Picha: Inawezekana kujenga nyumba kwa Design hii kwa milioni 16?

I wonder!
 
Kona kona nyingi sana, inashangaza kwakweli na kusikitisha
 
Kwa picha tu Ni vigumu sana kufanya tathimini. Scale na Vipimo Ni muhimu sana, idadi ya vyumba pia; na materials gani. Vinginevyo ni ramli tu na watakudanganya.
 
Hiyo bei sahau mkuu.
 
Kwa picha tu Ni vigumu sana kufanya tathimini. Scale na Vipimo Ni muhimu sana, idadi ya vyumba pia; na materials gani. Vinginevyo ni ramli tu na watakudanganya.
Idadi ya vyumba si umeshaambiwa!
 
Naona watu wameshindwa kumuuliza muhusika swali la msingi kwamba hilo jengo anajengea wapi?

Ujenzi wa mji kama wa Dar huwezi kuufananisha na wa Mbeya,gharama zinazidiana mkoa kwa mkoa.
Kabla ya hayo ..kikubwa ramani ya mjengo ....
 
Hiyo ya kuwa Scammers ni wao, sisi tunachotaka kujua ni kwamba inawezekana au haiwezekani?

Kama inawezekana unadhani nitawaacha mafundi wote hapa Tz nikamtafute mnigeria wa kazi gani?
Kifupi 16m haitoshi japo hujatoa dimensions.
Ungetoa ramani ingewasaidia wataalamu kufanya makadirio.
 
Kona kona nyingi sana, inashangaza kwakweli na kusikitisha
Ndio walivo hawa wasomi wetu, yani we ukitaka kufeli Jambo lako at the beginning kabisa mshirikishe mtu mwenye professional yake

Let's say unataka kufungua biashara, Mwambie Afisa biashara aje akushauri aina ya biashara kulingana na Eneo lako,ndo basi tena we kiuno Feni hiyo biashara imefia hapo

Unataka kujenga ita engineer akupe ushauri wa kitaalamu,uchunguzi,Tathmini,majaribio nk, ujue ndo anakuja kuzika kabisaaa ndoto zako

Yani kibongo bongo the vice versa is False, professional ndio wana behave like layman na layman ndio wana behave like professional
 
Idadi ya vyumba si umeshaambiwa!
Dimensions..Idadi sio issue.. issue vipimo, upana na urefu wa ukuta pamoja na msingi, milango, madirisha ...nyumba inaweza kuwa vyumba 3 ila Kwa mwingine vyote hivyo ni kimoja...vipimo
 
Kwani hiyo picha hadi imekaa hivyo si imetokana na ramani
Mkuu Ni kweli imetokana na ramani. Kwa hiyo leta na hiyo ramani pamoja na hiyo picha yako watu waifanyie kazi.
Ramani ina migawanyo ya vyumba na vipimo.
 
Kona kona nyingi sana, inashangaza kwakweli na kusikitisha

Mkuu hapo tusiwalaumu hawa architects wetu kwa kutokujibu unavyohitaji, kwa nijuavyo mimi hapo fundi akikupa makadirio atakuwa anakudanganya maana makadirio huwa yanatokana kwa vipimo unless just unataka makadirio yasiyo ya kitaalam.

Ila kama makadirio ya huyo mnigeria ni 16M ikiwa na garage,kwa kuwa room itakuwa na mahitaji ya material zaidi ya hapo garage tegemea zaidi ya 16M.
 
16 haitoshi. By the way unajenga wapi
 
Dimensions..Idadi sio issue.. issue vipimo, upana na urefu wa ukuta pamoja na msingi, milango, madirisha ...nyumba inaweza kuwa vyumba 3 ila Kwa mwingine vyote hivyo ni kimoja...vipimo
Wewe kama mtaalamu ukipiga Calculations zako kwa Design hiyo na kiasi hicho cha pesa tutatoa vyumba vya ukubwa gani? Wacha pesa ituamulie ukubwa wa nyumba lakini materials yabaki kuwa standard
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…