PICHA: Hili jengo linalojengwa Kariakoo kwa PPP ni balaa ni zaidi ya Mlimani City unaambiwa Serikali itajizolea zaidi ya TZS 2.5bn kila mwaka

PICHA: Hili jengo linalojengwa Kariakoo kwa PPP ni balaa ni zaidi ya Mlimani City unaambiwa Serikali itajizolea zaidi ya TZS 2.5bn kila mwaka

Kafulila Siyo Mchumi mbobezi

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ni Mtu mkubwa sana kinchi ๐Ÿ˜€
Na CV kama hizi
Mafuru.jpeg
 
Mkuu, idea yako ni nzuri ila inahitaji eneo jingine sio kkoo,
Tutengeneze soko la madini kwingine, pale kkoo ni soko la watu wa chini la vitu vya kawaida, pale watapanga wauza TV, Nguo, simu, kapeti na vitu vingine kama hivyo,

Kama tunataka international malls hebu tukaweke maeneo mengine haina haja ya kubadili kkoo nzima kisa international malls,

Mana ukifanya hivyo, mawinga wote na kina mwajuma wa mbagala wanaoenda kkoo wataacha kwenda, utakuta ushaibadilisha kkoo kabisa,
Kwani haiwezekani floor moja kati ya hizo kumi ikawa soko la madini?

Yani umejikubalisha kabisa kuwa hatuwezi kuji organize?
 
Lakini bado maeneo yapo sio lazima mjini kwani mji unatanuka kwa huduma
Kama kutakuwa na huduma zote lazima watu watakwenda tu

Hapa nilipo kuna masoko makubwa mbali na mji lakini watu wamejaa kila siku
Kuwa na soko la ghorofa 10 ina changamoto nyingi sana ila siwezi kubisha labda ndio wajenzi wameshauri hivyo
Mkuu,

Katika miaka 10 ijayo idadi ya watu Dar ita double. Kwa sasa kuna umuhimu wa kujenga juu ama sivyo patakuwa hapakaliki hapo.
 
Kwani haiwezekani floor moja kati ya hizo kumi ikawa soko la madini?

Yani umejikubalisha kabisa kuwa hatuwezi kuji organize?
Sijasema hatuwezi kuji organize,

Nakukumbusha umuhimu wa kujiorganize kwa kuweka masoko ya madini sehemu yake na masoko ya vitu vya kawaida sehemu yake,

Nchi hii masoko ya madini yapo mengi tu, na yote yanafanya vema sana, na hakuna hata moja lililo changanywa na soko la vitu vya kawaida
 
Sijasema hatuwezi kuji organize,

Nakukumbusha umuhimu wa kujiorganize kwa kuweka masoko ya madini sehemu yake na masoko ya vitu vya kawaida sehemu yake,

Nchi hii masoko ya madini yapo mengi tu, na yote yanafanya vema sana, na hakuna hata moja lililo changanywa na soko la vitu vya kawaida
Again,

I am talking about what is possible, you are stuck on what is.
 
mim sikujua kamq ni PPP ila hilo jengo karibu nq klab ya simba nimewasifu kitu kimoja cha muhimu sana katika majenzi. wao wanatumia bomba badalq ya mirunda, mim najiuliza sana kkoo sasa hiv kila kona magorofa ila nashangaa hawatumii scafold issipokuwa mirunda/props. mim nadhan wasiwe wanatumia mirunda.na tupunguze kujengea tofal mpaka juu
 
Akili za kimasikini hizi UNAFKIRI hizo Trilioni zinafikaje kama sio kudunduliza? 2.5B kwa jengo moja ni lot of money ila I doubt serikali inapata hio hela kwenye jengo moja tu, unahitaji si Chini ya frame 400 zinazolipiwa around 2M kwa mwezi kugenerate hela hio kwenye PPP ya kariakoo.

Kikawaida kkoo Ghorofa binafsi hata 1B kwa mwaka hazifiki, la sivyo Maghorofa yasingeuzwa Bilioni 5.
Kuna mijitu inajiropokea tuh ,.
 
2.5bn kwa mwaka bado ni pesa dogo kwa Kariakoo naona kama tumepigwa sijui mzalendo Kafulila anasemaj

Huwezi ukafanya project hio kariakoo, Hasa katikati ya kariakoo, ili ufike hapo na Gari lazima uwaombe machinga si chini ya 20 watoe vitu vyao Barabarani ili upite, project gani ya kimataifa unafanya eneo hilo?

