Picha: Jumapili ya Leo nikiwa kwenye Ibada

Kujenga chumba kimoja cha mgongo mmoja sh ngapi?
Chumba Cha ukubwa gani mkuu? Kama ni Chumba Cha wastani Naweza kukujengea Kwa 280k tu.
Inaweza kupanda kutegemeana na mambo mengi.
Hiyo nimekupa makadilio ya chini kabisa
 
Kwa hapa Niko mwenyewe (kazi ya Leo ni ndogo ndiyo maana Niko mimi na kibarua wangu)
Kazi ikiwa kubwa Nina mafundi wenzangu Huwa nashirikiana nao.
Karibu
Dah! Kweli maisha ni safari ndefu! Nikikumbuka enzi zile umetoka Kigoma na treni ya reli ya kati, ulipokuja kutafuta kibarua chochote kile jijini Darisalama!

Na hatimaye leo umekuwa ni fundi mkubwa mwenye wasaidizi! Unafanya kazi Mkoa wowote ule!! Hakika utukufu na sifa apewe Mwenyezi Mungu kwa kumlea vizuri kijana wetu aise. 🙏
 
Kuna mengi nimepitia mpaka hapa nilipo mkuu, unaweza kukubali kwamba nilitembea na miguu kutoka mwanza mpaka kigoma?
Basi taarifa ndiyo hiyo, nimewahi kutoka mwanza (Tena ni Bariadi mpaka Kigoma Kwa miguu)

Hilo ni Moja kati ya mengi nimepitia ambayo ni ngumu kumeza lakini ndiyo nimepitia mimi
 
Ulipumzika wap na wap na ulikula nini JE kwa wastani ulitembea kufwata lamii au ulitumia usafiri wa asilii.
 
Nilipumzika maeneo mengi mkuu, nikiwa njiani watu niliokuwa nawaambia naenda kigoma walikuwa wanasema labda nimevuta bangi 🤣🤣
kwamba nitafia njiani tu sifiki popote.
Kuna kipande nilitembea siku nzima sioni nyumba mpaka jua likazama.
Ilikuwa ni kipindi kigumu Sana wakati ule.
Nilijaribu kwenda kuomba msaada Kwa watu wa dini, lakini niliishia kupew majibu yasiyo mazuri.
Wapo waliosema mimi ni kibaka/chokoraa kwahiyo nitawaibia au nimeenda pale kusoma ramani ya wizi.
Kuna sehemu niliitiwa mpaka sungusungu nikachezea kichapo huku naambiwa nitaje makundi ya wezi ambao wamenituma.
Nikipigwa Sana mpaka kesho yake sikuweza kuendelea na safari Tena.
Nilienda mbele kama kilomita 5 hivi ilikuwa ni mashmbani nikakaa huko kama wiki hivi nauguza majeraha yangu.

Ni mengi Sana nilipitia mpaka muda mwingine Huwa nakaa peke yangu naanza kucheka japo SI mambo ya kuchekesha
 
Pole sana kaka kwa hayo mapito hope umekua mtu Bora sana sana
 
Ulipumzika wap na wap na ulikula nini JE kwa wastani ulitembea kufwata lamii au ulitumia usafiri wa asilii.
Kuna kipindi niliwahi kwenda mbali huko kutafuta uchawi ila kwakuwa nilikuwa mdogo watu wa kule wakaishia kunitishia tu lakini sikufanikiwa.
Nimewahi kwenda msumbiji Kwa miguu pia via kilwa road mpaka ndani kule msumbiji nikarudishwa bongo na watu wa kule kidogo wanichome moto wakisema mimi ni gaidi (Kuna kundi moja la waasi liko kule maarufu Sana wakawa wanasema mimi ni .mmoja wao.

Nilikaa ofisi ya Kijiji na Wana Kijiji wote wa pale walikuja kuniangalia 🤣🤣 yaani ilikuwa kama muvi vile yaani Kijiji chote wamekuja kuniangalia mimi kwamba ni gaidi hatari Sana, ila wakiangalia umri wangu hayo mawazo ni kama yanakosa nguvu.
Basi baada ya kukaa pale Kwa siku kadhaa Wana Kijiji wanashauriana juu yangu ikabidi Kuna wasamalia wema wakanitolosha usiku wa manane.
Njia waliyoniambia nipitie ni porini (bila shaka ni hifadhi ya wanyama ile, maana nilikuwa sitembei zaidi ya lisaa bila kukutana na Hawa swala)
Basi niliambiwa Kuna sehemu nikifika Kuna mto, nikivuka huo mto Niko Tanzania.
Nimefika pale mtoni Sina hata mia ya kuvuka pale, Kuna jamaa alikuwa pale anavusha watu akasema kama Sina hela basi anachagua chochote kwenye kibegi changu chenye thamani halafu ndiyo anivushe.
Nilikuwa na shati mbili Kali Sana na suruali Moja yule mbwa akazichukua.
Kabla nilijaribu kuangalia kama naweza kuvuka Kwa kuogelea, nikaelekea Kwa mbele kidogo kuangalia kama Kuna sehemu naweza kuvuka, nikaona mamba wanaota lile jua la asubuhi, ikabidi niwe mpole
 
Kuna mengi nimepitia mpaka hapa nilipo mkuu, unaweza kukubali kwamba nilitembea na miguu kutoka mwanza mpaka kigoma?
Basi taarifa ndiyo hiyo, nimewahi kutoka mwanza (Tena ni Bariadi mpaka Kigoma Kwa miguu)

Hilo ni Moja kati ya mengi nimepitia ambayo ni ngumu kumeza lakini ndiyo nimepitia mimi
💪
 
Back
Top Bottom