PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Bwana ametoa polisi wametwaa, tunajua duniani tunayodhiki, haki na amani kwa mwandishi itapatikana Mbinguni.
R.I.P Brother DM
 
Mkuu n00b kama video ipo imwage kabla hatujalishwa uongo.
Naomba hii iwe katika kumbu kumbu.
Ikidhihirika kuwa Mwangos aliuawa kwa risasi/bomu au kiwacho kutoka kwa Polisi, msemaji wa jeshi Advera awajibike naye.

Lakini wa kuanzia tu, hivi huyu Said Mwema aliyeshuhudia mauaji lukuki ya raia bila kuwachukuliwa hatua wahusika, leo anawezaje kutuambia kuwa atafanya uchunguzi wa maana. Kwa moral authority gani inayoweza kukubalika.

Waziri Nchimbi aliyeunda tume iliyotoa taarifa za udanganyifu naye atawezaje kusimamia mambo ya ndani ya nchi katika kiwango cha chini cha uongozi kiasi hicho.

Rais aliyeapa kulinda watu na mali zao anachukua hatua gani dhidi ya wahalifu hawa wasio na utu, hisani wala huruma.

Na maswali machache yanalodhihirisha kuwa mauaji haya yalipangwa:
Hivi Mwangos(R.I.P) alikuwa na nguvu kiasi gani cha kuweza kuwashinda askari nane wenye silaha?

Mwangos alikuwa anajulikana Iringa nzima na nchi nzima, kwanini Polisi wasitafute utaratibu wa kumkamata bila kuathiri usalama wao au wa mtuhumiwa na wananchi wengine kwa muda muafaka.
Mwangos angetoroka aende wapi asikojulikana. Je, jeshi la Polisi lilitumia 'common sense' na professionalism kufikia judgement au liliongozwa na ujinga, ukosefu wa busara unaotokana na weledi duni

Kama ilibidi, narudia kama ilibidi sheria za jeshi zinaruhusu matumizi ya silaha pale tu iliporuhusiwa ikiwa ni pamoja na eneo wanaloweza kutumia silaha katika mwili wa mwanadamu. Je, kulitumika weledi, busara au hekima yoyote ile kuepusha madhara tunayoyaona. Je, Marehemu alikuwa mhalaifu kiasi cha kulipuliwa na mabomu?

Inasikitisha sana! Naona aibu kusema tuna jeshi la Polisi maana nikiangalia Polisi wa nchi zingine wanavyofanya kazi nadhani sisi tuna 'jeshi la valanti' linalojua kupakia risasi na kukamua trigger. Wakati wakifanya hayo ndani ya akili kunakuwa wazi na unaweza kujaza pamba.

Inauma, inasikitisha sana. Inauma kwakweli.
 
Mwema na ujumbe wake mpaka sasa wangekuwa wamejiuzulu..mliwafanya wazazi wetu mabwege ila sisi hamtakaa mtushikie chini.
 
Hapo ndipo tulipo!Kweli amani yetu ipo rehani.TUSALI SANA ILI MUNGU atusaidie kuondokana na roho za kikatili kama hizi za hawa wauaji.

UKAPUMZIKE KWA KWA AMANI NDG YETU,MUUMBA ATAHUKUMU.
 
Inasikitisha sana jamani, hizi series za matukio ya kinyama yanayofanywa na jeshi letu la polisi nayalaani vikali mno.hv kweli hadi rpc na rco wapo kwenye tukio wakathubutu kushuhudia kitendo kama hicho? Sidhani kama kuna haja ya kuunda tume tena tume yenyewe wahusika wawe ndo viongozi unategemea kitu gani hapo? Kumbukeni hata paka ukimkimbiza sana akiona hana jinsi husimama gafla kujiweka tayari kwa lolote,atapambana vkali dhidi ya adui kwa makucha yake coz peaceful means imeshindikana.hvyohvyo hawa raia wanaoteswa namna hii itafikia mahali watastop gafla na ndipo revolution ya aina yake itatokea.2015 hawa askari ndo wataua kama njugu.
 
Siku yaja ambayo jk ,mwema na wote wanaounga mkono matendo haya watalia na kusaga meno, halita salia neno jambo ovu hata moja ambalo halita tolewa hesabu yake na malipo yake hahapa duniani.
 
Hizi picha tuzitume kwenye balozi zote hapa Tanzania,zifike kila pembe ya duniani hasa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ,umoja wa mataifa,tume ya kutetea haki za binadamu nk.Hii inaweza saidia kilio chetu wanyonge kusikika zaidi hasa kwa matukio haya ya karibu yaani la Moro na Iringa.
Tuzitume kwa wingi kadili tuwezavyo.
 
Hiyo hapo kwenye picha ya kwanza ndiyo njemba ambayo inataka kukimbia kivuli chake cha kushiriki kwenye mauaji ya kinyama kwa kudai kuwa ilikuwa ndani ya gari. Huu ni ushahidi mwingine wa kuonyesha hakuwemo ndani ya gari hivyo anastahili kabisa kupandishwa kizimbani kwa kesi ya mauaji.
 
Kweli inaashiria dola sasa imeshindwa kuiongoza nchi hii. Nadhani ni muda muafaka wa kufanya mabadiliko,haiwezekani tukio kama hili limeshuhudiwa na majority ya watanzania leo hii msemaji wa jeshi la polisi anasema alirushiwa kitu kutoka kwa wananchi ambao wanadai ni wafuasi wa NGUVU YA UMMA(CHADEMA).Wakati picha zote znaonyesha wanavyompigania ka mpira wa kona? Tena mtu mmoja jamani kundi lote hila na silaa zao utadhani walikuwa wanapambana na master flani hv kumbe wapi maskini wa mungu ni mtu wa kawaida tu.
 
hivi itakuwa imemumuua risasi au bom la machozi maana sidhani kama risasi inaweza kusambaratisha mwili wa mwanadamu kama hivyo.tueleweshane wana great thinkers
 
Ndoano! Kwa uelewa wangu mdogo wa explosives kusambaratishwa kwa mwili wa Daudi Mwangosi ni "effects of firing of tear gas gun at the human body at A VERY CLOSE RANGE" ndiyo kilichotokea na ndiyo maana OCS amejeruhiwa kwenye mguu kwa sababu yeye na marehemu walikuwa in proximity of each other.
 
kwanini wanyakyusi tu. Prof mwandosya , dr mwakyembe, dr ulimboka na sasa mwangosi who is going to be next victim from mbeya
 
Inasikitisha sana. Cha ajabu, sijasikia kama kuna polisi wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya ndugu Mwangosi. Ingekuwa ni vizuri polisi wote wanaooneka kwenye hizo picha watiwe mbaroni wakati uchunguzi ukiendelea wasije wakatoroka kama alivyotoroka koplo Saadi kwenye ile kesi ya kina Zombe.
 

So Mungu amemua? sasa kuna haja gani ya sisi kuomboleza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…