Elections 2010 Picha: Kikwete Tanga, Bumbuli, Kilindi, Kilimanjaro, Arusha

Mi siamini katika huo uzushi wa eti kuna majini, uchawi etc...Ndio maana hata BBC walisema kwenye kura zao za maoni kuwa sisi waTz tunaongoza Afrika kwa kuamini mambo ya nguvu za giza.

Naamini kuwa kila mtu ana haki sawa ya kuomba kuongoza wanachi wenzake, sijali kama huyo ni mganga au profesa ama ni mlalahoi mradi tu apewe nafasi ajieleze kwa wanachi wakimkubali basi ni haki yake kwenda bungeni.

Maswala haya ya waganga na kuwaendekeza ndio tatizo letu. Awe ni huyu au kumpa nafasi sheikh Yahya kuongea utumbo kwenye national Tv hiyo ni wadhi kuwa sisi wa Tz tuna walakini kama jamii, tuinue kioo na kujiangalia kwa kweli...
 
Huwa namkubali kwa baadhi ya mambo Sheikh Prof Lipumba


 


Unataka kuniambia kwamba waliomchagua hawana akili?
 
Nawaomba wahudumu wa bunge wampange Maji marefu (kama akishinda) kiti kando ya Mama Rwakatare (kama akiteuliwa)...
 
Jk amnadi Prof Maji Marefu Korogwe leo


(Picha toka MICHUZI)





Jk anamnadi jamaa kwa mbali akiwa nje ya gari la muheshimiwa!
Huyu jamaa amemwamgusha msomi Dr E Mdolwa na anaaminika kuwa kigagula wa kutupwa.
JK amefanya vema kumweka kwa mbali maana huwezi jua si ajabu pengine Sheikh Yahya hafui dafu hapo!!
 
Post imerudiwa hii.
Mods iunganishe na illleeeee nyingine
 
Kinachoangaliwa zaidi ni matokeo-sasa hivi haendelei tena kuanguka jukwaani :becky:
 
Mi sidhani kachaguliwa kwa sababu ya uganga wake. Nilikuwepo Korogwe muda mfupi uliopita Steven Ngonyani ndio mgombea anayekubalika kwa wananchi wa jimbo lake kuliko mgombea yeyote. Labda uniambie kuna mengine nisiyoyajua.

He's a great intellectual. Vote CCM
 
Kinachoangaliwa zaidi ni matokeo-sasa hivi haendelei tena kuanguka jukwaani :becky:

Si usha sikia kuwa Sheikh Yahya amepeleka majeshi kumuongezea ulinzi, halafu ukichanganya na Prof. MM haanguki mtu tena!!!
 

Hivi mgombea mwenza wa Dr Slaa anaitwa nani? nijuze japo cv yake.
 
Ngoja tuone kama wananchi wataamua nini siku ya kupiga kura,nimeshangaa kmuona JK akimnadi wakati Maji Marefu yupo kwa nje,sijui ndio masharti ya uganga?
 

CCM ni kumbakumba, wachawi nao humohumo. Ntawashangaa sana wana Korogwe ikiwa watampigia kura Mchawi MAji MArefu kuwa Mbunge wao zama hizi za Sayansi na Teknolojia, kweli kabisa. CCM kimekuwa chama cha Wachai sasa- Sheikh Yahya, Maji MArefu, hatari kubwa!
 
Nasikia siku hizi ameacha uganga ni tajiri wa kutupwa huko Korogwe....

Ingekuwa kweli hilo jina la Taaluma- Maji marefu lisingetumika. Hivi unamjua Ibilisi vizuri weye? Akupe utajiri halafu umuasi! Hawezi kufanya hilo kosa, kama hajakuua basi ataudai utajiri wake na uanze upya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…