Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
OCD aliyeumia katika tukio na ambaye yuko critical condition hospitalini ni yupi katika kundi hili? Au huyo aliyevaa kiraia? Waliopo Iringa wanaweza kutupasha maana wanawajua watu wao.
Ushahidi huu apa eti police wanakanusha kweri wana akili angalia jamaa anavyo mlenga ili amuue untaka tume ya nini hapa au unataka ushahidi gani mwingine huyu police niwa wapi na sale alizo vaa nizanani ccm mmekuwa mawakala wa kuua watu kwa kutumia jeshi la police why?
Mkuu kosa la kwanza kabisa ni matumizi ya Silaha za moto dhidi ya raia ambao kimsingi ndiyo waajiri wa Polisi!.
Na ukiangalia vizuri Polisi waliokuwepo kwenye tukio ni zaidi ya wanne iweje watumie nguvu nyingi kwa mtu mmoja asiye na silaha, hadi kusababisha kifo cha kikatili hivyo?.
Huu ni uzembe mkubwa sana na lawama haziwezi kuwaendea polisi wadogo ila wakubwa wao wanaowapa ruhusa ya kufanya hivyo.
Pole sikuwa namaanisha bangi ila moshi wa mabomu. Hiyo picha yako itakuwa ni diffence ya polisi, marehemu anaonekana kakamata silaha ya askari.
Was the police intervention fully legal? Was the intervention based on a lawful objective, such as a valid arrest, detention, search, frisk, defense of a police officer or a citizen, or to prevent escape?
Was the use of force proportional to the person's resistance? Was there an urgent need to resolve the situation? Could the police officers have used lesser force and still safely accomplish the lawful objective?
Are the police officers well-trained, qualified and competent with all force tools authorized by the agency?
Is the police conduct objectively reasonable?
Mkuu nina feeling kwamba wengi humu jamii farums hamkusikiliza WAPO radio 98.0 FM. Kila siku saa moja na dakika 20 wana kipindi cha matukio asubuhi na jioni muda huo huo. I am not trying to sell them, ila wanajitahidi sana kutafuta wahusika halisi wa matukio. Hapa natoa kile nilichokisikia kutoka kwa DEREVA ALIYEKODIWA NA WAANDISHI WA HABARI kuwapeleka kwenye eneo la tukio (ndimo alimokuwamo marehemu). Dereva huyo amejitambulisha kama John Joseph.
Kwanza kabisa ameanza kwa kusema AMESHUHUDIA KWA MACHO YAKE TUKIO HILI MWANZO HADI KIFO CHA MAREHEMU. Wakati kikao cha ndani kinaendelea ghafla zikafika defender nne za FFU akiwapo OCD. OCD baada ya kuzungumza na viongozi wa CHADEMA na kumweleza kuwa hakuna mkutano wa hadhara akakubali waendelee, FFU wakawa nje. Mara akatokea RPC na gari lake. Yeye alipofika akasema NI AMRI TAWANYIKENI. Wananchi waliokuwapo nje ya ofisi WAKAJISALIMISHA KWA KUKAA CHINI NA KUNYOOSHA MIKONO JUU. Lakini hiyo isitoshe mabomu ya machozi yakaanza kumiminika kama mvua hovyo hovyo. Waandishi wakarudi kwenye gari lao. Ndipo polisi wakamdaka mwandishi mmoja na kuanza kumpa kipigo kikali. Kuona hivyo, marehumu akashuka kwenye gari akakimbilia kwa RPC aliyekuwa garini akaanza kugonga kioo cha gari kumsihi RPC afungue kioo. RPC akafungua kidogo tu na marehemu akaanza kumsihi kuwa yule waliyemkamata si mfuasi wa CHADEMA bali ni mwandishi wa habari. RPC akamtazama marehemu kwa dharau halafu askari wengine wakamdaka.Ndipo RPC akamgeukia askari mmoja "na kumwambia BOMU". Mara moja ukasikika mlipuko wa kutisha na marehemu akadondoka hapo hapo. Maaskari wengine wakalifuata gari la huyu mr. Joseph na kuanza kuligonga gonga, akalazimika kuondoka kwa kasi sana eneo la tukio kujinusuru.
Habari hii mliosikiliza wapo mtakuwa mmeisikia laivu kuto kwa dereva mwenyewe. Yaani bila kuumauma maneno kasema alimsikia RPC akitamka BOMU kabla ya huo mlipuko kutokea. Hebu sasa fanyeni MAGAZIJUTO!
Picha haijachakachulia ni sawa na ile ya mwanzo. Alichofanya ni kuweka mishale na maelezo kwenye picha.