Huyu anaweza kutoa ushahidi, ndani ya Polisi kuna wazalendo wa kweli akiwemo yule aliyejinyonga Morogoro ambaye alitaja watuhumiwa wanaolichafua jeshi la polisi, nawaachia vionozi hebu cheki huyu:
Askari huyu bila shaka alijeruhiwa na bomu hilohilo lililomuua Mwangosi an hapa alikuwa anasubiri kuondolewa. Tazama kwa makini umri wa askari aliyemfyatulia Bomu Mwangosi, ni Kijana mdogo kabisa, na tabia hii ya jazba ya vijana inahitaji ushauri ama sivyo itatupeleka pabaya.
Tatizo la uwezo wa vijana katika kutetea yanayowahusu si la CCM peke yake, CHDEMA pia wako kwenye shida hii ya kumudu hisia za vijana, na wakati mwingine wanatoa msimamo wa chama kusuppport ubaya uliyotendwa na vijana ili mradi tu kulinda support yao vijana kwa chama.
Tunahitaji kufanya jambo kuwasaisia viajana wetu kuchukua nchi hii katika umoja na kuheshimu mawazo ya kila mmoja si vitisho na ubabe wa upande wowote ule ukiwemo wa wale wanaosema damu itamwagika au nchi haitatawalika, kwani mimi nisiamini unachoamini si ndugu yako? Kwahiyo Dawa ni kuniangamiza, la hasha.
Na wale wanaotumia dola kuwaumiza wenye itikadi tofauti ilimradi tu uufurahishe utawala, unasahau kuwa utawala wa Mh Kikwete hauwezi kukulinda utaumbuka na kustaafu kwako kutakuwa kwa aibu ka isa sijui hamsomi alama za nyakati? Waulizeni akina Mgonja, je wewe ni nani?
TUHEHIMIANE NA TUDUMISHE UMOJA hata kama tuna mawazo tofauti.