KWELI Picha hii kuonyesha barabara ikiwa imeharibika imetengezwa kwa kutumia Akili unde

KWELI Picha hii kuonyesha barabara ikiwa imeharibika imetengezwa kwa kutumia Akili unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
669811990_897844969977503_2601158001882074_n.jpg
​
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na picha inayosambazwa na baadhi ya watumiaji kwenye mtandao wa Facebook, ikionesha barabara ikiwa imeharibika vibaya. Picha hiyo imeenea kwa kasi katika vikundi mbalimbali, huku ikitumika kuunga mkono madai kwamba serikali barani Afrika hazifanyi kazi kwa ufanisi. Baadhi ya watumiaji wameihusisha hali hiyo na uzembe pamoja na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Katika muktadha huo, mojawapo ya kurasa za Facebook, Maravi Post, ilichapisha nukuu isemayo: “Death trap: Balaka–Liwonde–Zomba Road… Where are you noisy Roads Authority (RA)?”

Vilevile, ukurasa wa Medy Chris ulichapisha : “Hali ya mvua imepungua kwa kiasi kikubwa kwa sasa nchini Tanzania. Vipi hali ya barabara huko kwenu? Bado ni safi kama awali, imeharibika kiasi, au hali ni mbaya kama inavyoonekana pichani?”

Hata hivyo, kupitia ufuatiliaji wa kidijitali, imebainika kuwa picha hiyo si halisi, bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde . Kwa hiyo, taarifa zinazotokana na picha hiyo zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari, kwani zinaweza kupotosha umma.

Hivyo picha hiyo sio halisi na haioneshi uharibifu wa baadhi ya mabarabara barani afrika kama inavyo ripotiwa na baadhi ya kurasa za mitandao mbalimbali ikiwemo facebook, instgram, na twitter. Picha hiyo inasambazwa huku kukiwa na sintofaham za baadhi ya mataifa kutokuwa na barabara bora ili kuwezesha shuhuli za usafirishaji na maendeleo.

Nyenzo za utambuzi wa maudhui yaliyotengenezwa kwa akili unde zinabainisha kuwa picha hiyo ina viashiria vinavyoonesha uwezekano wa zaidi ya asilimia 90 ya kutengenezwa kwa AI.
​
screenshot-2026-04-21-085600-png.3576668
Hata kama siyo kweli ni AI lkn ndo uhalisia wa Barabara zetu nyingi za Tanzania hasa uku Bara....maana Hali za Barabara zetu zimekuwa mbaya sana.
Na zaidi zinachangia kukwamishwa Kwa maendeleo apa nchini hasa kule vijijini tunakotoka sisi Wananchi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom