Kwenye Picha ambayo DM alikuwa anaongea na RPC unaona kuwa polisi wengine wote walikuwepo hivyo basi walimuona na walimtambua kuwa huyo ni Mwandishi wa habari. Kwa hiyo sababu ya kuwa hakuvaa Press Vest haiwezi kuwa na nguvu. Lakini hata kama tutakubali kuwa hakuvaa kizibau cha waandishi wa habari kwa hiyo jeshi la polisi lilishindwa kumtofautisha na wananchi wengine, Je hao wananchi wengine ndio wauwawe na Polisi?
Kweli mkuu,serikali hii unadhani itawaadhibu???aaa wapi sana sana watahamishiwa mikoa mingine kuwaficha,hiyo haitakuwa dawa issue hapa tuwatambue ngoma ni mitaani wamuulize msangi yule mtesaji wa ulimboka hadi aliomba uliinzi mtaani kunatisha.wapo jamaa wa pikipiki watashughulika nao tu.Wakitambuliwa kwa majina itakuwasafi sana maana hata wasipofikishwa mahakamani tutawapa treet justice iringa nyororo tunasubiri
there you are Emerald.....mi nachoka ninapoyawaza majibu ambayo ni kinyume na tuyafikiriyo
hapa ndipo napolikumbuka gazeti mwanaharisi.
Wale wa ulimboka walitajwa kwa majina lkn hakuna kilichofanyika na tupo nao tu mitaani kwa raha zao na sisi watz tumenyamaza kimyaaaa....sasa hayo majina ya waliomuua mwangosi tutayafanyia nini?
Watz tumekuwa mazuzu sana!
updates? watu wa magazeti tayari wamepewa baadhi ya majina wa mapolisi. hakuna waandishi jasiri watupatie hayo majina?
Gazeti la Tanzania Daima la leo Ijumaa tar 7 Septemba limewataja wawili, Mwampamba (yule aliyekuwa anawazuia wenzake) na Gabriel (aliyekuwa ameshikilia bastola)
Hadi mwili unasisimka halafu NAPE bila aibu anasanifu wa Tanzania leo kwa media ati kunahitajika uchunguzi ili kubaini waliomuua mwandishi huyo.Mungu kamwe hawezi kuyanyamazia hayaMungu wangu, huyu wamemkatakata kwa panga au ni risasi tu? Ee Mungu, inusuru nchi yako hii!!!!!!!!!!!!!
Damu ya watu wasio na hatia na iwe juu yao serikali na taasisi zake zote hata mwisho wa dahariWana JF,
Naomba mniruhusu niweke picha zenye sura za walioshiriki kitendo hiki cha kihuni ambacho ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama kamera yangu ilivyokinasa.
Nina picha ambazo zimechukuliwa zinazoonyesha walioshiriki na jinsi walivyoshiriki. Hata RPC alikuwepo eneo la tukio.
Mods, naomba msiunganishe thread yangu plz.
Picha nyingine nimezituma kwa watetezi wa haki za binadamu na video nimeziweka YouTube (sitatoa link kwa sasa).
Wanahabari, ni wakati wa kuonyesha umoja wetu dhidi ya udhalimu huu.
-----
Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.
Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio
Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.
Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.
Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.