PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

RIP Mwangosi najua umetangulia hata walo kutanguliza nao watafata,Mungu anajua
 
mambo nje nje namna hii tume ya nini? watu wanaonekana na wanajulikana? mtu mmoja, tena mwandishi alihitaji kweli askari saba wenye silaha? hao askari sasa wako wapi? wako huru tu au wameshafichwa? kuna maswli mengi hayana majibu na majibu yake hayahitaji tume!
 
Umeona JG jamaa wa nyololo ni muhimu kutoa ushahidi lakini utashangaa tume haitawafikia

Si umemsikia jamaa mwenyewe kasema pale kijijini wameenda kuchukuliwa watu wengine kabisa na kuwaacha mashuhuda halisi....

Ila leo Tendwa kajibu mafumbo yote haya.... wanajiandaa kuwatest watz kuota ndoto ya kukifuta CDM!
 
Dah, inatosha kujua polisi wa Tanzania hufanya mauaji mengi kwa raia. Hawana kabisa busara za kushughulikia matukio ya namna hii.

Wamemuua Mtanzania mwenzetu kama mnyama, ni nini hasa alichowakosea? Aliwafanya nini kibaya hadi mkawa na hasira naye namna hii?

Hakuwa na haki ya walau kuwekwa kizuizini kama mnavyowaweka wanasiasa inapotokea vurugu za namna hiyo? Mmemdhalilisha akiwa hai kwa kumpiga kwa kumshambulia na bado mkadhalilisha maiti yake kwa kifo hiki.

Aliwakosea nini ninyi polisi?
 
hii inatukumbusha soweto enzi hizo, wakaburu walikuwa hawakawii kuua! tanzania tunayoipenda haikuwa ya mauaji ya kuholela tena kutumia vyombo vya dola!
 
Kwa picha hizo,tume haina kazi hapo,,,tama mimi mwenyewe ningemaliza kazi,kamata hao wenye sura wote,the hegue moja...
 
hapa ndipo napolikumbuka gazeti mwanaharisi.
 
Seriously hawa Polisi inabidi wote wawajibishwe.........ni uzembe wa hali ya juu......idara ya mafunzo nayo ivunjwe kabisa..........
 
Umbea tuu hamna cha kufanyaaaa!!

Uko sawa kabisa, ni umbea na kukosa cha kufanya.
Si kwa sababu alokufa hakuhusu wala huna uchungu naye?! Na kwamba wewe hitakufa milele?
Ngoja cku uone 'mzoga' wa ndugu yako halafu ujaribu kumtafuta mhusika mtu akwambie "Umbea tuu hamna cha kufanyaaaa!!" nafikiri ndio utajisikia kama wanavyojisikia ndugu wa Mwangosi leo.
Leo kwao, kesho kwako.
 
nimeupitia huu uzi kwa kina zaidi, lakini nimeambulia haya hapa:

[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]1. Watambulike na majina yao yawekwe hadaharani, lakini wa kwamna muuaji ni huyo RPC Semuhanda
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 628, bgcolor: transparent"]2. SACP Michael Kamhanda ambaye alikuwa eneo la tukio kama kiongozi wa polisi
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 628, bgcolor: transparent"]3. Huyo dogo aliyeshika mtutu (uliomlipua marehemu) nahisi ni Abdallah Balawazi (Sina hakika sana kwani sura yake siipati vizuri hapo kwa sababu ya hilo likofia). Mwenye jina nililolitaja hapo ni askari wa kutuliza ghasia pale Morogoro na anafanana kwa kila kitu na huyo jamaa...hata sura yake naifananisha na huyo kwa asilimia 80%.
Kama kuna mtu anaweza kufanya uchunguzi kutoka hapo nilipoishia mimi tunaweza tukathibitisha kuwa huyo ni Abdallah Balawazi.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 628, bgcolor: transparent"]4. Mtu mwenye kofia (Barret) aliyekumbatiwa na Daudi ambaye anasemekana kuwa ni mkuu wa kituo cha polici Mafinga na ambaye inasemakana pia kuwa huenda ndio alitoa order ya kuua kwa askari waliokuwa na siraha ni nani kwa jina
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 628, bgcolor: transparent"]5. Nina wasiwasi sana na huyu jamaa alievaa shat la mikono mifupi na kushika bendera. Huyu sio askari wa iringa. Huyu amekuja special kwa kazi ya uuaji. Hapa kuna kitu kizito sana nyuma ya hili. Iweje wammkamate mwandishi tu na sio mwananchi mwingine wa kawaida? Kipindi kidogo nilishawahi kusikia harakati za huyu Marehemu katika tasnia ya habari hapo Iringa
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 628, bgcolor: transparent"]6. Michael Kamhanda
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


 
Watanzania wa leo sio wa miaka ya 60. Kwa woga huu tusingeweza kupata Uhuru kabisa. Na ndivyo tutazidi kunyanyasika tu maana hatujui kutetea haki zetu.
 
Katika hili suala la mauaji kuna maswali mengi zaidi ya majibu, let's think out aloud...
 

Una bonge la biti mkuu..
Enhee, halafu tukishawajua itatusaidiaje!?? sisi ndo tutaenda kufungua mashitaka ama!??
 
Mimi ningekuwa Iringa nikimfahamu askari naanza kumvizia yeye, mke wake, mtoto wake au wazazi wake. Naua mmoja baada ya mwingine silently! Wananchi tukiua Polisi 3 kwa wiki kwa mwezi mmoja it means 12 a month. Lazima serikali ishtuke!


sikubaliani na hili......wakati mnawaua 12 wao watakiwa kimya tu! huo mtaa ambapo mauaji yamefanyika utabai shwari tu? wakati mnaanza moja...mbili...tatu nyie idadi yenu itakiwa imefika ngapo?????
 
Wale wa ulimboka walitajwa kwa majina lkn hakuna kilichofanyika na tupo nao tu mitaani kwa raha zao na sisi watz tumenyamaza kimyaaaa....sasa hayo majina ya waliomuua mwangosi tutayafanyia nini?
Watz tumekuwa mazuzu sana!
 
Katika hili suala la mauaji kuna maswali mengi zaidi ya majibu, let's think out aloud...

there you are Emerald.....mi nachoka ninapoyawaza majibu ambayo ni kinyume na tuyafikiriyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…