PICHA: Hili jengo linalojengwa Kariakoo kwa PPP ni balaa ni zaidi ya Mlimani City unaambiwa Serikali itajizolea zaidi ya TZS 2.5bn kila mwaka

Hatimaye PPP ya David Kafulila iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 103 ya mwaka 2010 ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2014, 2018 na 2023 imeanza kuzaa matunda chanya kwa Watanzania hasa baada ya kuanza kutumika kwa marekebisho mapya ya ya mwaka 2023 ya Sheria hiyo.

PPP kwa kumtumia mbia mzawa toka kampuni ya Tosh Logistics Limited wanajenga jengo kubwa huenda ikawa ni zaidi ya lile la Mlimani City kwa gharama ya TZS 36.7bn wakati matumizi yatagharimu kiasi cha TZS 13.3bn litakalokuwa na wapangaji zaidi ya 900 lenye ghorofa 10 kwenda juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-Centre Bw. David Kafulila ameiambia kamati ya Bunge ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuwa Dar es Salaam City Council's Economic and Development Corporation (DDC) katika wakati wote wa Ujenzi wa mradi huo kila mwaka watajizolea kiasi cha TZS 2 bilioni na baada ya mradi huo kukamilika watalipwa kiasi cha TZS 2.5 bilioni kama kodi ya jengo tu bila kuhesabu kodi za TRA pamoja na shuru zingine mbalimbali lakini kubwa zaidi baada ya muda wa mkataba kuisha jengo hilo litakuwa ni mali halali ya serikali ya Tanzania.

Mkurugenzi huyo ameiambia kamati hiyo ya Bunge kuwa Ujenzi wa mradi huo ni miongoni mwamiradi yenye mikataba bora zaidi ya uwekezaji na Ubia kuwahi kushuhudiwa hapa kwenye ardhi ya Tanzania.

Mkurugenzi huyo ameishukuru na kuipongeza kamati hiyo ya Bunge kwa kutembelea mradi huo wa Ubia huku akiomba ushirikiano zaidi kati ya TAMISEMI na PPP ili kwa pamoja waweze kuvuta mitaji toka sekta binafsi ili kujenga miradi yenye tija na thamani halisi ya fedha kwa manufaa ya Taifa kwani miradi hii itaipatia Serikali Kodi pamoja na tozo mbalimbali na hivyo kuchochea ukuaji wa Uchumi endelevu huku Serikali ikiachwa ifanye miradi ile tu ambayo haina sura ya kibiashara na hivyo kuipa nafuu zaidi Serikali katika kutafuta Mikopo na misaada mbalimbali toka kwa wahisani na mashirika mbalimbali nje na ndani ya nchi.
2 bilion..naona aibu
 
Naona watu wamekurupuka kuchangia uzi kwa mihemko bila kuelewa kilichoandikwa. Mmeambiwa mradi ni wa serikali na mbia. Wakati ujenzi ukiendelea serikali itakuwa ikijipatia 2b kwa mwaka na baada ya mradi kukamilika serikali itajipatia 2.5b kama kodi ya jengo (kumbuka m'bia naye ana mgao wake nje ya hizo 2.5b) na bado hapo serikali itakusanya kodi na shuru nyingine kutoka kwenye uwekezaji huo. Kwa namna wakurupukaji wanavyochangia ni kama walitaka serikali ikusanye kilakitu na mbia asipate chochote kitu ambacho hakiwezekani. Nilidhani tungempongeza kwanza Kafulila kabla ya kucomment kwa chuki na mihemko.
Kabla ya kutulaumu unaonaje nyie mliobarikiwa wenye uelewa mkubwa wa jambo hili mkaja na justification ya hizo 2B na 2.5B? Huyo mbia yeye ataingiza kiasi gani?
Yaaani siku hizi watu kuhoji ni chuki na mihemko?
Mnaficha Nini?
 
Mkuu labda nikusaidie kidogo,

Mbali na hizi 2bn au 2.5bn still jengo baada ya Mkataba litakuwa Mali yetu/Serikali,

So hivyo angalia pia hi 59bn ya ujenzi
 
Ukiwaondoa hao wafanyabiashara wadogo na Soko nalo linakufa vile vile.

Swali moja kwako, kwanini uwapokonye wafanyabiashara wadogo kariakoo wakati kuna maeneo yaliyotengwa ya biashara ya kimataifa yenye ukubwa zaidi ya mara 10 ya kariakoo? Eneo kote kuanzia Mjini na barabara ya salender kwenda hadi mwenge kuna Eneo kuubwa lenye maelfu ya Biashara za kimataifa.
Nia aibu serikali kushobokea Kariakoo soko kongwe badala ya kwenda kufungua masoko mapya kwa upande mwengine.
 
