Wanamuziki wa bongo fleva wanaounda kundi la muziki la Samia Kings ambao ni Chege, Madee na Ay, wakitoa burudani katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkata wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, ambako Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzungumza na wananchi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.
Rais Samia ameanza ziara ya kikazi ya siku saba mkoani Tanga kuanzia leo Februari 23,2025, kwa lengo la kuzungumza na wakazi wa mkoa huo pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Soma pia:
Wasanii kujiingiza kwenye siasa na kuwa machawa ipi faida yao kama nao wanashiriki kuingiza wananchi shimoni?
Tayari Rais Samia amezindua Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni saba.
View attachment 3246553