PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Kwenye Picha ambayo DM alikuwa anaongea na RPC unaona kuwa polisi wengine wote walikuwepo hivyo basi walimuona na walimtambua kuwa huyo ni Mwandishi wa habari. Kwa hiyo sababu ya kuwa hakuvaa Press Vest haiwezi kuwa na nguvu. Lakini hata kama tutakubali kuwa hakuvaa kizibau cha waandishi wa habari kwa hiyo jeshi la polisi lilishindwa kumtofautisha na wananchi wengine, Je hao wananchi wengine ndio wauwawe na Polisi?

Kwani Polisi wanaruhusiwa kuua raia yeyote isipokuwa mwandishi wa habari?
 
Wakitambuliwa kwa majina itakuwasafi sana maana hata wasipofikishwa mahakamani tutawapa treet justice iringa nyororo tunasubiri
Kweli mkuu,serikali hii unadhani itawaadhibu???aaa wapi sana sana watahamishiwa mikoa mingine kuwaficha,hiyo haitakuwa dawa issue hapa tuwatambue ngoma ni mitaani wamuulize msangi yule mtesaji wa ulimboka hadi aliomba uliinzi mtaani kunatisha.wapo jamaa wa pikipiki watashughulika nao tu.
 
there you are Emerald.....mi nachoka ninapoyawaza majibu ambayo ni kinyume na tuyafikiriyo

Saa ingine tunayowaza ni tofauti sana na reality...ila kimsingi, R.P.C angepisha uchunguzi kwanza, and then tukiwa tunaendelea kuwaza...That would suffice.
 
Wale wa ulimboka walitajwa kwa majina lkn hakuna kilichofanyika na tupo nao tu mitaani kwa raha zao na sisi watz tumenyamaza kimyaaaa....sasa hayo majina ya waliomuua mwangosi tutayafanyia nini?
Watz tumekuwa mazuzu sana!

nani kakwambia akina Rama wapo mitaani?
 
nasikia hao polisi wametoka dodoma
walipo wasakwe washikishwe adabu manake wanaishi mitaani na sisi.
kama jamabazi au kibaka anaeiba kuku anauwawa iweja huyu aliuwa mwandishi asie na hatia abaki hai?
 
updates? watu wa magazeti tayari wamepewa baadhi ya majina wa mapolisi. hakuna waandishi jasiri watupatie hayo majina?
 
updates? watu wa magazeti tayari wamepewa baadhi ya majina wa mapolisi. hakuna waandishi jasiri watupatie hayo majina?

Gazeti la Tanzania Daima la leo Ijumaa tar 7 Septemba limewataja wawili, Mwampamba (yule aliyekuwa anawazuia wenzake) na Gabriel (aliyekuwa ameshikilia bastola)
 
Gazeti la Tanzania Daima la leo Ijumaa tar 7 Septemba limewataja wawili, Mwampamba (yule aliyekuwa anawazuia wenzake) na Gabriel (aliyekuwa ameshikilia bastola)

Safiii! Watatu wameisha julikana sasa, Kamuhabwa,Mwampamba na Gabriel. Kuna hawa wengine waliotoka nje ya mkoa Iringa bado majina yao!
 
Mungu wangu, huyu wamemkatakata kwa panga au ni risasi tu? Ee Mungu, inusuru nchi yako hii!!!!!!!!!!!!!
Hadi mwili unasisimka halafu NAPE bila aibu anasanifu wa Tanzania leo kwa media ati kunahitajika uchunguzi ili kubaini waliomuua mwandishi huyo.Mungu kamwe hawezi kuyanyamazia haya
 
Nnatamani kinuke tu,kama tabu,mateso na kila aina ya mateso imekuwa km ni sehemu ya maisha yetu,ni bore tukinukishe tu.
 
Wana JF,

Naomba mniruhusu niweke picha zenye sura za walioshiriki kitendo hiki cha kihuni ambacho ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama kamera yangu ilivyokinasa.

Nina picha ambazo zimechukuliwa zinazoonyesha walioshiriki na jinsi walivyoshiriki. Hata RPC alikuwepo eneo la tukio.

Mods, naomba msiunganishe thread yangu plz.

Picha nyingine nimezituma kwa watetezi wa haki za binadamu na video nimeziweka YouTube (sitatoa link kwa sasa).

Wanahabari, ni wakati wa kuonyesha umoja wetu dhidi ya udhalimu huu.

-----​

attachment.php

Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.


attachment.php

Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio

Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.

attachment.php

Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.

Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.
Damu ya watu wasio na hatia na iwe juu yao serikali na taasisi zake zote hata mwisho wa dahari
 
Duh! Huyu jamaa walimua kinyama. Hawa wahusika wachuliwa hatua ipasavyo.
May his heart rest in the bosom of the Lord.
 
Back
Top Bottom