Profesa
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 903
- 629
Serikali lazima ijisafishe kihalali kwa kutenda haki kwa hili isifanye utoto wa kufunikafunika mambo kwa ushabiki wa chama. Kwani Polisi wana chama? Hata kama mimi ningekuwa kiongozi wa serikali leo, ningetangaza kuchukuliwa hatua za kinidhamu askari aliyehusika na viongozi wake, kwakuwa hali inaonyesha kuwepo kwa kila dalili za askari wadogo kutokutiii amri halali iliyokuwa ikitolewa na kamanda wao akionyesha kama anazuia kuendlea kusulubiwa kwa raia aliyekuwa amemshika "akimsihi??". Na pia uchunguzi ufanyike kama kijana huyu aliwahi kutumia silaha kama hii na kama anajua ukimlenga mtu inaleta madhara gani? Yaonekana hakuwa ana uzoefu wakuitumia, au alidhani akifanya hivyo atasifiwa. Kwa serikali hili ni doa na yeyote anaehusika achukuliwe hatua za kinidhamu hata kama ni za kijeshi, kuiweka serikali pasafi. Tukio hili linatia doa kabisa ubora na kiwango chetu cha utkelezaji wa Haki za Binadamu tena kwa nchi ambayo inaonekana kuwa na amani kama Tanzania.
Jeshi la polisi hata kama ni la kuzuia ghasia lisipokuwa na nidhamu ni tatizo kubwa.
Jeshi la polisi hata kama ni la kuzuia ghasia lisipokuwa na nidhamu ni tatizo kubwa.