Mkuu n00b kama video ipo imwage kabla hatujalishwa uongo.
Naomba hii iwe katika kumbu kumbu.
Ikidhihirika kuwa Mwangos aliuawa kwa risasi/bomu au kiwacho kutoka kwa Polisi, msemaji wa jeshi Advera awajibike naye.
Lakini wa kuanzia tu, hivi huyu Said Mwema aliyeshuhudia mauaji lukuki ya raia bila kuwachukuliwa hatua wahusika, leo anawezaje kutuambia kuwa atafanya uchunguzi wa maana. Kwa moral authority gani inayoweza kukubalika.
Waziri Nchimbi aliyeunda tume iliyotoa taarifa za udanganyifu naye atawezaje kusimamia mambo ya ndani ya nchi katika kiwango cha chini cha uongozi kiasi hicho.
Rais aliyeapa kulinda watu na mali zao anachukua hatua gani dhidi ya wahalifu hawa wasio na utu, hisani wala huruma.
Na maswali machache yanalodhihirisha kuwa mauaji haya yalipangwa:
Hivi Mwangos(R.I.P) alikuwa na nguvu kiasi gani cha kuweza kuwashinda askari nane wenye silaha?
Mwangos alikuwa anajulikana Iringa nzima na nchi nzima, kwanini Polisi wasitafute utaratibu wa kumkamata bila kuathiri usalama wao au wa mtuhumiwa na wananchi wengine kwa muda muafaka.
Mwangos angetoroka aende wapi asikojulikana. Je, jeshi la Polisi lilitumia 'common sense' na professionalism kufikia judgement au liliongozwa na ujinga, ukosefu wa busara unaotokana na weledi duni
Kama ilibidi, narudia kama ilibidi sheria za jeshi zinaruhusu matumizi ya silaha pale tu iliporuhusiwa ikiwa ni pamoja na eneo wanaloweza kutumia silaha katika mwili wa mwanadamu. Je, kulitumika weledi, busara au hekima yoyote ile kuepusha madhara tunayoyaona. Je, Marehemu alikuwa mhalaifu kiasi cha kulipuliwa na mabomu?
Inasikitisha sana! Naona aibu kusema tuna jeshi la Polisi maana nikiangalia Polisi wa nchi zingine wanavyofanya kazi nadhani sisi tuna 'jeshi la valanti' linalojua kupakia risasi na kukamua trigger. Wakati wakifanya hayo ndani ya akili kunakuwa wazi na unaweza kujaza pamba.
Inauma, inasikitisha sana. Inauma kwakweli.