Picha hizi ni funzo kwetu

Picha hizi ni funzo kwetu

Hivi baada ya kuswaliwa na Masheikh Wakuu ama Maaskofu Wakuu kama ilivyotokea Kwa JPM ama Lowasa ndiyo inakuwa umefutiwa dhambi na Mola wako?

Muhimu kumcha Mola na kuacha kutenda dhambi ukiwa bado hujalala mauti.

Kifo kipo kwaajili ya kutukumbusha hilo
Matendo yako ndiyo yatayoamua pakubwa hatima yako akhera
 
Elimu kwanza Madrasa za nini?
Madarasa inatokana na madrasa,ni pahala panapotoa elimu ya mahusiano baina ya mja na mola wake,namna gani Aishi na binaadam wenzie,unyenyekevu na utu wa mwinyi unatoka madrasa
 
Upo sahihi Mkuu, japo mtoa mada alitaka kupindisha maana
Ila Dua za kukuombea maghfira zinasaidia pia,rejea surat tawba '...umuombee Dua au usimuombee Dua, hata ukimuombea Dua Mara 70,mwenyezi Mungu hatomsamehe,hakika yeye alimkataa mwenyezi Mungu na mtume wake..' sikumbuki Aya ipo kwa wingi au umoja,lakini hapo ni dhahiri kwamba ikiwa mzikwaji alikua mtenda mema na muumini basi kumuombea Dua Kunamsaidia
 
Daah ila watu yaani mnatumia msiba kama fimbo za kuwatishia wengine. Kufa kupo tu karne na karne hakuna funzo hapo mkuu
Ata kama una watoto 18 elfu.... kama Wewe uliishi maisha ya dhuruma na dhambi ata hao watoto wakikesha Kukuswalia ni kazi bure😭Mungu ana mpa Pepo yule anaishi kama alivyo elekeza na anavyotaka Yeye.Tusitishane Swali kabla ujaswaliwa
 
Madarasa inatokana na madrasa,ni pahala panapotoa elimu ya mahusiano baina ya mja na mola wake,namna gani Aishi na binaadam wenzie,unyenyekevu na utu wa mwinyi unatoka madrasa
Madrasa ni sehemu ya kwenda kuwakaririsha Watu na kuwafunza kuwa kumuabudu Mungu ni lazima uongee Kiarabu.

Mungu atuumbe sisi Waafrika halafu tumuabudu Kiarabu Mungu sio Racist.

Au Mungu ni Mwarabu?
 
Back
Top Bottom