PICHA: Hili jengo linalojengwa Kariakoo kwa PPP ni balaa ni zaidi ya Mlimani City unaambiwa Serikali itajizolea zaidi ya TZS 2.5bn kila mwaka

Hakuna bil 2.7 itapatilana kwa mwaka

Hizi ni hesabu zetu. Mm nimefurahi mwekezaji kupewa sababu pataendelezwa vizuri sana na sio suala la mapato kwa serikali. Rejea kilichotokea kwa mlimani city

Huyo.mwekezaji hatalipa pesa stahiki, ataweka malimbikizo na mwisho itaibuka kesi ambayo tutarudi kwenye mkataba ulivyosema(ambao kwa Sasa wewe huujui na Mimi siujui)
 
Wapi nimetaja nchi X?
 
Kwa uwekezaji wa pale ddc, serikali haiwezi kupata 2.5bil kwa mwaka. Mlimani city tu haipatikani hiyo pesa

Hakuna mwekezaji atatoa 2.5bil kwa mwaka, kwa mradi wa rooms 400. Pia haya maneno huwa mazuri sasa baadae wataanza ku-default na kesi juu

Mimi nilichopenda ni mwekezaji kuepewa patakua tofauti sana japo najua kwenye mapato serikali itapigwa kiini macho
 
Hatua nzuri, but eneo la ddc haliwezi kuwa kama mlimani city. Ni eneo dogo sana
 
Binafsi mwenyewe nimeshangaa,
2.5B kwa mwaka kwenye jengo moja tena hapo mpo kwenye PPP means kuna % kibao za mwekezaji kasepa nazo, hizo hesabu ni kubwa sana, sijui mwekezaji atarudishaje
 
Mkuu, idea yako ni nzuri ila inahitaji eneo jingine sio kkoo,
Tutengeneze soko la madini kwingine, pale kkoo ni soko la watu wa chini la vitu vya kawaida, pale watapanga wauza TV, Nguo, simu, kapeti na vitu vingine kama hivyo,

Kama tunataka international malls hebu tukaweke maeneo mengine haina haja ya kubadili kkoo nzima kisa international malls,

Mana ukifanya hivyo, mawinga wote na kina mwajuma wa mbagala wanaoenda kkoo wataacha kwenda, utakuta ushaibadilisha kkoo kabisa,
 
Dar es salaam imejaa sana kwa sababu watu wamejenga vibanda vya chinichini mji mzima. Sasa ni wakati wa kujenga juu.

Pia, kujenga kwenda juu kunapunguza safari ndefu, badala ya kwenda maduka kumi sehemu tofauti unapata kila kitu sehemu moja.
Lakini bado maeneo yapo sio lazima mjini kwani mji unatanuka kwa huduma
Kama kutakuwa na huduma zote lazima watu watakwenda tu

Hapa nilipo kuna masoko makubwa mbali na mji lakini watu wamejaa kila siku
Kuwa na soko la ghorofa 10 ina changamoto nyingi sana ila siwezi kubisha labda ndio wajenzi wameshauri hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…