PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Huyu takataka anatitafutia ban ya bure saa hizi! Unatetea wauaji!
 
WAPO radio 98.0 FM. Kila siku saa moja na dakika 20 wana kipindi cha matukio asubuhi na jioni muda huo huo. Wanajitahidi sana kutafuta wahusika halisi wa matukio. Hapa natoa kile nilichokisikia kutoka kwa DEREVA ALIYEKODIWA NA WAANDISHI WA HABARI kuwapeleka kwenye eneo la tukio (ndimo alimokuwamo marehemu). Dereva huyo amejitambulisha kama John Joseph.

Kwanza kabisa ameanza kwa kusema AMESHUHUDIA KWA MACHO YAKE TUKIO HILI MWANZO HADI KIFO CHA MAREHEMU. Wakati kikao cha ndani kinaendelea ghafla zikafika defender nne za FFU akiwapo OCD. OCD baada ya kuzungumza na viongozi wa CHADEMA na kumweleza kuwa hakuna mkutano wa hadhara akakubali waendelee, FFU wakawa nje. Mara akatokea RPC na gari lake. Yeye alipofika akasema NI AMRI TAWANYIKENI. Wananchi waliokuwapo nje ya ofisi WAKAJISALIMISHA KWA KUKAA CHINI NA KUNYOOSHA MIKONO JUU. Lakini hiyo isitoshe mabomu ya machozi yakaanza kumiminika kama mvua hovyo hovyo. Waandishi wakarudi kwenye gari lao. Ndipo polisi wakamdaka mwandishi mmoja na kuanza kumpa kipigo kikali. Kuona hivyo, marehumu akashuka kwenye gari akakimbilia kwa RPC aliyekuwa garini akaanza kugonga kioo cha gari kumsihi RPC afungue kioo. RPC akafungua kidogo tu na marehemu akaanza kumsihi kuwa yule waliyemkamata si mfuasi wa CHADEMA bali ni mwandishi wa habari. RPC akamtazama marehemu kwa dharau halafu askari wengine wakamdaka.Ndipo RPC akamgeukia askari mmoja "na kumwambia BOMU". Mara moja ukasikika mlipuko wa kutisha na marehemu akadondoka hapo hapo. Maaskari wengine wakalifuata gari la huyu mr. Joseph na kuanza kuligonga gonga, akalazimika kuondoka kwa kasi sana eneo la tukio kujinusuru.


Habari hii mliosikiliza wapo mtakuwa mmeisikia laivu kuto kwa dereva mwenyewe. Yaani bila kuumauma maneno kasema alimsikia RPC akitamka BOMU kabla ya huo mlipuko kutokea.

Quoted from​ Nyenyere
 
Reactions: Ame
Mkuu Nyeyere umesema kweli. Hawa jamaa WAPO ni mahiri sana katika kutafuta habari hasa katika kipindi chao cha Patapata. Mimi kila siku huwa nakisikiliza hicho kipindi hata leo nimekisikiliza. Ulichokisema ndicho walichokisema na dereva nimemsikia na RPC pia.
 
Last edited by a moderator:
maelezo ya mwandishi aliyeahuhudia tukio hili yanasema yeye ndiye aliyomba msaada kwa RPC na sio marehemu.
Je huyo alionyeshwa kwenye picha ni RPC?


KWA HISANI YA MTU WA TANZANI
 
TUTAYAJUA MENGI ..........kale ka-harufu ka WHO IS WHO in all these killings kanakaribia kupatikana......! na karibia mauaji yote ni tata, WANGWE....ARUSHA...IGUNGA....IRAMBA....MOROGORO...IRINGAAND it seems the MUNGIKI ooh sorry the killer is a proffessional that leaves no traces behind but "mshikwa na ngozi ndiye muhusika" INNOCENT who was present at the scene
 
Oh my my my

Hii nchi imefikia viwango vya udhalimu wa hali ya juu!
 
Hakuna ukweli wowote kuhusu kuchakachuliwa picha. Hii Picha ni ya ukweli kabisa huyo RPC asitake kukimbia kivuli chake kuhusiana na mauaji ya kinyama ambayo alishiriki.

 
Tusha washtukia ccm!mna taka kubadili ukweli ila msha chelewa sanaaa!nyambavv!
 
Alie nyoosha fimbo juu ni ocd nae amejeruhiwa kidogo mapajani.
 

Nilikuwa nailaumu na kuilaani idara ya usalam wa Taifa ila kwa utafiti wangu mdogo siku hizi mbili tatu nimegundua kuna ambao bado wanafanya kazi kwa stadi na mapenzi makubwa kwa nchi yao. Msife moyo hata sasa mumefanya kwa sehemu yenu nami nashukuru kwakuni linda japo niliamua kujilipua nione ni kiasi gani bado kama raia wa kawaida nikiamua ku-blo whistle naweza lindwa? Swali moja kwenu je kwanini mliingia kijambazi nyumbani kwangu nakuniibia electronic gajets zangu zote? Kama hamkukuta taarifa yeyote ya kihaini kwanini basi hamni rudishii kwanjia za kiintelijensia? Ama si ninyi wazalendo ni ile sehemu ya ninyi ambao wako upande wa mafisadi ndiyo wahusika? Mwenzenu hizo zilikuwa data base zangu zingine muhimu kwa maendeleo......Off point lakini hope mume nisoma!
 
Either way, in totality, CHADEMA gets more Political Mileage than CCM.
 
...Kuna umuhimu sana wa kuwa na camera popote pale nchini hasa kwenye maandamano ya CDM ili kuweza kupata ushahidi kama huu. Bila kuwa na hizi picha polisi magamba wangelibadili hili ili kuonyesha waliofanya mauaji ni CDM....

Tusha washtukia ccm!mna taka kubadili ukweli ila msha chelewa sanaaa!nyambavv!
 
Jaji mihayo ameulizwa km sheria zinaruhusu jesh la polis kushtakiwa, amesema inahusiwa na amewasii wanasheria wajitokeze kuisaidia familia kulishtaki jeshi la polisi

Channel ten kuna kipindi kinaendelea "Jenerali on Monday". Jaji Mihayo anasema Jeshi la Polisi linaweza kushtakiwa.
 
Reactions: Ame
Hii BAN inanukia tena naiona hivi hivi.........................................
 
Wewe na huyo dereva mmeshanunuliwa na wauaji, so mnataka kubadili ukweli.....? Kwani dereva ni nani hasa mpaka tuamini anachokisema na tukatae tunachokiona kwa macho?
 
haijalishi maelezo yapo vipi lakini upande wa polisi kuna kasoro,katika tukio zima sijaona kama kuna wafuasi wa chadema waliokaidi au kuambulia kichapo...nadhani kilichomponza marehemu ni ile hulka ya kiuongozi aliyokuwa nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…