Picha: Rejeta yangu inamwaga maji kwa presha

hp4510

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
7,235
Reaction score
7,392
Wakuu Habari za weekend

Jana nimedrive gari Kwa umbali kama wa kilometres 2,

Nikafungua mfuniko wa rejeta, kilichotokea ni maji kuruka Kwa nguvu Sana kama video inavyoonyesha,

Maswali yangu ni kama ifuatavyo

1 shida ni Rejeta

2 shida ni engine

3 shida ni gasket

4 au shida ni feni zile za kupoza?

Haya maswali 4 ndio mafundi wamesema ndio tatizo kuna mmoja kanambia nishushe injini kabisa

Sasa naomba mawazo kidogo

Hii gari ni NISSANI TEANA 230JM

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Umeunguza gasket. Peleka gereji wabadilishe gasket. Pia mwambie fundi apime rejeta kama ni nzima na pia apime mfuniko.

Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba.

Kila mara unapofanya service ya gari fanya nayafuatayo kulinda mfumo wa upoozaji.

Pima rejeta, pima mfuniko, safisha rejeta na badilisha coolant.
 
Itakuwa ina-SQUIRT baada ya kupigwa mboko sana
 
Niliona kwenye kifuniko kama moshi wa mvuke unatoka
Mwana kulifind…..mwana kuliget!
Mkuu ipo hivii, tumia dashboard yako kusoma gari kama inachemsha au la. Kwenye dashboard mshale wa temperature utakuwa kwenye red kama gari linachemsha kama sivo basi position ya mshale itakuwa around hapo kwenye nusu ya gauge.
Gari iliyounguza cylinder head gasket au kupindisha cylinder head huwa inaingiza upepo kwenye cooling system na dalili yake kuu ni gari kuchemsha na kurudisha maji kwenye reserve tank.
Iwapo pia mfuniko wako wa rejeta ni mbovu basi gari itarudisha maji kwenye reserve tank.
Kabla hujagusa cylinder head au gasket ya cylinder head au rejeta, hakikisha umebadili mfuniko wa rejeta then watch gauge ya temperature kwenye instrumental cluster hapo.
Ni hayo tuu, I hope umeelewa.
 

Thank you so much

Kula bia Kwa bill yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…