Picha: Mwonekano mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Arusha, utakaotumika kwenye michuano ya AFCON 2027

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Matukio mbalimbali katika picha wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Methusela Ntonda alipokwenda kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Arusha, wakati wa kikao kazi cha mwezi cha maendeleo ya mradi huo.

Ntonda alikuwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa wizara hiyo.




Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya 2027, ambayo pia inajulikana kama AFCON 2027 au CAN 2027, imeratibiwa kuwa toleo la 36 la mashindano ya kandanda ya Afrika yanayoandaliwa kila baada ya miaka miwili na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF). Michuano hiyo mikubwa itaandaliwa na Uganda, Kenya, na Tanzania, Juni na Julai 2027.
 
Chuga wanaendaga kwa mpira lakini?
 
Chuga wanaendaga kwa mpira lakini?
Kwani walienda lini simba au yanga walishaenda arusha alafu uwanja haukujaa watu wasiojua mpira ndio watasema arusha hakuna mashabiki kipindi kile cha michuano ya challenge mechi nyingi za tanzania zilikua zinafanyika sheikh amria abeid arusha bila kusahau arusha ilikua na timu kama ndovu, pallssons, afc na baadae jkt oljoro na zote zilikua ligikuu kipind mpira ni mpira haswa mambo yalikuja kuharibika mpira ulivoingiliwa na matajiri wenye pesa jkt oljoro iliuzwa ndio sasa imekua geita gold watu wa arusha wanapenda sana mpira na hata mechi zikifanyika arusha timu zinaweka viingilio vya juu kuliko mikoa mingine changamoto ya arusha kwa sasa ni kwamba hamna watu wenye hela walioweka nguvu kuinua timu ligi kuu hiv sasa kuna timu mbili daraja la kwanza mbuni na tma stars si ajabu mwakani ukaiona arusha ligi kuu tena
 
Mkuu hii Mbuzi FC na TMA ni timu za Arusha? Na huu uwanja mpya unajengwa maeneo gani hapo Arusha? Asante
 
Mkuu hii Mbuni FC na TMA ni timu za Arusha? Na huu uwanja mpya unajengwa maeneo gani hapo Arusha? Asante
 
Mkuu hii Mbuni FC na TMA ni timu za Arusha? Na huu uwanja mpya unajengwa maeneo gani hapo Arusha? Asante
Yes zote ni timu za arusha
Uwanja mpya unajengwa maeneo ya kisongo karibu na idara ya maji au mradi wa safari city
Ujenzi unaendelea kwa kasi
 

Attachments

  • Screenshot_20241203_132800_Chrome.jpg
    324.2 KB · Views: 12
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…