Picha: Inawezekana kujenga nyumba kwa Design hii kwa milioni 16?

Okay, so hapo budget yake ni ngapi kwa makadirio yako hadi nyumba isimame kama hivyo
Makadirio yangu, kwa reasonable house ya 80m² itakuwa 30,000,000±
 
Hapo fundi unampa lawama hasizo stahili. Kwenye ujenzi kuna taaluma nyingi zinafanya kazi kwa pamoja. Kuna Wasanifu (Architect), Wakadiliaji (Quantity Surveyor), wahandisi (Engineers) wa ujenzi, umeme, mifumo ya maji, mifumo ya air-conditioning na mifumo ya mawasiliano then ndipo wanafuata mafundi.
Fundi kumbebesha mzigo wa kukadilia ni kumuonea tu. Watu wengi wanaojenga ukwepa kutumia wataalam wa ujenzi na kumbebesha fundi mzigo wote wakidhani wanapunguza ghalama. Kimsingi hawapunguzi bali wameongeza ghalama bila kujua kwani matokeo yake ni kujenga nyumba substandard kwa ghalama kubwa.
 
Nyumba imenivutia design yake. Ila kwa 16M hufiki popote mkuu
 
Sio mkoa kwa mkoa tu hata hapa dsm unatofautiana sana, ujenzi wa kivule na goba ni tofauti
 
Mpaka miaka ya leo kuna mabata bado mnapigwa deal na hizo mbuzi za Kinaigeria?
 
Ina maana arch wa hapa home ni vilaza sana hawawezi kufanya reverse engineering na kupata ndani kupoje?
Kama hawawezi basi si wakisie(trial and error) waunde model tofauti za vyumba ili kipata minimum cost modal.
Nadhani wataalamu haoa wanaweza kabisa kupata namna vyumba vinaweza kijipanga na kupata uhalisia wa gharama.
 
Dunia inaenda kwa kasi huu upauaji kwenye picha ndio upauaji utakaokuja kutrend mbeleni hapo, muda si muda watu wataachana na contemporary
 
Hii uliyoweka ni ramani au picha?!
 
Ngoja jumba bovu liwaangukie Mnigeria ana lake jambo.
Kwani Mnigeria kasema anajenga nyumba TANZANIA ????
Bei yenyewe kataja kwa naira, sio hata dollar, walengwa wake ni Wanaigeria, sasa utapigwaje na huyo mtu ? Mi nilidhani discussion ni je, kweli inawezekana kwa hapa Tanzania ukiachana ha huyo Mnigeria?

Kwa mimi hicho kijumba ni kibovu ajabu. Mbele kuna ki craw space, yani unaingia kwa kutambaa, gari haiingii wala mtu hasimami wima, cha nini ? Na ardhi ni tambarare, sasa amepandisha level upande mmoja na kuweka craw space ili iweje ???

Na ki ngazi cha mbele kinapiga kona bila sababu, chembamba kama kinjia cha kuku wakati nafasi ipo kama ngazi zisingepiga kona...

Dirisha la vioo kuanzia darini mpaka sakafuni, well, kama unajenga kijumba cha kichumi kama hicho ina maana hela huna, walinzi huna, ukuta huna na umekijenga high density, high crime area, Kizuiani Mbagala, panya road wanaingia kwa kupiga kofi dirisha. The design is atrocious.


 
Mimi naomba kujua kama 1.5 storey kama hii inahutaji design approval kama mgorofa? Yaani architects, structural, umeme, maji na bango? Au ni kawaida tu kama tunavyofanya mijengo ya kawaida?
 
Ndani jamaa kagoma kuonesha isipokuwa kwa wale ambao wapo tayari kufanya nae kazi
Hiyo ramani sio yake, picha hiyo katoa mtandaoni, nimeshaiona. Hilo jengo linafaa kwenye slope kidogo. Pia naamini kuna ramani nzuri zaidi ya higo. cha msingi hapo eneo lako likoje. Unachukua ramani hakikisha iendane na site, km hilo umezingatia sawa. kurekebisha garage kuwa chumba hapo hakitakaa sawa mana urefu mdogo, katakuwa kama kaandaki.
 
Mimi naomba kujua kama 1.5 storey kama hii inahutaji design approval kama mgorofa? Yaani architects, structural, umeme, maji na bango? Au ni kawaida tu kama tunavyofanya mijengo ya kawaida?
Hilo gorofa kaka. kuna mtu alipigwa X kibalaza tu cha nche mbele baada ya kujiongeza akataka aweke ngazi na sehemu ya kupumzikia juu. Akakuta X hakuna kuendelea juu
 
Ndoto za Alinacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…