tanzania tanzania!nchi yangu tanzaia ,mama yangu tanzania!nakulilia mama yangu tanzania nakulilia tanzania!wanao hatujui adui yetu ni nani,na rafikia yetu ni nani!anayeahidi kulinda usalama wetu ndiye anayetengua usalamua huo,anayeahidi kututetea ndiye wakili wa aliyetudhulumu,anayelia pamoja nasi ndiye anayecheka na adui yetu,anayekuja kwenye misiba yetu ndiye anayelipia mauaji yetu!mama yangu tanzania uko wapi utunisuru,hataujui mchana wala usiku salama ni wapi!hatujui kichaka wala pepo tutasalimika wapi,hatuijui shibe maana njaa manusura yetu!nalia na mama yangu tanzania ainuke atupe ujasiri wa kusimama!nalia na mama yangu tanzania ikiwezekana atuzae upya maana uhai ulio sawa na kifo ni kheri nikabaki mfu!mama yangu tanzania inuka sasa tujitambue leo!inuka tanzania wanao hatujui tunakwenda wapi,inuka mama yangu tanzania tuonyeshe njia ya kupita maana juu yetu kuna chui,pembeni kuna simba,nyuma yetu moto,mbele yetu bahari chini yetu kuzimu.damu ya wanao tanzania inamwagika na bila shaka umechoka kuifyonza ,itapike sasa mama yangu tanzania itapike sasa na wanao ituloweshe tukijua kama leo sio sisi kesho yetu haipo mbali!walipowaua wenzetu tulinyamaza,watakapotuua sisi hakutakuwa na wa kutututetea.ole wako tanzania mama yangu na katika hili unyamaze!ole wako tanzania?ole wako na damu hii uinywe kimya bila kuicheua adhabu yako sitaki kuikadiria !