Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Kila la heri Klabu zetu Tanzania Simba SC na Yanga FC kutuwakilisha kimataifa. Kikosi cha Yanga kilikuwa kikitua mchana wa leo katika uwanja wa Jomo Kenyatta nchini Kenya tayari kwa safari kuelekea Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya St Louis FC.
Kikosi cha Simba SC kikiwa kimefika salama jioni ya leo nchini Kenya kikisubiri kuelekea nchini Djibouti tayari kuwavaa Gendamarie Internationale FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Kila la heri wawakilishi wetu wa kimataifa.
=====
UPDATES;
Simba na Yanga katika viwanja tofauti vya Djibouti ns Shelisheli wakifanya mazoezi tayari kuwavaa Gendamarie Internationale FC na St Louis FC
Wakati Simba SC ikijiandaa kuwakabili Gendamarie, golikipa Aishi Manula amumia mkono kwenye mazoezini.. pole sana upone haraka