PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

SAM_4973.JPG
 
Inapokuja mauti hadi Wauwaji Huuzunika!! Angalia Hao Waliokaa pembeni (Polisi) Hawaamini kilichotokea!! Ila ndio Hivyo tena Roho imeshatenganishwa na Kiwiliwili (Mwili) RIP Mwandishi Shupavu!!
 
mwisho wa kutufanya watoto sasa umefika, kwa pamoja tunaungana mabadiliko lazima yawe hata kama damu imwagike na wakae wakijua hawato maliza kutuua kwa mabavu yao wanayo yatumia, mabadiliko lazima
 
...Sijui kama hili litatokea Mkuu. Kikwete ni msanii wa hali ya juu na hana ubavu wa kufanya lolote lile. Siku zote ameweka mbele maslahi ya magamba badala ya yale ya nchi. Nchimbi, Mwema na RPC wa Iringa wote wanatakiwa kujiuzulu mara moja na polisi wote waliohusika na mauaji haya ya kinyama kuwekwa ndani mara moja na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.
Huyu ndiye annze maana vifo ni TZ nzima .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
huyo askari aliyepiga risasi ni kwamba anamori sana au vipi,ndo aonekane mfanyakazi bora ama/tena mbaya zaidi kuna mmoja anaonekana anazuia huo unyama,maana sielewi2 hapo

Hii lazima ilipangwa; na inavyoonekana sio wote hapo walikuwa wanaelewa huo mpango. Lakini huyo aliyeelekeza bunduki alikuwa anaelewa anachokifanya na matokeo yake. I have a feeling waliambiwa wa-uwe ili iwe fundisho kwa wengine (wanahabari na wananchi kwa ujumla wakatae kuhudhuria mikutano ya CDM kwakuhofia kuuwawa). Nafikiri ni strategy hiyo hiyo iliyotumika kwa Ulimboka; mpaka leo migomo mingi ata iliyo legit haifanikiwi kwasababu ya uoga.
However, jinsi wanavyofanya vitendo hivi hadharani nafikiri watu watazoea na kuwa kama wanyama. Kitakachotokea ni watu kuwa na mioyo ya ukatili, hujali tena kuua au kuuwawa unaona ni ajali tu kazini. Itakumbukwa zamani mtu ukiingiliwa na wezi unafikiria mara mbili umfukuze au kumkamata vipi; ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Sasa hivi mwizi au jambazi akinijaribu, hata sichukui dakika kufikiria kumuua on the spot. Sitaki kupoteza muda wakumfikisha kwenye vyombo vya sheria -nikupotezeana muda. Hiki ndicho kinachoelekea
kutokea TZ.
 
Polisi wakiwa kazini na kwenye vurugu hutakiwi kuwakimbilia na kuwakumbatia, unatakiwa ulale chini tena kifudifudi, kwenye sakata kama hilo hata kunyanyua mikono juu ni kujitafutia balaa.

Kumvamia askari na kumkumbatia ni kosa kubwa sana hususan kwenye fujo. Na kama kapigwa na polisi mwengine kwa chochote kile basi huyo Polisi hana makosa kwani anajuwa umemshambulia mwenzake.

Sheria inasema "the police can use "reasonable force" when faced with someone who is a threat to life "

Nani hapo ni "threat to life"?

Kwa akili yako kumuua huyo mwandishi mwenye camera mkononi ndio "reasonable force"?

Standards zako ni zipi?

Hata kama unachukia Chadema ukatili namna hii hauwezi kuhalalishwa. CCM italipa tu, na askari hao wamekamatwa wakiwa na damu mikononi. Wana murder case na utaona safari hii hawataepuka kama wale waliomtesa Ulimboka au waliomuua Ally kule Morogoro.
 
Nimejaribu tena kuziangalia picture kwa makini naona kuna surprises nyingi sana.

