Mkuu
Mchambuzi hebu chambua kidogo. Hiyo mileage inatengenezwa na CHADEMA au ni Polisi wanaihujumu CCM ama ni CCM wanahujumiana? Nadhani kuna kitu kimejificha hapa hasa katika kufo cha huyu mwandishi wa habari. Kama picha ni za kweli inakuwaje mtu apigwe bomu katikati ya kundi la polisi na kutawanyika mwili mzima?
Mkuu Kimbunga,
Asante sana kwa swali lako. Maana yangu kuhusu ‘Chadema na Mileage' ni kwamba matukio kama haya yana faida zaidi kwa Chadema kuliko CCM regardless nani ana makosa katika hili kwani kwa mujibu wa Katiba ya nchi, serikali (ambayo tangia uhuru ipo chini ya TANU-CCM), ndiyo yenye mamlaka ya kuunda majeshi yote ya ulinzi na usalama, hivyo jukumu la kulinda usalama wa raia wote na mali zao bila ya kujali dini, kabila, jinsia, political orientation, occupation (ajira) n.k, ni ya majeshi ya ulinzi na usalama, jeshi la polisi likiwa ni moja wapo. Kwa mfano, katika sura ya tisa ya katiba yetu, ibara ya 147, [sehemu 1,2, & 3] inatamka kwamba:
(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa
mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
Kwa maana hii, matarajio yetu kutoka jeshi la polisi ni kinyume cha yaliyotokea huko Iringa. Hata kama ilibidi jeshi litumie nguvu ya ziada, nguvu hiyo haina mahusiano na waandishi wa habari kwani
kazi yao pale sio ushabiki wa siasa bali wao
ni sikio la umma. Kama vile media wanapokuwa ni watu wa mwisho kuondoka kwenye press conferences, makongamano n.k, ilitakiwa iwe vivyo hivyo katika sakata la Iringa, na uwepo wa Polisi sana sana iwe kuwalinda waandishi wa habari na mali zao ili wakimaliza shughuli zao waondoke salama.
Lakini ukitazama the strained relationship iliyopo baina ya vyombo vya habari na jeshi la polisi kwa muda mrefu sasa, na pia the combative relationship iliyojitokeza baina ya CCM na Chadema in the context ya dhana za
Nguvu ya Umma versus
Amani na Utulivu, na vile vile given upepo wa kisiasa wa sasa nchini, in the final analysis juu ya tukio hili,
''Either Way', it is Chadema that gets more political mileage than CCM.
Sasa kuhusu maswali yako kwamba: (1) Who provides Chadema with the political mileage…, jibu langu ni ‘the political atmosphere in the country ambayo itaendelea to favour Chadema pengine mpaka uchaguzi mkuu ujao (2015);
Na swali lako la pili kuhusu mazingira ya kifo cha mwangosi kuwa ya utata, ni kweli, lakini sote tunatoa tu maoni yetu based on how mashahidi wanavyotujuza, na kwa vile we are both entitled to our own opinions, itabakia hivyo while we await for the facts kwani katika suala la facts, none of us is entitled. Lakini hata tukija pata the actual facts that gives an account of what happened, in totality,BADO it offers more political mileage for Chadema than CCM. That's the bottom line. Inawezakana majibu yangu yasiwe ya kuridhisha sana lakini ni kutokana na kuheshimu dhana ya kwamba We are all entitled to our own opinion but not our own facts.
Until then, tusubiri kupata
'Raw facts', not
'Processed facts';