Daniel Mjema, Same
WAKATI joto la uchaguzi mkuu likizidi kupanda, matukio ya ajabu yanazidi baada ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete kuamua kutumia helikopta tatu kwa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro kukampeni katika jitihada za kufikia maeneo mengi.
Kikwete, ambaye ameanza ziara yake mkoani Kilimanjaro jana, alitumia idadi hiyo ya helkopta tofauti na awali alipokuwa akitumia helikopta mbili na magari, ingawa kabla alikuwa akitumia helikopta moja ambayo iliharibika.
Akianza kampeni kwenye mkoa ambao unaonekana kuwa na upinzani mkubwa dhidi ya CCM, Kikwete alitua kwenye Kijiji cha Ndungu kwenye Jimbo la Same Mashariki saa 7:20 mchana akiwa kwenye moja ya helkopta tatu za msafara wake wa angani.
Mikutano ya mgombea huyo wa CCM, ambaye sasa ni dhahiri anaonekana kuzidiwa na wingi wa mikutano ya kampeni anayoifanya kwa siku, imekuwa ikichelewa kuanza kwa muda uliopangwa kutokana na kuwa mingi na wakati mwingine kufanya mikutano isiyo
rasmi au kutumia muda kusalimia kutokana na mamia ya wananchi kujikusanya
barabarani kutaka wamuone.
Helkopta ya kwanza ilitua saa 6:50 mchana kwenye eneo maalum lililoandaliwa
ikitokea Tanga na mshereheshaji alionekana kutojua chochote kuhusu chombo hicho baada ya kutangaza kuwa Kikwete alikuwa ndani ya helkopta hiyo, lakini baadaye ikafahamika kuwa hakuwemo
Baada ya muda wa dakika 30 ndipo zilipoonekana angani helikopta mbili
zaidi zikifuatana na kuzunguka eneo la mkutano kwa juu huku mgombeahuyo akionekana kwa mbali akiupungia umati mkubwa wa wananchiwaliokusanyika kwenye eneo hilo.
Akihutubia wananchi katika mikutano ya hadhara ya kampeni katikavijiji vya Ndungu, Kisiwani na Same Mjini, Kikwete alisema serikali yake itaongeza kasi yakupambana na magonjwa makubwa ikiwamo malaria kwa lengo la kuifanya Tanzania itangazwe haina malaria ifikapo mwaka 2015.
Alisema ugonjwa wa malaria ndio unaoongoza kwa kuua Watanzania wengi ukifuatiwa na Ukimwi na ndiyo maana serikali yake imeutengenezea kila ugonjwa mpango wa namna ya
kuushughulikia.
Alifafanua kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania" ni pamoja na kuwa na
afya bora.
"Tumekusanya nguvu zetu sana katika maradhi kama ya saratani,
moyo na figo na mwakani tutaanza kushughulikia kansa ya shingo ya
uzazi, alisema mgombea huyo wa urais.
Kuhusu ugonjwa hatari wa malaria, Kikwete alisema umekuwa ukiua kwa wingi watoto walio na umri chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito na ndio maana serikali imeamua kutoa vyandarua vya bure.
Mtoto atakayezaliwa leo chandarua chake kipo na atakayezaliwa keshochandarua chake kipo na kina mama wajawazito chandarua cha Sh10,000wanakinunua kwa Sh500; ukitoa pesa zaidi ya hapo wanakuibia,alisema.
Mbali na mikakati hiyo, serikali imeandaa na inatekeleza mpango wa kumwezesha kila Mtanzania kulala katika chandarua na kwamba mahitaji nivyandarua milioni 14 na ugawaji wake utaanza sasa hadi kufikia Disembamwaka huu.
Kwa mujibu wa mgombea huyo, mpango mwingine utakaoiwezesha Tanzaniakufikia ndoto ya kutokuwa na malaria ifikapo 2015 ni kuua mazalia yambu na mpango huo umekwishaanza mkoani Kagera na utasambaa nchi nzima.
Mpango mwingine ni kuua viluwiluwi vya Malaria pale vinapozaliwa natayari tumeshawapa fedha Wakyuba na kiwanda kinajendwa Dar esSalaam
tunataka 2015 Tanzania itangazwe haina malaria, alisisitiza Kikwete.
Mgombea huyo aliwaahidi wananchi wa jimbo hilo kujenga barabara yalami kutoka Same-Kisiwani-Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu yaMoshi-Dar es Salaam na kushughulikia tatizo sugu la maji katika wilaya hiyo.
Katika mikutano hiyo, wagombea ubunge wa majimbo ya Same Mashariki,Anne Kilango Malecela na Dk. David Mathayo walitumia mikutano hiyo kumlilia Kikwete awasaidie kutatua kero zinazoyakabili majimbo hayo.
Kero hizo ni pamoja na barabara za milimani; kupatiwa wataalamu katika kiwanda pekee cha tangawizi kilichopo Mamba Myamba; tatizo sugu la maji kwenye mji wa Same na baadhi ya vijiji na msaada wa chakula cha njaa.
Mgombea huyo ataendelea na ziara yake leo katika majimbo ya Rombo,Vunjo na Moshi mjini ambapo haijafahamika ni maeneo gani hasa atatumiahelkopta na yapi atatumia Helkopta kama alivyofanya kwa siku ya jana.
Chanzo:
JK apasua anga kwa helikopta tatu