Jamaa kama alikuwa akijishika asianguke, pakawa na tafsir tofauti kwa skari wadogo kwa boss wao.Mikono yake imejisokotea kiunoni ila imefungwa na kushikilia camera.Police wanaweza kuwa walijikuwa hapo kwa kosa tofauti labda walikuwa wakimpa kipondo cha rungu na kumsukuma wakati akianguka reflex ikamtuma kujishika na askari bila kuweka fahamu sana.Hiii ikapelekea polisi wengine kuhisi "he was going for the officers gun".

Katika picture utaona askari wengine wakiwa busy na wengine kushangaa kilichotokea.Ni wazi police hawakupanga kuua (kwa staili hiyo) ila makosa ya mwanzo ndiyo yaliwafikisha hapo.Mpigaji angebahatika chukua video,basi tungeona marehemu alikaribia kwa kiasi gani katika tendo la kuwachanganya polisi kiasi hicho.Report ya police ikisema kuwa ni bomu lilirushwa baada ya kuwafikia polisi itapingana na hizi picture kwani,katik tukio la mabumu ya maadui si rahisi polise kuzubaa namna hiyo wakati hawana hakika kama bomu lingine linaweza kuja.Pangeonekana wengine wakijaribu thibiti chanzo cha mabomu na wengine wakiondoa majeruhi kwa haraka.

Kuna makosa ya mwanzo ambayo kama yangefanyiwa kazi palepale haya yasingefikia.Kama palikuwa na majibizano mkuu wa polisi angetumia mamlaka yake kumweka chini ya ulinzi bila jamaa kupata virungu pengine mamabo isingefikia hapa.Na ni wazi hata polisi nao hawakujiandaa kwa hiii hali,ndio maana hata press conferense ya yule afisa ilikuwa ya kujichanganya.

Hembu aliyekuwa katika tukio aweke brief Discriptions,ili polisi wapate msaada wa kutoa maelezo yatakayoruhusu ama kusema kosa lilifanyika wapi na ili jeshi likiri hayo maeneo ya makosa.Tuanze kuwa na mpango mpya kujenga nchi na kulinda raia na polisi.Damu ya huyu jamaa inaweza kuwa ni mwanzo wa Polisi kuwa na mahusiano mazuri na waandamanajiwa Chadema, raia na hata wao wenyewe.
 
Wenzake wakina Ritz na Rijao,Njiwa Kimyaaaaa!Kweli Zooomba!
 
Kikwete huu mwaka hauishi magogoni utakuwa unapasikia
 
Jamani huyo mwandishi alikosea nini, alikuwa jambazi na bastola? after all mbona jamaa kalala chini, na kuelekezewa mgobole?
Nilikuwa sina mtandao jamani nini kimetokea na watanzania mmefika je huko?
 
Duuuuh huu ni zaidi ya unyama aloo maana jamaaa kama ni kuwa nguvuni tayari alikua mikononi mwa polisi, iweje huyo polisi amlipue papo kwa papo? ingekua rungu ningesema imetua pabay lakini kumwelekezea mtutu wa kurushia bomu si kawaid hata kidogo. Kuna umuhimu wa kufanya la ziada kama mwanzisha mada alivyoshauri na kwa wenzetu wa kitua cha sheria watusaidie kumshitaki huyo askari najua anafahamika, IGP na RPC.

Nina wasiwasi kama askari hakutumwa kumwondoa Mwangosi basi ana kisa binafsi maana si kawaida bomu la machozi kumwelekezea mtu huwa linarushwa angani umbali fulani ili moshi uwashe macho.

Eee MUNGU utulinde utuongoze katika maamuzi yetu, tusiongozwe na hisia, chuki, itikadi au mambo mengine ya kidunia bali ubinadamu, busara na uchaji wako. MUNGU ailaze roho ya marehemu Mwangosi Mahala pema peponi. Na hili liwe ni chimbuko la mabadiliko katika mfumo wa mafunzo kwa askari wetu, maana tatizo ni mfumo. Amen
 
Nimejaribu tena kuziangalia picture kwa makini naona kuna surprises nyingi sana.

