Papizo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,253
- 2,166
Unajua wanachofanya hapa ni kutaka kuwaondoa watu katika mada ya MAUAJI YA POLISI. Jana zimewekwa picha zote kwa wakati mmoja na kila aliyeona tukio hakuna anayebisha hilo.
Nimesoma gazeti la mwananchi msemaji wa JESHI LA POLISI TANZANIA amekuja na madai ya kipumbavu na kijinga sana. Anasema Mwangos alikuwa anakimbia kutoka kundi la watu kuja kwa askari na kuna kitu kilirushwa kutoka kwa wananchi kikamuangukia tumboni.
Jeshi la Polisi linapoongoza kwa ujinga inatia wasi wasi. Ni ujinga kwasababu Msemaji wa jeshi hakujua kuwa picha zipo katika mtandao tayari. Sijui kama msemaji anajua hata key board ikoje achilia mbali kutafuta habari.
Matokeo ya kuwa na mazuzu kama hawa ni matumizi ya mabomu ya moshi kufumua watu.
Tayari amesha pre-empty uchunguzi wa IGP kwasababu tu idha ya mafunzo kidogo, au uweledi sifuri
Tatizo linalotukabili kama nchi ni ile tabia yetu ya kudhani kuwa ili uwe askari Polisi ni lazima uwe mjinga.
Tunajeshi lisilo na watu wenye uwezo kabisa. Imagine msemaji wa jeshi hajui nini kinaendelea katika nchi, je,askari aliye na risasi anajua kuitumia?
Jeshi la Polisi halina maana ya genge la watu wajinga au wapumbavu, halina maana watu wasiojua mazingira na mawasiliano.Jeshi la Polisi ni taaluma muhimu sana katika jamii kama taaluma zingine.
Kwakweli inauma sana! Niiweni radhi
Ifike wakati tuwe na jeshi la Polisi siyo wapuuzi, wajinga na mazuzu waliovaa uniform na kutoa roho za watu.
Mkuu si umeona hawa jamaaa wanajaribu kuja nakila namna ya kupoteza hii topic kil mtu anakuja na lake, sisi hatuitaji kujua kama RPC alikuwa kwenye gari au alikuwa wapi we don't care about that kwa sababu hizo picha inaonyesha kila kitu, kama ndio huyo RPC mmemuonyesha basi na yeye alihusika na achukuliwe haraka tu, tunachotaka kuona hawa jamaa wanachukuliwa hatuwa na hatutaki story za abunusi sijui RPC alikuwa kwenye gari au alikuwa kwenye tukio sisi hayo mambo hayatuhusu...
Hawa viongozi wa CCM na dhaifu wao ni watu waajabu sana kwa kweli sijapata kuona hata siku moja, yaani wanadiriki kufanya vitu alafu wanakuja kuropoka kwenye vyombo vya habari eti kitu kimemuangukia..Mkuu wangu hawa jamaa now wamekamatika so hawana ujanja now na hawajui waapi waanzie maana picha inaeleza kila kitu kipo wazi kabisa hawaajui nini watawaambia wananchi,
Hatuna Jeshi la maana zaidi ya vilaza na form 4 hawajui sheria zaidi ya kubuluzwa kama watoto wadogo, hamna kitu kabisame nawaonea huruma sana hawajamaa maana hamn kitu kabisaaa hata kidogo kichwani wapo empty kabisaaa....