PPP ni akina nani? Unakuta ni Wanu na Abdul, mnasema ni PPP😳
Kwani we mgeni hapa nchini? Humo Kariakoo kuna magorofa mengi ya viongozi wa Mbogamboga party wakiwemo wastaafu. Haya ya PPP ni miradi ya viongozi hao hao. Mtu anayeweza kulamba mgao wa more than 100B kwenye dili la kifisadi anashindwaje kujenga ghorofa la 50B?
 
Kama unatumia standard za Nje unakosea, hilo jengo lipo Tanzania, watakaokodi ni Watanzania, kama sio Watanzania waliokodi watauzia Watanzania, kivyovyote Rent zita reflect soko la Kariakoo, ukiweka Rent za Dubai ama London watu wata rent majengo mengine badala ya hilo.

Rent za kariakoo on average ni milioni 2 kwa frame za nje kama ni kubwa sana inafika 3-5M, frame za ndani laki 7 hadi 1.2M, unahitaji maelfu ya frame kugenerate 2.5B kwa mwezi, hakuna jengo la frame 2000 hapo.
Nadhani frame zitapishana ki maeneo kama ilivyo Mlimano City.
Labda tutumie kipimo cha square meter mmoja itapangishwa sh ngapi?
Na hata square meter mmoja bei yaweza kuwa tofauti kulinganisha na ni ghorofa ya ngapi n.k
 
Mkuu labda nikusaidie kidogo,

Mbali na hizi 2bn au 2.5bn still jengo baada ya Mkataba litakuwa Mali yetu/Serikali,

So hivyo angalia pia hi 59bn ya ujenzi
Ungelete mkataba humu ungekuwa umetusaidia sana!
Words come so easy and often intentionally jumbled.
 
Hii model ni kama nchi inaenda kutoboa hivi pipi shilingi ngapi maeneo ya kwenu!?
images (3).jpeg
 
Nadhani frame zitapishana ki maeneo kama ilivyo Mlimano City.
Labda tutumie kipimo cha square meter mmoja itapangishwa sh ngapi?
Na hata square meter mmoja bei yaweza kuwa tofauti kulinganisha na ni ghorofa ya ngapi n.k
Hakuna mambo ya Sqm kkoo, na bei zinatofautiana ndio ila huko ambapo frame ya nje haifiki 2M ujue hakuna issue na biashara imedoda.
 
Hatimaye PPP ya David Kafulila iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 103 ya mwaka 2010 ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2014, 2018 na 2023 imeanza kuzaa matunda chanya kwa Watanzania hasa baada ya kuanza kutumika kwa marekebisho mapya ya ya mwaka 2023 ya Sheria hiyo.

PPP kwa kumtumia mbia mzawa toka kampuni ya Tosh Logistics Limited wanajenga jengo kubwa huenda ikawa ni zaidi ya lile la Mlimani City kwa gharama ya TZS 36.7bn wakati matumizi yatagharimu kiasi cha TZS 13.3bn litakalokuwa na wapangaji zaidi ya 900 lenye ghorofa 10 kwenda juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-Centre Bw. David Kafulila ameiambia kamati ya Bunge ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuwa Dar es Salaam City Council's Economic and Development Corporation (DDC) katika wakati wote wa Ujenzi wa mradi huo kila mwaka watajizolea kiasi cha TZS 2 bilioni na baada ya mradi huo kukamilika watalipwa kiasi cha TZS 2.5 bilioni kama kodi ya jengo tu bila kuhesabu kodi za TRA pamoja na shuru zingine mbalimbali lakini kubwa zaidi baada ya muda wa mkataba kuisha jengo hilo litakuwa ni mali halali ya serikali ya Tanzania.

Mkurugenzi huyo ameiambia kamati hiyo ya Bunge kuwa Ujenzi wa mradi huo ni miongoni mwamiradi yenye mikataba bora zaidi ya uwekezaji na Ubia kuwahi kushuhudiwa hapa kwenye ardhi ya Tanzania.

Mkurugenzi huyo ameishukuru na kuipongeza kamati hiyo ya Bunge kwa kutembelea mradi huo wa Ubia huku akiomba ushirikiano zaidi kati ya TAMISEMI na PPP ili kwa pamoja waweze kuvuta mitaji toka sekta binafsi ili kujenga miradi yenye tija na thamani halisi ya fedha kwa manufaa ya Taifa kwani miradi hii itaipatia Serikali Kodi pamoja na tozo mbalimbali na hivyo kuchochea ukuaji wa Uchumi endelevu huku Serikali ikiachwa ifanye miradi ile tu ambayo haina sura ya kibiashara na hivyo kuipa nafuu zaidi Serikali katika kutafuta Mikopo na misaada mbalimbali toka kwa wahisani na mashirika mbalimbali nje na ndani ya nchi.
Huyu Kafulila level yake ni Uwaziri hakika Rais amepata mtu sahihi pale PPP
 
Back
Top Bottom