Tukishamjua halafu what next?
Tuachie vyombo husika vifanyie kazi hili swala, huko itakuwa kuanzisha ugomvi, fujo, mfarakano baina ya raia na askari.
Kwenye picha hizi mbili who is who?
Tukishamjua halafu what next?
Tuachie vyombo husika vifanyie kazi hili swala, huko itakuwa kuanzisha ugomvi, fujo, mfarakano baina ya raia na askari.
Ugomvi wameuanzisha wao,kukusema ukweli nchuki wameanzisha wao ,sisi raia tulikuwa wavumilivu saana ila sasa uvumilivu unafikia mwisho.Mimi sina imani kabisa na jeshi hili maana wamekuwa watu wakutumia nguvu nyingi mno pasipo sababu ya msingi.Tukishamjua halafu what next?
Tuachie vyombo husika vifanyie kazi hili swala, huko itakuwa kuanzisha ugomvi, fujo, mfarakano baina ya raia na askari.
mkuu tume iliyoundwa ikipita ni vema mkamwaga huu ukweli unaotisha..dahMimi niko Nyololo, 2kio la mauaji ya Mwangosi tulishuhudia toka mwanzo mpaka mwisho. Ffu walitoka sehemu mbalimbali hivyo kuwatambua kwa majina ningumu kidogo labda askari wanaofanyanao kazi waliopo humu watutajie. Mpaka sasa wamekuja watu tofautitofauti sehemu ya2kio, kuna wataalamu wa satelite wametega vyombovyao pale tangu juzi cjui wanataka nn. Kjiji kimeandaa watu 50 walioona kutoa ushahidi na wamesema wataeleza ukweli walichokiona, chakushangaza wale hawajahojiwa mpaka sasa badalayake wamechukuliwa watu tusiowafahamu na co wahapa na hawakuwepo eti ndo wanahojiwa. Sisi kama wananyololo tunashangaa eti kamati zinaundwa na magari yanakuja kilasaa eti kufanya uchunguzi wakati tumeona kwamacho yetu Mwangosi akipigwa risasi na kupoteza ushahidi wa risasi wakamlipulia bomu lisambaratishe mwiliwake hasa sehemu alopigwa risasi. POLISI WAMEMPIGA RISASI NA KUMLIPULIA BOMU. Anaebisha ajehapa Nyololo aulize wananchi waliokuwepo nikiwemo mimi. Ninamengi yakueleza ilangoja niishie hapa. Mniulize maswali niyajibu khsu 2kio zima.
Wana JF,
Naomba mniruhusu niweke picha zenye sura za walioshiriki kitendo hiki cha kihuni ambacho ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama kamera yangu ilivyokinasa.
Nina picha ambazo zimechukuliwa zinazoonyesha walioshiriki na jinsi walivyoshiriki. Hata RPC alikuwepo eneo la tukio.
Mods, naomba msiunganishe thread yangu plz.
Picha nyingine nimezituma kwa watetezi wa haki za binadamu na video nimeziweka YouTube (sitatoa link kwa sasa).
Wanahabari, ni wakati wa kuonyesha umoja wetu dhidi ya udhalimu huu.
-----
Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.
Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio
Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.
Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.
Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.
Mimi siamini kuwa hao FFU walitoka DAR, Kwanini walete kikosi kizima cha FFU kutoka Dsm wakati kila mkoa una kikosi cha FFU kwa ajili ya kazi za kutuliza ghasia? Iringa Pale Kihesa kuna kambi kubwa ya FFU ambayo inatosha kwa shughuri zote za mkoa wa Iringa. Nadhani hii nadharia imepandikizwa ili kupoteza upelelezi.Jamani kuna watu nyororo ambao wanaumia na kitendo hki na askari mmoja amesema ataleta majina na huyo anayesadikika kumuua lakini kasema ak4undulika tu hatuta muona nch hii tena lakini anasema ffu hao wametokea dar
Tunahitaji kuwa reformed. Tanzania ya Mwl si Tanzania ya leo.mkuu hebu ziweke wakati mods wanatafakari !
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA