Elections 2010 Picha: Kikwete Tanga, Bumbuli, Kilindi, Kilimanjaro, Arusha

Elections 2010 Picha: Kikwete Tanga, Bumbuli, Kilindi, Kilimanjaro, Arusha

comoro-jk-2603.jpg


Hapa anavunja Katiba hizi ni kazi za Dr Shein!

ha ha ha kweli kabisa, hii kazi ya mikasi ni ya Dr Shein
 
Hahahaaa, nimegundua. Kumbe ulikuwa unamaandisha hii PETE siyo? Daaa, watu mna macho kweeeli.

kikwete+pemba.jpg
 
ha ha ha aiseee

Ila mods waingilie kati na kupunguza size ya hizi picha kama inawezekana (maana nina wasiwasi mr madrassa al sul hajui hata kupunguza size ya picha).

Hivi suala la ukubwa wa picha na maendeleo yetu na taifa letu vinahusiana nini?
 
Hivi suala la ukubwa wa picha na maendeleo yetu na taifa letu vinahusiana nini?

kama hiyo madrassa yako ya Temeke hawakukuambia hili, ukiweka mipicha mikubwa kama hii yako, inafanya watumiaji wengine ambao connection zao sio fast kushindwa kufungua thread yako. Bila wewe kujua, unaua lengo lako la kuweka picha in the first place.
 
Pete yenyewe ni hii au nyingine?

kikwete-msanii.jpg
Sheikh-Yahaya-Hussein-700347.JPG


Kenyewe kanapiga ya Njano...... Hiyo ni kali zaidi atakuja kukabidhiwa Ridhiwan

Yaani hadi PETE zao eti ni CCM (Green and Yellow), lohh!!!!

Ha ha ha nilikuwa sijaiona hii,
Sikonge naomba uniruhusu niiweke hii kwenye tairi la gari yangu for a week.
 
Nawaomba wahudumu wa bunge wampange Maji marefu (kama akishinda) kiti kando ya Mama Rwakatare (kama akiteuliwa)...

Kwa mtaji huu Maalbino na watoto imekula kwao... kuna mtetezi bungeni!!
 
helcopter.jpg
Daniel Mjema, Same
WAKATI joto la uchaguzi mkuu likizidi kupanda, matukio ya ajabu yanazidi baada ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete kuamua kutumia helikopta tatu kwa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro kukampeni katika jitihada za kufikia maeneo mengi.

Kikwete, ambaye ameanza ziara yake mkoani Kilimanjaro jana, alitumia idadi hiyo ya helkopta tofauti na awali alipokuwa akitumia helikopta mbili na magari, ingawa kabla alikuwa akitumia helikopta moja ambayo iliharibika.

Akianza kampeni kwenye mkoa ambao unaonekana kuwa na upinzani mkubwa dhidi ya CCM, Kikwete alitua kwenye Kijiji cha Ndungu kwenye Jimbo la Same Mashariki saa 7:20 mchana akiwa kwenye moja ya helkopta tatu za msafara wake wa angani.

Mikutano ya mgombea huyo wa CCM, ambaye sasa ni dhahiri anaonekana kuzidiwa na wingi wa mikutano ya kampeni anayoifanya kwa siku, imekuwa ikichelewa kuanza kwa muda uliopangwa kutokana na kuwa mingi na wakati mwingine kufanya mikutano isiyo
rasmi au kutumia muda kusalimia kutokana na mamia ya wananchi kujikusanya
barabarani kutaka wamuone.

Helkopta ya kwanza ilitua saa 6:50 mchana kwenye eneo maalum lililoandaliwa
ikitokea Tanga na mshereheshaji alionekana kutojua chochote kuhusu chombo hicho baada ya kutangaza kuwa Kikwete alikuwa ndani ya helkopta hiyo, lakini baadaye ikafahamika kuwa hakuwemo

Baada ya muda wa dakika 30 ndipo zilipoonekana angani helikopta mbili
zaidi zikifuatana na kuzunguka eneo la mkutano kwa juu huku mgombeahuyo akionekana kwa mbali akiupungia umati mkubwa wa wananchiwaliokusanyika kwenye eneo hilo.

Akihutubia wananchi katika mikutano ya hadhara ya kampeni katikavijiji vya Ndungu, Kisiwani na Same Mjini, Kikwete alisema serikali yake itaongeza kasi yakupambana na magonjwa makubwa ikiwamo malaria kwa lengo la kuifanya Tanzania itangazwe haina malaria ifikapo mwaka 2015.

Alisema ugonjwa wa malaria ndio unaoongoza kwa kuua Watanzania wengi ukifuatiwa na Ukimwi na ndiyo maana serikali yake imeutengenezea kila ugonjwa mpango wa namna ya
kuushughulikia.

