Picha: Samia Kings (AY, Madee na Chege ) waongoza kwenye mapokezi ya Rais Samia huko Mkata

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wasaniii wa Bongofleva Madee, AY na Chege (Samia Kings) wameshiriki kwenye shangwe za mapokezi ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Mkata Mkoani Tanga ambako anaanza ziara ya kikazi leo.

Soma Pia:
Screenshot 2025-02-23 155744.png
Screenshot 2025-02-23 155754.png

Screenshot 2025-02-23 155807.png
 
Ambene kashindwa kuvumilia kuside na vyama
 
Wanamuziki wa bongo fleva wanaounda kundi la muziki la Samia Kings ambao ni Chege, Madee na Ay, wakitoa burudani katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkata wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, ambako Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzungumza na wananchi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.

Rais Samia ameanza ziara ya kikazi ya siku saba mkoani Tanga kuanzia leo Februari 23,2025, kwa lengo la kuzungumza na wakazi wa mkoa huo pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Soma pia: Wasanii kujiingiza kwenye siasa na kuwa machawa ipi faida yao kama nao wanashiriki kuingiza wananchi shimoni?

Tayari Rais Samia amezindua Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni saba.

View attachment 3246553
Wacha watafute hela ya kula Aisee! Njaa haimpendezi mtu.
 
Hata Tume haijapuliza kipenga cha kuanza kampeni, Chama Cha Mapinduzi kinaanza kufanya kampeni waziwazi. Halafu CHADEMA wakisema No Reform No Election kuna watu wanawaona hawana akili.

Nchi hii CCM wamefikia hatua hata Sheria walizotunga wao na wabunge wao hawaziheshimu halafu kuna watu wanategemea waende kwenye uchaguzi halafu washinde? Inasikitisha sana.
 
Wasaniii wa Bongofleva Madee, AY na Chege (Samia Kings) wameshiriki kwenye shangwe za mapokezi ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Mkata Mkoani Tanga ambako anaanza ziara ya kikazi leo.

Soma Pia:
Hakuna rangi tutaacha kuona mwaka huu
 
Kama wanafanya hivyo na kulipwa basi imekaa njema maana hao ni wasanii maybe cameos.
 
Bila wasanii mbogamboga ni kama maiti tu.
Huyu bibi lazima atakuwa ni incompetence tu...haiwezekani apigiwe promo kubwa hv kote nchini na machawa wakati kwa muda aliohudumu hiyo nafasi angejiuza mwenyewe!!.
 
Zamani nilikuwa na ule msimamo wa hata unipe nini sitamani sioni 🔊🎼🎶🎵
Lakini sasa nimekuwa mtu mzima nimegundua kwamba hata wapenzi wa Yanga wakilipwa wanaweza kuichezea Simba.
 
Hao wengine sina shida nao ni chawa kitambo. Ila mpaka Ambwene!
 
Back
Top Bottom