Pre GE2025 Picha: Nape Nnauye atua mtaani akiwa na nguo za kiraia huku akila ubwabwa na wananchi

Pre GE2025 Picha: Nape Nnauye atua mtaani akiwa na nguo za kiraia huku akila ubwabwa na wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Si hizi ndio nguo anazaaga sasa za kiraia vipi kwani lini alikuwa na gwanda?

Tangu lini mwanasiasa wa Tanzania anaenda kukutana na wananchi anavaa mkofia wa kushona kwa mkono na track suits za mazoezi?

Yaani Nape ni wa kukutana na wananchi na ma Tshirt ya Foma Gold?
 
Sema ndo hivyo tu humu jukwaaani mtu alichukiwa basi inakuwa nongwa; maelezo hayajitoshelezi kuwa alikuwa ana shughuli gani? Kwamba imesemwa wapi kuwa amepeleka mchele? Je, kama ye ndo amekaribishwa tu?
Kwa taarifa yenu, kwa aliyoyafanya huko tangu awe mbunge hakuna hata wa kumtoa........hayo maji, umeme na afya amefanya kweli vijiji vingi tu.
 
Tangu lini mwanasiasa wa Tanzania anaenda kukutana na wananchi anavaa mkofia wa kushona kwa mkono na track suits za mazoezi?

Yaani Nape ni wa kukutana na wananchi na ma Tshirt ya Foma Gold?
Hata suti ni ya kiraia
 
Naelewa mkuu ila hapo kwenye wali wangetia hata maharage na matembele ya kutosha kuboresha lishe.
But who cares afya ya mpiga kura? kwasababu anachokifanya ni maigizo at the end of the day ni wizi wa kura au kama yeye anavyoita "goli la mkono"

Wapigakura wanafanyiwa kiini macho wajione wamechagua kumbe hakuna kitu.
 
Naelewa mkuu ila hapo kwenye wali wangetia hata maharage na matembele ya kutosha kuboresha lishe.
Mkuu bongo tunakula kwa ajili ya ladha. Mambo ya nutrients ni wachache wanajali ndio maana tunabugia ubuyu na kutafuna kashata Ila faida yake mwilini hatuijui zaidi ya kufurahisha mdomo na kuendeleza mifumo ya maisha tuliyoikuta

Labda kama inaongeza nguvu za kiume ndio tunajali na hatujali inaongezaje, cha msingi tuweke heshima..
 
Sema ndo hivyo tu humu jukwaaani mtu alichukiwa basi inakuwa nongwa; maelezo hayajitoshelezi kuwa alikuwa ana shughuli gani? Kwamba imesemwa wapi kuwa amepeleka mchele? Je, kama ye ndo amekaribishwa tu?
Kwa taarifa yenu, kwa aliyoyafanya huko tangu awe mbunge hakuna hata wa kumtoa........hayo maji, umeme na afya amefanya kweli vijiji vingi tu.

Haya ndo MAMBO MENGI anayoyafanya Nape kwenye jimbo lake sio?

Mtama .png
 
Hata suti ni ya kiraia

Serious unafananisha hadhi ya suti na li track la suti la jogging in the name of nguo za kiraia?

Kama zote ni za kiraia kwanini wakienda kuapishwa hawavaagi track suits wanavaa designer suits?

Uko serious?
 
Hivi huwa hela ya kiinus mgongo cha wabunge haitoshi kumanya mtu astaafu ubunge?
 
Haya ndo MAMBO MENGI anayoyafanya Nape kwenye jimbo lake sio?

Kuna makumi ya vijiji mtama, vp umehangaika na kamoja tu hako?!!! Nakushauri tembelea vijiji vingine, hususani vile vya njia ya tandahimba (eg lindwandwali, chiuta, Mandwanga, lipome, nahukahuka, litipu, nyangamara, mbindo, mandwangwa, mnyambe n.k) halafu uje hapa baada ya kujua vilivyokuwa kabla na baada (yaani Sasa)
 
Back
Top Bottom