Alifafanua kuwa “maisha bora kwa kila Mtanzania" ni pamoja na kuwa na
afya bora.
"Tumekusanya nguvu zetu sana katika maradhi kama ya saratani,
moyo na figo na mwakani tutaanza kushughulikia kansa ya shingo ya
uzazi,” alisema mgombea huyo wa urais.

Kuhusu ugonjwa hatari wa malaria, Kikwete alisema umekuwa ukiua kwa wingi watoto walio na umri chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito na ndio maana serikali imeamua kutoa vyandarua vya bure.

“Mtoto atakayezaliwa leo chandarua chake kipo na atakayezaliwa keshochandarua chake kipo na kina mama wajawazito chandarua cha Sh10,000wanakinunua kwa Sh500; ukitoa pesa zaidi ya hapo wanakuibia,”alisema.

Mbali na mikakati hiyo, serikali imeandaa na inatekeleza mpango wa kumwezesha kila Mtanzania kulala katika chandarua na kwamba mahitaji nivyandarua milioni 14 na ugawaji wake utaanza sasa hadi kufikia Disembamwaka huu.

Kwa mujibu wa mgombea huyo, mpango mwingine utakaoiwezesha Tanzaniakufikia ndoto ya kutokuwa na malaria ifikapo 2015 ni kuua mazalia yambu na mpango huo umekwishaanza mkoani Kagera na utasambaa nchi nzima.

“Mpango mwingine ni kuua viluwiluwi vya Malaria pale vinapozaliwa natayari tumeshawapa fedha Wakyuba na kiwanda kinajendwa Dar esSalaam…tunataka 2015 Tanzania itangazwe haina malaria,” alisisitiza Kikwete.

Mgombea huyo aliwaahidi wananchi wa jimbo hilo kujenga barabara yalami kutoka Same-Kisiwani-Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu yaMoshi-Dar es Salaam na kushughulikia tatizo sugu la maji katika wilaya hiyo.

Katika mikutano hiyo, wagombea ubunge wa majimbo ya Same Mashariki,Anne Kilango Malecela na Dk. David Mathayo walitumia mikutano hiyo kumlilia Kikwete awasaidie kutatua kero zinazoyakabili majimbo hayo.

Kero hizo ni pamoja na barabara za milimani; kupatiwa wataalamu katika kiwanda pekee cha tangawizi kilichopo Mamba Myamba; tatizo sugu la maji kwenye mji wa Same na baadhi ya vijiji na msaada wa chakula cha njaa.

Mgombea huyo ataendelea na ziara yake leo katika majimbo ya Rombo,Vunjo na Moshi mjini ambapo haijafahamika ni maeneo gani hasa atatumiahelkopta na yapi atatumia Helkopta kama alivyofanya kwa siku ya jana.

Chanzo: JK apasua anga kwa helikopta tatu
 
JK amnadi Profesa Maji Marefu Korogwe vijijini leo

jk2.jpg


JK akimnadi mgombea ubunge wa CCM kiti cha Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu mchana huu katika kijiji cha Mashewa kilichoko Korogwe vijijini

jk5.jpg

Bango la Profesa Maji Marefu

Huyu ni Mganga Maarufu wa CCM wameona wampe Ubunge kwa tiketi ya Chama Chao Sasa Je Huko Bungeni na Kazi yake itakuwaje au anakwenda kwa ajili ya kuwaagu wa Bunge kule Bungeni au atasaidia kuleta maendeleo ya Taifa letu??? Hii Nchi sio Gambia Mbunge lazima awe mganga sasa huku tunapokwenda sasa Ni hatari zaid. Wananchi CHAGUA CHADEMA KWA MAENDELEO YAKO. Usikubali kupoteza kura yako kwa kuchagua hii. HATARI NCHI IMESHAUZWA SASA WANATAFUTA KINGA ZA GIZA.​

Maji marefu ni mtaalamu wa dawa za ASILI? Sio mtu wa tunguli.. mbona mazishushia hadhi dawa zetu za asili, wenzetu wachina dawa zao saa hivi zinatumiaka hadi bara ulaya!...
ila huyu mbunge wangu kichekesho kweli eti hajui kiingereza HHAHAHA!!!

USHINDI MWAKA HUU LAZIMA YAANI WA KISHINDO!!! GO.. GO.. GO JAKAYA
 
Tuma ujumbe huu kwa watu 50 thanks

 
Last edited by a moderator:
Anakwenda kutoa "ulinzi wa majini" kwa wabunge wa CCM na Kikwete, kama alivyoahidi sheikh Yahaya.

Ahaaaaaaaaaaaa now i know. Huu ndo ulinzi aliokuwa anauongelea Yahaya Huseni. Sisiemu wana akili hao!
 
Back
Top Bottom