PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Haya yote yana baraka za Sirikali tangu ile kauli ya Liwalo na Liwee ni mauaji kwenda mbele nafikiri kuna mauaji yako mbele ya viongozi wa Chadem...Mungu okoa watu wako
 
RIP Mwangosya,
Damu yako iliyomwagika haitaondoka hivi hivi,
Familia yako inakulilia kwa unyama ulotendewa, hawana la kufanya.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu anyoshe mkono wake, kuuondoa madarakani utawala dhalimu na wamauaji wa ccm.
 
Damu mwanadamu nzito wakuu.majibu yatatoka kabla 2015.
 
hivi ulimsikia mandishi aliyeojiwa na itv? anasema wakati marehemu anapigwa rpc alikuwa kwenye gari

hata mimi nilisikia hizi habari zinaanza kuchakachuliwa,sijui tushike lipi kama leo tunaambiwa ni marehemu ndiye alimfata rpc, jana mwandishi mmoja kasema yeye ndiyo alimgongea rpc.tushike lipi?
 
Police kitaa msije kushika gongo wala bange,majambazi fresh tofauti na hapo mje mmejiandaa maana machungu juu yenu hayapimiki.
 
Kaka tutajie bas hata jina la hiyo link sisi tukatafte
 
Jeshi letu la polisi limekuwa genge la majambazi na wauaji kuna haja ya kulivunja mara moja. Wauaji mkono wa sheria ufuate mkondo wake.
 
Hili Gazeti halistahili kuitwa Gazeti la Uhuru bali Gazeti la Ukoloni waandishi wake hawaandiki habari za uhuru kama Jina la Gazeti


SAM_4974.JPG
Eti Chadema wafanya Vurugu tena???????
 
IMG_1875.JPG
Sura yake na Roho yake Vinafanana Bayaaaaaaa Tizama Tumbo hadi linataka kupasua Jezi za Polisi... Yaani hapo ana kiu ya Roho za Watu... Polisi mnatumiwa kama Ndom kisha Mnatupwa Wacheni kujiingiza kwenye Siasa za ccm Nafsi zenu zitakataliwa na Muumba...

Mnatia Kinyaa....
 
mwisho wa udhalimu haupo mbali ndugu zanguni! Mungu yu pamoja na watenda haki.
 
Mkuu Kimbunga,
Asante sana kwa swali lako. Maana yangu kuhusu ‘Chadema na Mileage’ ni kwamba matukio kama haya yana faida zaidi kwa Chadema kuliko CCM regardless nani ana makosa katika hili kwani kwa mujibu wa Katiba ya nchi, serikali (ambayo tangia uhuru ipo chini ya TANU-CCM), ndiyo yenye mamlaka ya kuunda majeshi yote ya ulinzi na usalama, hivyo jukumu la kulinda usalama wa raia wote na mali zao bila ya kujali dini, kabila, jinsia, political orientation, occupation (ajira) n.k, ni ya majeshi ya ulinzi na usalama, jeshi la polisi likiwa ni moja wapo. Kwa mfano, katika sura ya tisa ya katiba yetu, ibara ya 147, [sehemu 1,2, & 3] inatamka kwamba:

(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.

(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania.

(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Kwa maana hii, matarajio yetu kutoka jeshi la polisi ni kinyume cha yaliyotokea huko Iringa. Hata kama ilibidi jeshi litumie nguvu ya ziada, nguvu hiyo haina mahusiano na waandishi wa habari kwani kazi yao pale sio ushabiki wa siasa bali wao ni sikio la umma. Kama vile media wanapokuwa ni watu wa mwisho kuondoka kwenye press conferences, makongamano n.k, ilitakiwa iwe vivyo hivyo katika sakata la Iringa, na uwepo wa Polisi sana sana iwe kuwalinda waandishi wa habari na mali zao ili wakimaliza shughuli zao waondoke salama.

Lakini ukitazama the strained relationship iliyopo baina ya vyombo vya habari na jeshi la polisi kwa muda mrefu sasa, na pia the combative relationship iliyojitokeza baina ya CCM na Chadema in the context ya dhana za Nguvu ya Umma versus Amani na Utulivu, na vile vile given upepo wa kisiasa wa sasa nchini, in the final analysis juu ya tukio hili, ‘'Either Way', it is Chadema that gets more political mileage than CCM.

Sasa kuhusu maswali yako kwamba: (1) Who provides Chadema with the political mileage…, jibu langu ni ‘the political atmosphere in the country ambayo itaendelea to favour Chadema pengine mpaka uchaguzi mkuu ujao (2015);

Na swali lako la pili kuhusu mazingira ya kifo cha mwangosi kuwa ya utata, ni kweli, lakini sote tunatoa tu maoni yetu based on how mashahidi wanavyotujuza, na kwa vile we are both entitled to our own opinions, itabakia hivyo while we await for the facts kwani katika suala la facts, none of us is entitled. Lakini hata tukija pata the actual facts that gives an account of what happened, in totality,BADO it offers more political mileage for Chadema than CCM. That’s the bottom line. Inawezakana majibu yangu yasiwe ya kuridhisha sana lakini ni kutokana na kuheshimu dhana ya kwamba We are all entitled to our own opinion but not our own facts.

Until then, tusubiri kupata 'Raw facts', not 'Processed facts';

Mkuu nimekuelewa vyema. Ni wazi kwamba CDM wanapata mileage katika matukio haya kama ulivyosema hapo juu. Lakini sasa wasiwasi wangu ni juu ya kupata mileage kwenye matukio yanayohusisha vifo. Si vyema mtu ama chama chochote au serikali kupata manufaa yoyote kutokana na vifo; hayo manufaa yanakuwa haramu iwavyo vyovyote si vivuri kuhusishwa na manufaa yanayoambatana na vifo.

Wito wangu vyama hivi viwili pamoja na serikali vikae chini na kukubaliana jinsi ya kuendesha siasa katika nchi hii bikla kuathiri maisha ya raia wa nchi hii. Watanzania na maisha yao ni zaidi ya vyma vya siasa na hakuna chama au mtu mwenye haki miliki na nchi hii bali raia ndi wenye haki miliki na nchi yao wakiwa mmoja mmoja na si kundi.
 
Mie naomba niulize swali moja tu!!!

" KWA NINI CHADEMA WANAFANYA MAANDAMANO PASIPO KIBALI.....? "
We una matatizo ya kifikra, wamesajiliwa kama chama cha siasa, wanamuomba nani? I think you are short sited!
 
Back
Top Bottom