ni kadeti?
Nilijibu hivyo ili yaishe, kuendelea kupingana naye ingekuwa kazi bure.
 
Duh!! Huu Unyama Unatisha!! Wamemuua bila sababu yoyote maskini!! Any way Kila kipumuacho Kitaonja mauti ila kwa nini Uuwe Mwenzako? Angalia yule Polisi anavyo Tumia lile Guruneti Kuua? "LIWALO NA LIWE" WAPO PALE KUTETEA CHAMA KISHINDE!! Shame on this statements
 
Huu ni unyama uliyopitiliza kwa kweli. Ila ukiwa na jeshi ambalo lina watu walioshindikana mtaani wakaghushi vyeti vya taaluma ya form four unategemea nini zaidi ya unyama huu.

Haya yana mwisho ,Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.
 
IGP Said Ally Mwema, na Kamishana wa Operation Paul Chagonja, mmechelewa sana kujiuzulu.

Picha zinaonyesha mwandishi wa habari amemkumbatia OCS,lakini kupitia katikati ya miguu ya OCS (yaanni doba ya OCS) Askari amepitisha bunduki kuelekea katika Tumbo la Daud Mwangosi, hapa maelezo yapo dhahiri.

Aliyepitisha bunduki katikati ya miguu ya OCS ndiye aliyerusha hicho kilichomuua, na OCS amejeruhiwa miguu kwa kuwa Bunduki ilipitishwa katikati ya miguu yake tokea nyuma na Askari mmojawapo wakati wanatekeleza mkakati wa kuua. Hapa mnachukua pesa zetu kwenda Iringa kuchunguza nini. Wauaji wakubwa nyie, Chinjachinja.

Mnashughulikia mikusanyiko ya Chadema tu wakati bububu kulikuwa na Mkutano wa Kampeni na huku wafuasi wa CCM wanaotishia watu bastola mnawaacha Mwandishi ambaye hakuwa na silaha isipokuwa kamera yake ndo mmemuua. Mmemsambaratisha kama Gaid.

Nashauri hata Polisi toka Makao makuu wasiende Iringa. Wachunguzi wateuliwe wengine au Taasisi zisizo za serikali ndo zisimamie jambo hili. Polisi ni watuhumiwa, Picha zinaonyesha wameua, wanaundaTume wao, wachunguze wao, na majibu watutangazie wao. Huu ni Uhuni, kama hakuna uchunguzi huru ama kuwawajibisha polisi, hakuna kitakachokubalika. Lakini hadi hayo yaendelee Mwema na Chagonja wanapaswa wawe wamejiuzulu hadi leo jioni.

Kama wanashindana na nguvu ya Umma, ama kulindwa na Ushemeji wa Amiri Jeshi, ngoja tusubiri hatima. Ila polisi wa Tanzania now it is too much, ninyi ni wauaji, chinjachinja na waporaji wakuu na Majambazi sugu ni polisi
 
Mkuu, hongera, weka mambo wazi ili mchawi ajulikane
 
nimeshikwa na hasira sana juu ya jesh letu la polisi.... hawa ni wauwaji wakubwa... we should do something!
 
Back
Top Bottom