Picha: Jinsi tapeli la Kinigeria lilivyojaribu kunitapeli mtoto wa Magomeni Mikumi leo asubuhi

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wana JF wenzangu, natumai kila mtu yuko vizuri.

Ebu fikiria mtu nimekulia maskani, dili zote za haram na halali nazijua, maana nyingi huwa zinapangwa katika maskani mbalimbali halafu ndo zinaenda kuchezwa halafu anakuja kijana from Lagos mashambani huko anataka kunitapeli mimi mbongo tena mchana kweupe, tena katika nchi ambayo kila mtu anatakiwa kuwa mafia ili maisha yaende.

Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi. Namuonea huruma sana kijana, hapa najiuliza sijui nimtapeli yeye ili liwe funzo kwa wengine!

Angalia code namba yake na code namba za hizo picha mbili nilizotuma chini.

Picha ya chini kabisa jamaa amehamaki na kujaribu kujitetea kinafiki ila nikampuuza na ku block yeye mwenyewe πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

 
Kumbe wewe ndo mara ya kwanza kukutana na hao jamaa baba?

Yani mpaka umeyaleta jf unajiona kama umeachieve kitu kikubwa sana[emoji3]
Nimeleta hapa kwa lengo la kutaka watu wawe macho na matapeli wa aina hii. Kumbuka sio wote ambao washawahi kukumbana na matapeli hawa. Na pia ni lazima kuna watu tena watanzania wenzetu maskini washalizwa na matapeli haya kwa sababu ya kutokosa kujua mambo haya.

Sasa kuleta hapa habari za aina hii tena nikiambatinisha na namba kutawasaidia na wengine kuwa macho zaidi na hawa wahuni.
 
Kumbe wewe ndo mara ya kwanza kukutana na hao jamaa baba?

Yani mpaka umeyaleta jf unajiona kama umeachieve kitu kikubwa sana[emoji3]

Kwa hiyo wewe code number ya nigeria huijui? Basi ata ya marekani 😳,ulikuwa huna haja ya ku google 🀣
Kwa hiyo kama nyie mnajua mmeona mleta mada ni mjinga kuleta stor yake hapa

Common sense
 
Wasap inaweza kutumika mahali popote Pia ujue. Mnajiria akienda USa anaweza Tumia namba yake ile ile.ujue hilo piah
 
Kwenye suala la utapeli wa kimataifa wenzetu wapo mbali sana....
Nigerian people are very far far faraway......πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚
Pole na hongera.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…