Na logic ya majengo ya NHC kkoo ni ya kizamani.

Unakuta Jengo halina basement, ground floor kuna frame 4 tu na juu wanaishi watu wanne, jengo katikati ya kkoo wapangaji 8 tu, juu nyumba wanalipa 200,000-350,000 kwa mwezi, chini Frame 800,000-1,200,000, just imagine chini ya milioni 10 kwa mwezi ghorofa zima katikati ya jiji.

Wawekezaji wanaopewa wanaanza kutoa frame basement, ground floor na 1st floor, kuanzia 2nd floor kuendelea unakuta hata ghorofa 10 ni stoo. So pato la NHC kwa sasa litaongezeka si chini ya Asilimia 100 na baada ya miaka 30 wakikabidhiwa jengo pato linaweza ongezeka hadi asilimia 1000 ama zaidi
Unahoja ya msingi sana wahusika wasome hii vizuri
 

Hatimaye PPP ya David Kafulila iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 103 ya mwaka 2010 ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2014, 2018 na 2023 imeanza kuzaa matunda chanya kwa Watanzania hasa baada ya kuanza kutumika kwa marekebisho mapya ya ya mwaka 2023 ya Sheria hiyo.

PPP kwa kumtumia mbia mzawa toka kampuni ya Tosh Logistics Limited wanajenga jengo kubwa huenda ikawa ni zaidi ya lile la Mlimani City kwa gharama ya TZS 36.7bn wakati matumizi yatagharimu kiasi cha TZS 13.3bn litakalokuwa na wapangaji zaidi ya 900 lenye ghorofa 10 kwenda juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-Centre Bw. David Kafulila ameiambia kamati ya Bunge ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuwa Dar es Salaam City Council's Economic and Development Corporation (DDC) katika wakati wote wa Ujenzi wa mradi huo kila mwaka watajizolea kiasi cha TZS 2 bilioni na baada ya mradi huo kukamilika watalipwa kiasi cha TZS 2.5 bilioni kama kodi ya jengo tu bila kuhesabu kodi za TRA pamoja na shuru zingine mbalimbali lakini kubwa zaidi baada ya muda wa mkataba kuisha jengo hilo litakuwa ni mali halali ya serikali ya Tanzania.

Mkurugenzi huyo ameiambia kamati hiyo ya Bunge kuwa Ujenzi wa mradi huo ni miongoni mwamiradi yenye mikataba bora zaidi ya uwekezaji na Ubia kuwahi kushuhudiwa hapa kwenye ardhi ya Tanzania.

Mkurugenzi huyo ameishukuru na kuipongeza kamati hiyo ya Bunge kwa kutembelea mradi huo wa Ubia huku akiomba ushirikiano zaidi kati ya TAMISEMI na PPP ili kwa pamoja waweze kuvuta mitaji toka sekta binafsi ili kujenga miradi yenye tija na thamani halisi ya fedha kwa manufaa ya Taifa kwani miradi hii itaipatia Serikali Kodi pamoja na tozo mbalimbali na hivyo kuchochea ukuaji wa Uchumi endelevu huku Serikali ikiachwa ifanye miradi ile tu ambayo haina sura ya kibiashara na hivyo kuipa nafuu zaidi Serikali katika kutafuta Mikopo na misaada mbalimbali toka kwa wahisani na mashirika mbalimbali nje na ndani ya nchi.
Uwaambie hizo fedha ni akiba ya watumishi.Wakistaafu au kuzihitaji ziwafikie mara moja.
 
Ivi wakati tunakomaa na ma physical investment ya majengo kariakoo tunaweka akilini mapinduzi ya TEHAMA kuwa mahitaji ya mafremu ya gharama kubwa yatapungua? Sihitaji display ya kwenye mafrem ya bei ghali. Nahitaji smartphone tu
 
Ivi wakati tunakomaa na ma physical investment ya majengo kariakoo tunaweka akilini mapinduzi ya TEHAMA kuwa mahitaji ya mafremu ya gharama kubwa yatapungua? Sihitaji display ya kwenye mafrem ya bei ghali. Nahitaji smartphone tu
Umeongea pointi sana mkuu,

Tehama itatufanya tusihitaji Majengo makubwa labda stoo tu
 
Back
Top Bottom