Picha: Inawezekana kujenga nyumba kwa Design hii kwa milioni 16?

Sasa nikichukua hiyo nafasi ya kibarua ambaye analipwa elfu 10 kwa siku ndio nitakuwa nimeokoa nini?
Tu-assume ujenzi utaenda mfululizo kwa siku saba so tufanye 10,000×7=70,000/= ukiongeza hapo 5,000/= una cement mifuko mitano kama unapandisha tofali hiyo mifuko inapiga karibia mizunguko minne hapo hujaokoa kitu?

Wabongo tunakwama tunapoanza kudharau hela ndogo,ujenzi hauna hela ndogo.
 
Mafundi wa kibongo wowote wengi wao ni full ujanja ujanja tu na maneno meengii utadhani waga sio professional

Kwani mkiwa mna design ramani waga kuna sehemu mnaigilizia? Si unauliza mtu anataka nyumba yake iweje na wewe fundi/architecture una design kulingana na mahitaji ya mteja

Sasa jamaa karahisisha kabisa Kwa kuleta picha, it's okay, hakuna anaejua dimension za vyumba,dining nk ila umeona picha ya mwonekano wa nje hiyo ndo kazi yako sasa

Hapo ndio sehemu ya kujitofautisha wewe fundi/architecture na mteja, sasa fundi unaanza ohhh unajua hapo hatujui ndani pakoje, ohhh unajua hapo chini ukiweka beam gharama itakuwa kubwa

Ohhh ohhh nyingi WTF, kaa chini toa kitu kuhusu Mambo ya gharama ashindwe mwenyewe muhusika, kama unabuni ramani kutoka kichwani sasa unashindwa nini kubuni ramani kutoka kwenye picha?
 
Makadirio ni kwa kuangalia ramani ya nyumba nzima na vipimo sio picha ya upande mmoja
La sivyo kwa pesa hiyo inaweza tosha kama utatumia mchanga tu na cement kujengea
We unahisi inawezekana kutumia mchanga na cement kujenga?
 
Kwani hiyo picha hadi imekaa hivyo si imetokana na ramani
Mkuu,
Kwenye hiyo picha unaweza kujibu yafuatayo;
... vyumba vingapi?
...vyoo vingapi?
...sitting/dunning ipo?
...size ya vyumba, sebule, jiko na vyoo?
...kuna corridors au niaje?

Kama huna hayo majibu, as huna dimensions. Unawezaje kuuliza kama 16m inatosha au vipi.
 
Professional hawezi kujibu maswali kirahisi tu namna hiyo mkuu. Ukileta picha, omba mtu adizain kulingana na picha then upate makadirio. Huwezi kupewa makadirio kirahisi tu namna hiyo. Dr hawezi kufanya diagnois kwa kukuangalia tu usoni, msirahisishe fani za watu namna hiyo.
 
Naona unapepelea sana, Hadi nahisi huenda wew ndiye mnufaika wa hiyo project. Samahani!
Labda tukuambie hivi, hiyo ni ghorofa, Si kila fundi atakujengea. Process zake ni ndefu pia
Hiyo sio Gorofa ni kigorofa, so hizo process ndefu unazosemea sijui ni zipi! Nondo na kokoto sio
 
Kwa foundation ipi? Mil 16 hata hiyo roof huwezi kujenga aisee
 
Mailioni hizo ulizotaja iwe kama tunavyoiona hapo kwenye picha au ifike katika levo gani ya ujenzi?
 
Vyumba viwili, ukubwa miguu 15 Kila upande

Sitting room na dinning ipo ukubwa wake wa kawaida tu

Kila chumba kiwe na choo then choo Cha public hakuna
 
Okay, Dr anaweza kuhisi unaumwa nini kutokana na maelezo yako pasipo ata kukupima Damu

Actually sitaki kusema kuwa narahisisha bali nasema kuwa nyie mnafanya Mambo yawe mengi sana

Wewe kama ni fundi au mchora ramani huwezi kupata shida kiasi hicho unless otherwise uwe huna uzoefu kabisa

Kama ni mzoefu basi utajua kabisa vyumba katika nyumba za kisasa let's say waga vina ukubwa wa 12*16, dining 20*25,Choo cha ndani 2*3, kitchen 8*8 and so on

Sasa hapo unashindwa kumpa simple analysis kulingana na uzoefu wako na pia jicho la kiufundi baada ya kuangalia mfano wa picha na kusikiliza matakwa yake? Kwanini usimpe mtu roughly sketch ata 3 ambazo yeye atachagua?

Na ndomana mara nyingi wateja waga wanapenda kutumia mafundi wa kawaida Kwa sababu waga wako straight na sio architecture au engineers Kwa sababu always Wana complicate Mambo
 
Huu Ushauri wako unamfaa jobless, na sijui ni jobless gani huyo anaweza akajenga nyumba hata ya room mmoja ikiwa yeye ni jobless

Yani niache kazi inayoniingizia Pesa ambayo inanifanya nijenge then nikawe saidia fundi!? Hii ni akili ya wapi?

Sio kwamba nadharau hela ndogo hapana lakini kama kuna chance ya kupata hela kubwa ya nini kujitesa na pesa ndogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…