Operation 255 ilipangwa kufanywa nchi nzima. Na kabla ya katibu mwenezi wa CCM kuapishwa mwenyekiti wa Chadema alikuwa ameshafika Tunduma anajiandaa kuingia katika mikoa mingine iliyobaki kama ratiba yao inavyoeleza.
Sasa ghafla wakasikia katibu kateuliwa na kuapishwa. Wakaanza kwanza kurusha vijembe vya hofu ili aliemteuwa amtengue waendelee na operation zao. Walivyoona mteuaji hawajali, basi wakaamua kuachana na mikutano.
Maana kisiasa ni aibu kwa mtu mwenye chawa wengi mitandaoni kama Mbowe, au Lisu washindwe kujaza watu, alaf mtu ambae wamemtengenezea fitna na majungu bila mafanikio, ajaze watu katika mikutano yake yote.
Ndiomaana wakaamua kukaa pembeni wasubiri mafuriko yake yaishe.