WAPO radio 98.0 FM. Kila siku saa moja na dakika 20 wana kipindi cha matukio asubuhi na jioni muda huo huo. Wanajitahidi sana kutafuta wahusika halisi wa matukio. Hapa natoa kile nilichokisikia kutoka kwa DEREVA ALIYEKODIWA NA WAANDISHI WA HABARI kuwapeleka kwenye eneo la tukio (ndimo alimokuwamo marehemu). Dereva huyo amejitambulisha kama John Joseph.
Kwanza kabisa ameanza kwa kusema AMESHUHUDIA KWA MACHO YAKE TUKIO HILI MWANZO HADI KIFO CHA MAREHEMU. Wakati kikao cha ndani kinaendelea ghafla zikafika defender nne za FFU akiwapo OCD. OCD baada ya kuzungumza na viongozi wa CHADEMA na kumweleza kuwa hakuna mkutano wa hadhara akakubali waendelee, FFU wakawa nje. Mara akatokea RPC na gari lake. Yeye alipofika akasema NI AMRI TAWANYIKENI. Wananchi waliokuwapo nje ya ofisi WAKAJISALIMISHA KWA KUKAA CHINI NA KUNYOOSHA MIKONO JUU. Lakini hiyo isitoshe mabomu ya machozi yakaanza kumiminika kama mvua hovyo hovyo. Waandishi wakarudi kwenye gari lao. Ndipo polisi wakamdaka mwandishi mmoja na kuanza kumpa kipigo kikali. Kuona hivyo, marehumu akashuka kwenye gari akakimbilia kwa RPC aliyekuwa garini akaanza kugonga kioo cha gari kumsihi RPC afungue kioo. RPC akafungua kidogo tu na marehemu akaanza kumsihi kuwa yule waliyemkamata si mfuasi wa CHADEMA bali ni mwandishi wa habari. RPC akamtazama marehemu kwa dharau halafu askari wengine wakamdaka.Ndipo RPC akamgeukia askari mmoja "na kumwambia BOMU". Mara moja ukasikika mlipuko wa kutisha na marehemu akadondoka hapo hapo. Maaskari wengine wakalifuata gari la huyu mr. Joseph na kuanza kuligonga gonga, akalazimika kuondoka kwa kasi sana eneo la tukio kujinusuru.
Habari hii mliosikiliza wapo mtakuwa mmeisikia laivu kuto kwa dereva mwenyewe. Yaani bila kuumauma maneno kasema alimsikia RPC akitamka BOMU kabla ya huo mlipuko kutokea.
Quoted from​ Nyenyere