Jamaa kama alikuwa akijishika asianguke, pakawa na tafsir tofauti kwa skari wadogo kwa boss wao.Mikono yake imejisokotea kiunoni ila imefungwa na kushikilia camera.Police wanaweza kuwa walijikuwa hapo kwa kosa tofauti labda walikuwa wakimpa kipondo cha rungu na kumsukuma wakati akianguka reflex ikamtuma kujishika na askari bila kuweka fahamu sana.Hiii ikapelekea polisi wengine kuhisi "he was going for the officers gun".

Katika picture utaona askari wengine wakiwa busy na wengine kushangaa kilichotokea.Ni wazi police hawakupanga kuua (kwa staili hiyo) ila makosa ya mwanzo ndiyo yaliwafikisha hapo.Mpigaji angebahatika chukua video,basi tungeona marehemu alikaribia kwa kiasi gani katik tendo la kuwachanganya polisi kiasi hicho.Report ya police ikisema kuwa ni bomu lilirushwa baada ya kuwafikia polisi itapingana na hizi picture kwani,katik tukio la mabumu ya maadui si rahisi polise kuzubaa namna hiyo wakati hawana hakina kama bomu lingine linaweza kuja.Pangeonekana wengine wakijaribu thibiti chanzo cha mabomu na wengine wakiondoa majeruhi kwa haraka.

Kuna makosa ya mwanzo ambayo kama yangefanyiwa kazi palepale haya yasingefikia.Kama palikuwa na majibizano mkuu wa polisi angetumia mamlaka yake kumweka chini ya ulinzi bila jamaa kupata virungu pengine mamaboisingefikia hapa.Na ni wazi hata polisi nao hawakujiandaa kwa hiii hali.

Hembu aliyekuwa katika tukio aweke brief Discriptions,ili polisi wapate msaada ya kutoa maelezo yatakayoruhusu ama kusema kosa lilifanyika wapi na Ili jeshi likiri hayo maeneo ya makosa.Tuanze kuwa na mpango mpya kujenga nchi n akulinda raia na polisi.
Mkuu kosa la kwanza kabisa ni matumizi ya Silaha za moto dhidi ya raia ambao kimsingi ndiyo waajiri wa Polisi!.
Na ukiangalia vizuri Polisi waliokuwepo kwenye tukio ni zaidi ya wanne iweje watumie nguvu nyingi kwa mtu mmoja asiye na silaha, hadi kusababisha kifo cha kikatili hivyo?.
Huu ni uzembe mkubwa sana na lawama haziwezi kuwaendea polisi wadogo ila wakubwa wao wanaowapa ruhusa ya kufanya hivyo.
 
Mungu awalaani polic wote waliohusika katika mpango wa kumuua huyo mwandishi.
 
Polisi wakiwa kazini na kwenye vurugu hutakiwi kuwakimbilia na kuwakumbatia, unatakiwa ulale chini tena kifudifudi, kwenye sakata kama hilo hata kunyanyua mikono juu ni kujitafutia balaa.

Kumvamia askari na kumkumbatia ni kosa kubwa sana hususan kwenye fujo. Na kama kapigwa na polisi mwengine kwa chochote kile basi huyo Polisi hana makosa kwani anajuwa umemshambulia mwenzake.

Was the police intervention fully legal? Was the intervention based on a lawful objective, such as a valid arrest, detention, search, frisk, defense of a police officer or a citizen, or to prevent escape?

Was the use of force proportional to the person's resistance? Was there an urgent need to resolve the situation? Could the police officers have used lesser force and still safely accomplish the lawful objective?

Are the police officers well-trained, qualified and competent with all force tools authorized by the agency?

Is the police conduct objectively reasonable?
 
Ukitulia zaidi utajutia hata post yako ya kwanza.......hujawahi ona waandishi vitani.............(hata CNN/BBC)???????
Hata kama hakuwa na kibali......kuuliwa raia kinyama namna hii unahoji kibali????? Are you up your senses??????

Kimbweka wahed

Acha nae huyo kapotea jukwaa, hakuna anachojua zaidi ya...
 
Back
Top Bottom