PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

hawa policcm wanahangaika bure wakati wenzao wanaowatuma wakiumwa wanatibiwa nje ya nchi na sijawahi kusikia polisi akipelekwa nje ya nchi kutibiwa sasa wanashindwa kutumia akili kivipi?
 
elewa hapa, rpc katoka wapi kwenye hii picha wakati maelezo yanasema alikuwa kwenye gari?

marehemu hakuanzwa tu kwa kuuwawa, bali alichezea sana kichapo, wakati wakuchezea kichapo ndio wakati ambao rpc alkuwa kwenye gari, baadae rpc alishuka kutoka kwenye gari nakusogea eneohilo la tukio wakati mwandishi anapoteza uhai wake, kuna picha moja hapa inaonesha gari la rpc likiwepo karibu na maiti ya marehemu. embu nenda kwenye thread ya jana inayoonesha picha jinsi tukio lilivyokuwa linafanyika
 
elewa hapa, rpc katoka wapi kwenye hii picha wakati maelezo yanasema alikuwa kwenye gari?

Mama taratibu katika ushaidi wa picha na maneno unadhani upi ni wa kuaminika? Maanake mie naye naweza kusimulia pumba za uongo tu redioni na kwenye television bila ukweli wowote ule.
 
haya kazi kwenu washabiki wa siasa. .....ukweli unaanza kukaa sawa mnakimbia vivuli vyenu.....ghost killer yumo kati yenu.....!
 
wanazani ni tz ya mwaka gani wanadanganya kipumbavu hivi na wanatarajia tawaamini? its too late for those fools
 

Nitasikitika kama hata na CDM wataiacha hii ikapita bila kuonyesha grievances zao na seriousness kwenye maisha ya raia na professionals wanaoambatana nao kwenye politics zao. Kamanda Mbowe and Dr. Slaa please itoshe sasa....Diplomacy na watu ambao hawaongei luga moja na watanzania ya nini? Go a step ahead kuwatetea watanzania kwa vitendo!.....Grrrrrrrr!
 
Wajue tu hata wakiuwa hawatatumaliza kabwa sisi hatujawamaliza
 
TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF)
KWA VYOBO VYA HABARI
KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI


​
UTANGULIZI:
1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.


2. Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


3. Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.


4. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.


5. Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.


6. Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF inachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo.


MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF
Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:


1. Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi ambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo "target ya polisi" wanapokuwa kwenye kazi zao.

2. Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi la polisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.


3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.


4. Tunasema hivi kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.


5. Taarifa ambazo TEF tunazo, pia zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa "kuwashughulikia waandishi wa habari watatu" (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.


6. Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi' ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.


7. Vitendo vya aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia badala ya kuwa walinzi wa raia.


8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.


9. Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.




IMETOLEWA NA:


NEVILLE MEENA,
KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
SEPTEMBA 3, 2012
 
Reactions: Ame
kusingekuwepo na wapiga picha ccm wangetuingiza mjini, asante sana jf, bila chenga tumemwona arapisii akisema "BOM" tutavimba nae mpaka kisomeke.
 
Nye polisi mnataka kuwaaminisha watanzania kuwa ninyi ndio muna uchungu sana na ccm kuliko wtz wote? pengine hata kuwazidi wenye ccm?. Mbona mumeitoa kikatili roho ya mtoto wa mwenzenu?.mme wa fulani,baba wa akina fulani.machungu muliyo waachia hayatakoma dhidi yenu.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya shughuli za kiintelijensia na kukuna nazi nyumbani. Wewe mama, maneno hata mimi naweza kuwa na yangu, twende pamoja:

"wakati marehemu anapigwa na askari wapatao 8, nilimwendea RPC katika gari lake lililokuwa mita chache toka shughuli aliyoagiza ilipokuwa inafanyika na nilipoomba usaidizi wake alikuwa bize na radio akimhimiza askari kumaliza kazi. Kwa kuona hanisikilizi, niliamua kurudi machinjioni kuendelea kuchukua picha za kipigo. Baadae RPC alikuja kutoa last command na muuaji akafanya kazi yake"


Vipi hapo? Kakune nazi huko. Umbea wa mitaani unaleta hapa wakati watu tuna machungu
 
hii picha ilikuwa kwenye gazet la mwananchi, nahisi litafungiwa siku za karibuni
 

Picha hiyo imetokea mapema sana katika picha za tuko la awali, nafasi ya kuichakachua haikuwepo, kilichoongezwa baadaye ni maandishi ya ufafanuzi nani ni nani na nani anafanya nini. Tuachane na kasumba za vyama, chombo cha dola ni kwa wote, kesho yakikupata ndipo utakapoongoka, la sivyo kidonda cha mwenzio hakiumi hadi utakapopata donda mwilini mwako.

Umeshakubali kuwa RPC alikuwepo katika tukio hilo, ilishishudie anavyouawa mwandishi wa habari na wakati utafiti wa nipashe ni kwamba RPC ndiye aliyeamrisha bomu lipigwe.
 
jaman haya ni mauwaji yaliyokusudiwa kabisa huyu askari utadhan yeye hana damu hadi anamfanyia unyama kiasi hiki huyu mwandishi jaman kweliii.....!
 
elewa hapa, rpc katoka wapi kwenye hii picha wakati maelezo yanasema alikuwa kwenye gari?

Una roho mbaya sana Dr Kupeng'e, machozi ya watoto wa4 wa marehemu na mama yako si kitu kwako? unatafuta laana mwogope Mungu kidogo.
 
hivi ulimsikia mandishi aliyeojiwa na itv? anasema wakati marehemu anapigwa rpc alikuwa kwenye gari

Kama anasema alikuwa kwenye gari,shida ikwapi?inawezekana hamfahamu RPC,hilo halina maana kuwa polisi hawakumuuwa na RPC akiwepo maeneo hayo,maana gari lake linaonekana.Na hata kama hakuwepo kwenye na alikuwepo nje,ina maana hakutoa amri,ama amri yake haikusikilizwa,maana kuna wanaoonekana wakijaribu kumkingia marehemu asiendelee kupata kipigo,na kuna anayemwua marehemu live,sasa what is this **** all about?kwanza kama hakuwepo ndani ya gari ndo mbaya zaidi,kwani ameya engineer mauwaji hayo.
 
Either way, in totality, CHADEMA gets more Political Mileage than CCM.

Mkuu Mchambuzi hebu chambua kidogo. Hiyo mileage inatengenezwa na CHADEMA au ni Polisi wanaihujumu CCM ama ni CCM wanahujumiana? Nadhani kuna kitu kimejificha hapa hasa katika kufo cha huyu mwandishi wa habari. Kama picha ni za kweli inakuwaje mtu apigwe bomu katikati ya kundi la polisi na kutawanyika mwili mzima?
 
Last edited by a moderator:
AMA kweli jeshi la polisi limejaa mipumbavu,na mivuta bangi period!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…